Uchaguzi 2020 Binafsi nimpongeza sana Tundu Lissu kugombea Urais 2020

Zanaco

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
1,621
1,581
Harakati za LISSU alianza zamani sana na ndie alieshinikiza serikali kuheshimu mchango wa wachimbaji wadogo na hadi leo matunda yake yanaonekana.

Nakumbuka vema sana hili sakata. Nyumba ya Lissu ilipekuliwa sana akiwa nje ya nchi kikazi. Walikuwa wanatafuta mkanda wa video ambao mhe. Mrema alisema anao, wa matingatinga yalivyokuwa nayafukia wachimbaji wadogo wadogo wa madini. Wakili Lissu ni mpiganaji wa siku nyingi sana.

Huyu jamaa ametoka mbali sana ni kichwa sana na ameanza kuwatetea wanyonge long time

Lissu akasaidia pia kushinda kesi za wananchi wanyonge 366 katika kipindi cha miezi minne tu. Hawa ni wananchi waliokuwa wakiishi pembezoni mwa migodi kabla ya kuswekwa ndani kwa kosa la kuvamia migodi hiyo. Lissu aliwatetea bure wananchi hawa mafukara na baada ya ushindi wa kesi hizo akatamka-"Uwekezaji umegeuka kuwa unyama Tanzania". Lissu akaonekana ni mtu asiye na uzalendo na taifa lake kwa kuwasema vibaya wawekezaji ambao serikali ilikuwaikidai walikuwa wakiliingizia taifa mapato makubwa. Hata hivyo, kwa wananchi hao wanyonge, Lissu alionekana ni Mfalme.

Lissu aliendelea na jitihada zake kuwasaidia wananchi waliokuwa wakinyanyasika migodini huku akiacha wateja wenye fedha nyingi Dar Es Salaam. Kwa Lissu, hakuna kitu kinamuuma moyoni mwake kama akiona mnyonge ana haki lakini anaonewa. Lissu kamwe hawezi kukaa kimya kuona hali hiyo ikiendelea.

Jitihada hizi zikamfanya Lissu azidi kukorofishana na serikali mara kwa mara. Serikali ikamwita ni mchochezi anaechochea wananchi kuwachukia wawekezaji wa Barrick ambao serikali ilikuwa ikidai ni wawekezaji wazuri waliokuwa wakiliingizia taifa pato kubwa.

Lissu amekuwa mstari wa mbele kwenye harakati za kutetea sekta ya madini nchini. Kwa miongo zaidi ya miwili amekuwa akipambana na wawekezaji wazungu waliokuwa wakikingiwa kifua na serikali ya awamu ya tatu na ya nne na kuonekana yeye si mzalendo.

Alikuwa ni mmoja wa waliopinga hadharani na kwenye maandiko yake, sheria ya madini ya mwaka 1998 na ya 2010 kwa hoja kwamba zinawatajirisha wawekezaji wazungu na kutuachia watanzania mashimo tu na umaskini mkubwa wakati Mungu aliibariki nchi hii kwa kuipa madini mengi.

Hoja hizi zilikuwa zikikejeriwa na wabunge wa CCM ambao walikuwa wakiipitisha miswada hii kutokana na wingi wao bungeni. Aidha, Lissu alipinga vikali kupitishwa na bunge sheria zote za madini kwa hati ya dharura mwaka 2015 na 2017.

Licha ya jitihada hizi kubwa za kuwapigania wananchi wanyonge na maskini huku wengi akiwatetea mahakamani bure na kupambana vikali na wawekezaji wa makampuni ya madini ambayo yeye miaka yote amekuwa akiyaita ni ya wezi wanaotuibia madini yetu na kunyanyasa wananchi migodini, Lissu anaonekana kwenye macho ya baadhi ya watu kwamba si mzalendo bali ni "kibaraka anaetumiwa na wazungu asieitakia mema nchi yetu". 2020 huyu jamaa anatufaa sana.
 
Wazalendo wa mashoga na wapigaji madili wakuu nyie mashetani wa kuzimu.

MAGUFULI SHIKILIA PAPO HAPO BABA, MAJIZI YANAFARAKANA HUKU SABABU YANALIPA KODI BILA KUPENDA, YAMEZIBIWA MIANYA YA MADILI NA MAGENDO NA YAMEKOSA VIROBA MITAANI.
Lissu anatosha sana Urais JMT.

Imagine, Lissu Rais, Zitto waziri Mkuu, Membe Makamo wa Rais.

Nchi itakua chini ya Wazalendo wa kweli sio wakuigiza

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa hali ilipofikia Tundu Lisu akae kimya asije akatusababishia machafuko kwa taifa, kama binadamu yeyote ni vigumu kuamini kama anaitafuta nafasi ya uraisi pasipo kulipiza kisasi kwa yale yalitendeka.

Vivyo hivyo kwa watawala wetu ni vigumu kuamini kwamba watakaa kimya eti demokrasia ichukue mkondo wake, ni wazi kwamba kuna hatari ya watawala kuamua liwalo na liwe endapo Tundu Lisu ataungwa mkono na hivo kupelekea mkorogano mkubwa kama tunavyo shuhudia kwenye mataifa mengine.

Mimi binafsi nautambua mchango mkubwa wa Mh. Tundu Lisu lakini kwa hali ilipofikia namuomba akae kimya aachane na harakati za kisiasa.

Kuna msemo wa kiswahili unaosema "Ukilikoroga utalinywa"

Nawasilisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa hali ilipofikia Tundu Lisu akae kimya asije akatusababishia machafuko kwa taifa, kama binadamu yeyote ni vigumu kuamini kama anaitafuta nafasi ya uraisi pasipo kulipiza kisasi kwa yale yalitendeka.

Vivyo hivyo kwa watawala wetu ni vigumu kuamini kwamba watakaa kimya eti demokrasia ichukue mkondo wake, ni wazi kwamba kuna hatari ya watawala kuamua liwalo na liwe endapo Tundu Lisu ataungwa mkono na hivo kupelekea mkorogano mkubwa kama tunavyo shuhudia kwenye mataifa mengine.

Mimi binafsi nautambua mchango mkubwa wa Mh. Tundu Lisu lakini kwa hali ilipofikia namuomba akae kimya aachane na harakati za kisiasa.

Kuna msemo wa kiswahili unaosema "Ukilikoroga utalinywa"

Nawasilisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hii nchi ni yawatawala tangu lini?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom