Uchaguzi 2020 Binafsi nimpongeza sana Tundu Lissu kugombea Urais 2020

A funny way of reasoning. Kwa hiyo wanaopelekwa India kila kesho na sirikari wanakuwa na mkataba kuishangilia sirikari?

Funny way of understanding issues, hao wa India na kwengineko wa kupelekwa na,serikali, wanakuwa katika mkono salama wa serikali. Mtu aliyefikia nyadhifa za Lissu hawezi kuwa stray bila kuleta changamoto katika suala zima la usalama wa Taifa. Ni kujidanganya ukisema hajui baadhi ya siri muhimu za nchi. Je anabehave vipi huko alipo katika kuhangaika kwake? Hazifanyi ni chambo cha kufikia malengo yake. Nikuulize unafikiri kwa nini hao wazungu wanamuona ni asset kwao? Lissu kwa sasa ni Asset kwa wazungu na Liability nchi.
 
Tuache ushabiki wa kisiasa, tuwe wazalendo wa kweli! Tusiende mbali sana kutoa historia! Wasimame tu mkulu na Lisu dakika 5 tu za kujieleza, nafikiri Lisu atamgonga za uso mkuu za kutosha, kama ni nundu basi mkuu atavimba uso mzima!
 
Tunapoanza mwaka mpya tunatafakari yaliyopita na kuona tutaenenda vipi.

Yaliyopita yameonysha upo mchuano wa kifikra na kitawala kwa watu Hawa wawili.

Kwa mtazamo wako, yapi mazuri Yao, yapi mabaya Yao na unadhani wakikutana Uwanja huru wa kisiasa mwakani 2020 Nani ataibuka mshindi? It's two years battle starting from now 2019

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tunapoanza mwaka mpya tunatafakari yaliyopita na kuona tutaenenda vipi.

Yaliyopita yameonysha upo mchuano wa kifikra na kitawala kwa watu Hawa wawili.

Kwa mtazamo wako, yapi mazuri Yao, yapi mabaya Yao na unadhani wakikutana Uwanja huru wa kisiasa mwakani 2020 Nani ataibuka mshindi? It's two years battle starting from now 2019

Sent using Jamii Forums mobile app
mabaya ya Lissu unayapimahe kwani hajawahi kushika nyazifa katika serikai ya ccm.

in whetever way, Lissu is 1000miles ahead.
 
Kabla ya kufikiria kugombea Urais atuambie fadhila za gharama ya matibabu yake ambayo mpaka sasa hayajulikani ni kiasi gani atalipa je? Ni hatari kwa mtu anayetafuta kuwa rais wa nchi akawa amelipiwa matibabu na watu tunao jua wana maslahi yao ya kificho na yasiyo ya kificho hapa nchini.

Atajiepusha vipi na tuhuma za kuwa rais ambaye ni pandikizi la walipia matibabu ughaibuni na kutuondolea shaka kuwa hatatumikia na kutumiwa kwa masilahi za wafadhili wa matibabu.
Acha fadhila ya matibabu ya Lisu, Tanzania inafadhiliwa mpaka bajeti ya nchi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
"Eti Mimi Jiwe"...Khaaaakh!!!..na hao kina Trump ndio wasemaje?!
tenor-4.gif
 
2020 kwa Tundu Lissu atajisumbua bure tu labda ajaribu 2025
 
=wanaufipa.

2020 kwa Tundu Lissu atajisumbua bure tu labda ajaribu 2025
NATAKA TUCHAMBUE AHADI CHACHE KATI YA 100 ZA MH RAIS KWENYE CAMPANI ZAKE KISHA
TOASABU YA KWANINI LISSU TUSIMPE NCHI?

1. MAJI-Kuboresha huduma za maji safi na salama kwa wananchi waishio vijijini na mijini,kukamilisha miradi mikubwa ya maji,kupanua miradi ya kitaifa katika meneo mbalimbali nchini kwa kuchimba visima virefu,kujenga mabwawa katika mikoa yenye ukame. Kuanzisha mfuko wa maji wa taifa (Nationa water Investment Fund) kwa ajili ya kuharakisha ujenzi wa miradi ya maji nchini. Pia ameahidi serikali yake kushirikiana na sekta binafsi katika kujenga miundombinu ya uondoshaji wa maji taka kwa mfumo wa ubia ili uendane na kasi ya ukuaji wa miji yetu.


2. ELIMU-Yeye na Chama Chake wanaamini elimu bora ina nafasi ya kipekee katika kufanikisha ujenzi wa misingi ya uchumi wa kisasa wa taifa linalojitegemea. Kwa kutambua ukweli huu,serikali ijayo ya CCM chini yake itaipa elimu umuhimu wa kipekee ili kuhakikisha inakidhi mahitaji ya sasa ya nchi kwa kumuandaa kila mtanzania kukabiliana na changamoto zinazomzunguka. Kulipa madeni yote ya walimu na kuboresha maslahi na makazi yao pamoja na kuanzisha tume ya walimu itakayosimamia maendeleo ya walimu kote nchini ikiwemo kupandishwa madaraja kwa wakati.
Kumaliza tatizo la madawati na upungufu wa vitabu vya kujifunza na kufundishia pamoja na kutoa elimu bila ada kuanzia ngazi ya msingi hadi sekondari. Kujenga vyuo vya ufundi stadi VETA kila wilaya.


Kurekebisha utaratibu wa utoaji mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu ili kila mwanafunzi anayestahili apate bila usumbufu na kwa wakati.Kuhakikisha ujenzi wa vyuo vikuu vikubwa 2; Chuo Kikuu Cha Kilimo na Sayansi Shirikishi Cha Mwl.J.K. Nyerere (Butiama-Mara) na Chuo Kikuu Cha Sayansi Za Madini Shinyanga.


3. AFYA-Kuongeza idadi ya waganga na wauuguzi pamoja na kuimarisha upatikanaji wa dawa na vifaa tiba katika vituo vyote vya tiba nchini.Kuboresha maslahi ya watumisha wa sekta ya afya kwa kuwalipa mishahara bora,kuwajengea nyumba ili kuwapa motisha ya kufanya kazi.


Serikali ya CCM chini ya MAGUFULI itwaweka utaratibu utakaowawezesha wananchi wote kuwa na bima za afya ili wamudu gharama za matibabu. Kukamilisha ujenzi wa zahanati kwa kila kijiji,kituo cha afya kila kata,hospitali kila wilaya na hospitali ya rufaa kwa kila mkoa. Tutaendelea kupunguza kwa kasi zaidi vifo vya mama na mtoto ili ikiwezekana kuvimaliza kabisa.Tutaanzisha pia mamlaka ya kudhibiti na kuzuia dawa za kulevya


4. KUKUZA VIWANDA-Kujenga viwanda mama na kuimarisha vilivyopo. Kuhamasisha sekta binafsi kuanzisha viwanda vikubwa na vya kati na kuweka utaratibu wa kuvilinda dhidi ya bidhaa zisizo na ubora zinazoingia nchini kinyume na utaratibu. Kujenga mazingira rafiki yatakayowezesha kupunguza gharama za uwekezaji na uendeshaji wa viwanda.Kuanzisha viwanda vya msingi vinavyotumia malighafi ya chuma na makaa katika maeneo ya Liganga na Mchuchuma.


5. USAFIRISHAJI NA UCHUKUZI
Barabara-Tutaimarisha mfuko wa barabara,kuboresha mfumo wa ufuatiliaji na kuanzisha wakala utakaosimamia kazi za ujenzi na matengenezo ya barabara za miji,majiji na halmashauri ambazo ziko chini ya TAMISEMI. Tutamalizia ujenzi wa barabara kuu za lami zenye urefu wa kilometa 2,358 na kujenga barabara mpya za lami zenye urefu wa kilometa 3,419 zitakazounganisha mikoa na wilaya zote nchini. Kukamilisha ujenzi wa flyovers katika jiji la Dar. Tutawashirikisha wakandarasi wadogo wadogo wa kitanzania wanaoonesha nia ya kushiriki kazi kubwa za ujenzi wa barabara ili kuwajengea uwezo na kuwapatia fursa za kushiriki katika sekta ya ujenzi.


Reli-Tutashirikiana na sekta binafsi kuanza na kukamilisha ujenzi wa reli zifuatazo kwa kiwango cha kimataifa (standard gauge); Dar-Tabora-Mwanza/Kigoma; Uvinza-Msongati(Burundi); Isaka-Kigali(Rwanda); Mtwara-Songea-Mbambabay(na matawi ya kwenda Mchuchuma na Liganga);Tanga-Arusha-Musoma na Kaliua-Mpanda-Karema. Kuyajengea uwezo mashirika yetu ya reli ya TRL na TAZARA ili yatoe huduma bora na kwa ufanisi.


Usafiri wa majini- Kuimarisha miundombinu ya usafiri wa majini kwa kuimarisha miundombinu katika bandari za Zanzibar, Dar, Mtwara,Tanga,Mafia,Mwanza,Kigo ma,Bukoba,Kyela na Musoma. Kununua meli mpya za abiria na mizigo katika ziwa Victoria, Tanganyika na Nyasa.


Usafiri wa anga-Kukamilisha ujenzi wa viwanja vya Dar,Zanzibar,Kigoma,Shinyanga, Dodoma,Mwanza,Lindi,Tanga,Geit a pamoja na ukarabati wa viwanja vya Iringa,Njombe,Simiyu,Musoma,Mo shi na Arusha. Kushirikiana na sekta binafsi kuliimarisha shirika letu la ndege la Taifa.


6. NISHATI-Kuongeza uzalishaji na upatikanaji wa umeme wa uhakika na gharama nafuu nchini pamoja na usambazaji wa umeme vijijini ili 60% ya watanzania wawe na umeme wa uhakika ifikapo 2020. Tutahimiza matumizi ya gesi asilia katika matumizi ya nyumbani na viwandani ili kupunguza matumizi ya kuni na mkaa hivyo kuhifadhi mazingira.


7.UWEZESHAJI WANANCHI KIUCHUMI:Serikali ya CCM awamu ya 5 chini ya MAGUFULI itwawawezesha wananchi kiuchumi kwa kuhakikisha kuwa: Inatenga milioni 50 kwa kila kijiji na kila mtaa kama mfuko wa mzunguzko kwa ajili ya kuwakopesha vijana na wanawake wajasiriamali kupitia vikundi; kutenga maeneo maalumu katika kila halmashauri kwa ajili ya wafanyabiashara ndogondogo kwa kuyajengea miundombinu yote muhimu;Kuondoa kero za ushuru na kodi zinazotozwa kwao.Kuhakikisha 30% ya zabuni za manunuzi ya halmashauri kwa ajili ya kampuni ndogo zinazomilikiwa na vijana na wanawake katika halmashauri husika.


8. MAHAKAMA MAALUM YA MAKOSA YA RUSHWA NA UHUJUMU UCHUMI
-Mahakama hii itaharakisha uchunguzi na utoaji hukumu kwa makosa ya Rushwa,Ufisadi,Ukwepaji kodi na yote yanayotambulika kama uhujumu uchumi.









1.-Laptop Kwa kila Mwalimu

3.-Mil 50 kila kijiji

4.- Kushusha PAYE mpaka 11%

5.-Barbara ya Karatu Mbulu kujengwa Kwa Lami

6. Kufufua viwanda nchi nzima

7.-atanunua Meli mbili kubwa kuliko MV Bukoba

8.- Elimu Bure mpaka Secondary

9.-Atajenga daraja ziwani Victoria busisi to kingongofery watu watavuka bure akiwa sengerema
 
2020 kwa Tundu Lissu atajisumbua bure tu labda ajaribu 2025
2020 anapita atakua Raisi wako anakuja kuwafundisha ccm siasa za kisanyansi, Tafuta kwenye ahadi zake zote Wapi Rais Magufulia aliahidi kukamata wapinzani wake kuwaweka ndani?Wapi aliahidi kodi za kero wapi aliahidi ugumu wa maisha kwa kila mtanzania?
 
21 Reactions
Reply
Back
Top Bottom