Uchaguzi 2020 Binafsi nimpongeza sana Tundu Lissu kugombea Urais 2020

Haya mpeni hizo kura zenu. Tunaoelewa hizi vitu tunajua kinachoendelea, tunaenda na JPM. Na nguvu zetu haziko mitandaoni siku hizi ziko kwa wananchi
Kipi kinaendelea funguka acha woga
 
Kwa hali ilipofikia Tundu Lisu akae kimya asije akatusababishia machafuko kwa taifa, kama binadamu yeyote ni vigumu kuamini kama anaitafuta nafasi ya uraisi pasipo kulipiza kisasi kwa yale yalitendeka.

Vivyo hivyo kwa watawala wetu ni vigumu kuamini kwamba watakaa kimya eti demokrasia ichukue mkondo wake, ni wazi kwamba kuna hatari ya watawala kuamua liwalo na liwe endapo Tundu Lisu ataungwa mkono na hivo kupelekea mkorogano mkubwa kama tunavyo shuhudia kwenye mataifa mengine.

Mimi binafsi nautambua mchango mkubwa wa Mh. Tundu Lisu lakini kwa hali ilipofikia namuomba akae kimya aachane na harakati za kisiasa.

Kuna msemo wa kiswahili unaosema "Ukilikoroga utalinywa"

Nawasilisha.

Sent using Jamii Forums mobile app

..Tundu Lissu siyo mtu wa vurugu au visasi.

..siku zote ameendesha harakati zake kwa kufuata sheria na taratibu za nchi hii.

..huyu bwana amepigwa na kunyanyaswa muda mwingi wakati akitetea wanyonge lakini hajawahi kumlipizia kisasi mtu yeyote yule.
 
Kwa hali ilipofikia Tundu Lisu akae kimya asije akatusababishia machafuko kwa taifa, kama binadamu yeyote ni vigumu kuamini kama anaitafuta nafasi ya uraisi pasipo kulipiza kisasi kwa yale yalitendeka.

Vivyo hivyo kwa watawala wetu ni vigumu kuamini kwamba watakaa kimya eti demokrasia ichukue mkondo wake, ni wazi kwamba kuna hatari ya watawala kuamua liwalo na liwe endapo Tundu Lisu ataungwa mkono na hivo kupelekea mkorogano mkubwa kama tunavyo shuhudia kwenye mataifa mengine.

Mimi binafsi nautambua mchango mkubwa wa Mh. Tundu Lisu lakini kwa hali ilipofikia namuomba akae kimya aachane na harakati za kisiasa.

Kuna msemo wa kiswahili unaosema "Ukilikoroga utalinywa"

Nawasilisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
We unafikiri hao waliomtendea ubaya watasalimika?? Hukumu yao yaja haiko mbali

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Harakati za LISSU alianza zamani sana na ndie alieshinikiza serikali kuheshimu mchango wa wachimbaji wadogo na hadi leo matunda yake yanaonekana.

Nakumbuka vema sana hili sakata. Nyumba ya Lissu ilipekuliwa sana akiwa nje ya nchi kikazi. Walikuwa wanatafuta mkanda wa video ambao mhe. Mrema alisema anao, wa matingatinga yalivyokuwa nayafukia wachimbaji wadogo wadogo wa madini. Wakili Lissu ni mpiganaji wa siku nyingi sana.

Huyu jamaa ametoka mbali sana ni kichwa sana na ameanza kuwatetea wanyonge long time

Lissu akasaidia pia kushinda kesi za wananchi wanyonge 366 katika kipindi cha miezi minne tu. Hawa ni wananchi waliokuwa wakiishi pembezoni mwa migodi kabla ya kuswekwa ndani kwa kosa la kuvamia migodi hiyo. Lissu aliwatetea bure wananchi hawa mafukara na baada ya ushindi wa kesi hizo akatamka-"Uwekezaji umegeuka kuwa unyama Tanzania". Lissu akaonekana ni mtu asiye na uzalendo na taifa lake kwa kuwasema vibaya wawekezaji ambao serikali ilikuwaikidai walikuwa wakiliingizia taifa mapato makubwa. Hata hivyo, kwa wananchi hao wanyonge, Lissu alionekana ni Mfalme.

Lissu aliendelea na jitihada zake kuwasaidia wananchi waliokuwa wakinyanyasika migodini huku akiacha wateja wenye fedha nyingi Dar Es Salaam. Kwa Lissu, hakuna kitu kinamuuma moyoni mwake kama akiona mnyonge ana haki lakini anaonewa. Lissu kamwe hawezi kukaa kimya kuona hali hiyo ikiendelea.

Jitihada hizi zikamfanya Lissu azidi kukorofishana na serikali mara kwa mara. Serikali ikamwita ni mchochezi anaechochea wananchi kuwachukia wawekezaji wa Barrick ambao serikali ilikuwa ikidai ni wawekezaji wazuri waliokuwa wakiliingizia taifa pato kubwa.

Lissu amekuwa mstari wa mbele kwenye harakati za kutetea sekta ya madini nchini. Kwa miongo zaidi ya miwili amekuwa akipambana na wawekezaji wazungu waliokuwa wakikingiwa kifua na serikali ya awamu ya tatu na ya nne na kuonekana yeye si mzalendo.

Alikuwa ni mmoja wa waliopinga hadharani na kwenye maandiko yake, sheria ya madini ya mwaka 1998 na ya 2010 kwa hoja kwamba zinawatajirisha wawekezaji wazungu na kutuachia watanzania mashimo tu na umaskini mkubwa wakati Mungu aliibariki nchi hii kwa kuipa madini mengi.

Hoja hizi zilikuwa zikikejeriwa na wabunge wa CCM ambao walikuwa wakiipitisha miswada hii kutokana na wingi wao bungeni. Aidha, Lissu alipinga vikali kupitishwa na bunge sheria zote za madini kwa hati ya dharura mwaka 2015 na 2017.

Licha ya jitihada hizi kubwa za kuwapigania wananchi wanyonge na maskini huku wengi akiwatetea mahakamani bure na kupambana vikali na wawekezaji wa makampuni ya madini ambayo yeye miaka yote amekuwa akiyaita ni ya wezi wanaotuibia madini yetu na kunyanyasa wananchi migodini, Lissu anaonekana kwenye macho ya baadhi ya watu kwamba si mzalendo bali ni "kibaraka anaetumiwa na wazungu asieitakia mema nchi yetu". 2020 huyu jamaa anatufaa sana.
na alikuwa anatetea wazungu kuendelea kuchukua makinikia
 
Amepona??

Maana katiba ambayo yeye anaijua vzr inasema miongoni mwa sifa za mtu kugombea urais wa nchi yetu ni kuwa na AKILI TIMAMU asiyesumbuliwa na MARADHI YA AKILI AU MWILI.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Iwapo Tundu LIssu atagombania nafasi ya Uraisi kupitia United Front atashinda kwa "Landslide"..eeMungu endelea kumpa baraka zako apone haraka..timu imekamilika.
 
Kabla ya kufikiria kugombea Urais atuambie fadhila za gharama ya matibabu yake ambayo mpaka sasa hayajulikani ni kiasi gani atalipa je? Ni hatari kwa mtu anayetafuta kuwa rais wa nchi akawa amelipiwa matibabu na watu tunao jua wana maslahi yao ya kificho na yasiyo ya kificho hapa nchini.

Atajiepusha vipi na tuhuma za kuwa rais ambaye ni pandikizi la walipia matibabu ughaibuni na kutuondolea shaka kuwa hatatumikia na kutumiwa kwa masilahi za wafadhili wa matibabu.
 
A funny way of reasoning. Kwa hiyo wanaopelekwa India kila kesho na sirikari wanakuwa na mkataba kuishangilia sirikari?
 
Similar Discussions

21 Reactions
Reply
Back
Top Bottom