Uchaguzi 2020 Binafsi nimpongeza sana Tundu Lissu kugombea Urais 2020

Haya mpeni hizo kura zenu. Tunaoelewa hizi vitu tunajua kinachoendelea, tunaenda na JPM. Na nguvu zetu haziko mitandaoni siku hizi ziko kwa wananchi
Nguvu zipo kwa polisi na mtangaza matokeo + masanduku ya ziada..
 
Kwa hali ilipofikia Tundu Lisu akae kimya asije akatusababishia machafuko kwa taifa, kama binadamu yeyote ni vigumu kuamini kama anaitafuta nafasi ya uraisi pasipo kulipiza kisasi kwa yale yalitendeka.

Vivyo hivyo kwa watawala wetu ni vigumu kuamini kwamba watakaa kimya eti demokrasia ichukue mkondo wake, ni wazi kwamba kuna hatari ya watawala kuamua liwalo na liwe endapo Tundu Lisu ataungwa mkono na hivo kupelekea mkorogano mkubwa kama tunavyo shuhudia kwenye mataifa mengine.

Mimi binafsi nautambua mchango mkubwa wa Mh. Tundu Lisu lakini kwa hali ilipofikia namuomba akae kimya aachane na harakati za kisiasa.

Kuna msemo wa kiswahili unaosema "Ukilikoroga utalinywa"

Nawasilisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
Acha nidhamu ya uoga mkuu, Lissu ameonesha nia ya kupeperusha bendera ya urais na anao uwezo huo, endapo atapitishwa na chama/vyama vya upinzani kugombea nafasi ya urais tumuunge mkono, kwani Lissu ni mzalendo wa kweli wa taifa letu.

Tumeona uelekeo wa michango yake kwa taifa akiwa bungeni na nje ya bunge, Lissu ni mzalendo haswaaa huwezi mlinganisha na jiwe and Co.ltd wanaolazimisha uzalendo baada ya kuliumiza taifa kwa mda mrefu.

Hizo kelele nyingi na kauli za kebehi kuonesha Lissu si mzalendo, ni kibaraka na anatumiwa na mabeberu wasioitakia mema nchi ni kauli za kisiasa toka kwa walioshindwa na kukosa hoja madhubuti ya kumkabili Lissu, ila raia tunajua na kuelewa mtetezi wa kweli wa rasilimali zetu ni nani,

Hofu yako ni visasi endapo Lissu atapata nafasi ya kuongoza nchi yetu, ila Lissu si mtu wa visasi kama unavyo dhani, na kwa nini awe na visasi ni mambo gani mabaya mliotendea mpaka muwe na hofu kiasi hicho? Je? Wewe ni miongoni mwa Wasiyojulikana waliotaka kuondoa uhai wake kwa risasi zaidi 38? Wahenga walisema muovu hukimbia hata kivuli chake...! Lissu akipata nafasi ya kuombea kiti cha urais, tumuunge mkono anatufaa sana watanzania.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
2020 anapita atakua Raisi wako anakuja kuwafundisha ccm siasa za kisanyansi, Tafuta kwenye ahadi zake zote Wapi Rais Magufulia aliahidi kukamata wapinzani wake kuwaweka ndani?Wapi aliahidi kodi za kero wapi aliahidi ugumu wa maisha kwa kila mtanzania?
Unaota ndoto za mchana wanaziita alinacha
 
Haya mpeni hizo kura zenu. Tunaoelewa hizi vitu tunajua kinachoendelea, tunaenda na JPM. Na nguvu zetu haziko mitandaoni siku hizi ziko kwa wananchi
Zile za kununua wabunge mil 60
 
Tuache ushabiki wa kisiasa, tuwe wazalendo wa kweli! Tusiende mbali sana kutoa historia! Wasimame tu mkulu na Lisu dakika 5 tu za kujieleza, nafikiri Lisu atamgonga za uso mkuu za kutosha, kama ni nundu basi mkuu atavimba uso mzima!
Lukoma sasa si wakati wa ngonjera ndio zimetufikisha hapa. Tunataka historia ya utendaji ambayo kwa JPM imejidhihiri kwa zaidi ya miaka 20 serikali.

Yeye ndiye mbunifu wa ujenzi wa barabara za lami kwa pesa za ndani ambapo alianza na bajeti ya tsh 1.2bn lakini kufikia leo nchi nzima inapitika. Thats why we trust him.

Lissu anakumbukumbu ipi yenye alama kwenye maendeleo endelevu ya Watanzania??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
K

Kwani Lisu amewahi kuwa waziri?
 
Kabla ya kufikiria kugombea Urais atuambie fadhila za gharama ya matibabu yake ambayo mpaka sasa hayajulikani ni kiasi gani atalipa je? Ni hatari kwa mtu anayetafuta kuwa rais wa nchi akawa amelipiwa matibabu na watu tunao jua wana maslahi yao ya kificho na yasiyo ya kificho hapa nchini.

Atajiepusha vipi na tuhuma za kuwa rais ambaye ni pandikizi la walipia matibabu ughaibuni na kutuondolea shaka kuwa hatatumikia na kutumiwa kwa masilahi za wafadhili wa matibabu.
Lissu alikata bima ya matibabu kWa hela tulizomchangia then hana njaa kama hapo Lumumba kila kitu nyinyi pesa za maafa korosh yaa ni utapeli tuu nyie
 
Hapa jamvini ni mahali pazuri kusema ukweli, kwa maoni yangu Tindua Risasi amekwisha kisiasa kiakili kisaikolojia na kimwili. Si kosa lake waliompiga risasi kujaribu kumuua wamemmaliza! Ndani ya ubongo wake Tindua amejaa kisasi as human nature unapoumizwa na bahati mbaya hamjui aliemshambulia hivyo akipata mamlaka atarusha mawe ovyo ovyo bila kujali litakaempata kwani jamii nzima ilikuwa wapi kumlinda asishambuliwe? Kisaikolojia amekwisha manake hata akisikia mlio wa pancha ya tairi la gari atazirai na kulazwa atajua anamiminiwa tena risasi, kimwili ndo kabisa mwili umeungwa ungwa mno hawezi kupanda ngazi ghorofa ishirini au kupiga push up jukwaani, ninamuonea huruma kama binadamu mwenzangu ila amepoteza mvuto na sifa za kimwili na kiakili kumudu kazi ngumu ya urais wa nchi, nafikiri walio karibu nae wamsaidie ushauri nasaha apumzike siasa zimemkataa sababu ya jazba alee wanawe, na wapinzani wote kimbilieni kwa Mh JK anajua mno kudeal na siasa zenu za maji taka na kuvumilia uchokozi wa kisiasa! Mimi ni modern CCM member nasimama kwenye ukweli daima! Pia namuonya sana yule mjinga asie na elimu ya kilichopo kwa wenzetu huyu mjinga anataka kugeuza bongo kuwa Burundi na Congo kwa vita na mauaji kwa kugusa suala nyeti la muhula wa urais wabongo mkemeeni aachane na ushetani wake manake mkianza kutinduana hamna pa kukimbilia! Watu wa idodomya tunajua warangi wengi hawana akili zaidi ya wanaume kuuza mahindi na kina mama wao wanajua tabia zao! Bongo ni yetu sote mkemeeni kwa nguvu zote yule bwana Mkamia Maji Hayanywi, majuto ni mjukuu!
Bora tutinduane tukose pa kukimbilia mim nikipewa mk 47 nikamwage pale Lumumba hata bure tuu
 
Kwa hali ilipofikia Tundu Lisu akae kimya asije akatusababishia machafuko kwa taifa, kama binadamu yeyote ni vigumu kuamini kama anaitafuta nafasi ya uraisi pasipo kulipiza kisasi kwa yale yalitendeka.

Vivyo hivyo kwa watawala wetu ni vigumu kuamini kwamba watakaa kimya eti demokrasia ichukue mkondo wake, ni wazi kwamba kuna hatari ya watawala kuamua liwalo na liwe endapo Tundu Lisu ataungwa mkono na hivo kupelekea mkorogano mkubwa kama tunavyo shuhudia kwenye mataifa mengine.

Mimi binafsi nautambua mchango mkubwa wa Mh. Tundu Lisu lakini kwa hali ilipofikia namuomba akae kimya aachane na harakati za kisiasa.

Kuna msemo wa kiswahili unaosema "Ukilikoroga utalinywa"

Nawasilisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
unamaanisha tuendelee na jiwe etiee

kama mbwai mbwai tu wacha aje kieleweke

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom