Elections 2015 Binafsi nasherehekea kuondoka Kikwete na siyo kuapishwa Magufuli

binafsi nimefurahi sana tena sana rais asiye jitambua ameondoka
raisi asiye tofautisha wapi yupo kichama na wapi yupi ki nchi
rais ambaye yeye hata sehemu ya kwenda mkurugenzi anakwenda yeye
rais ambaye amechochea udini kwa kiasi kikubwa sasa hivi taasisi nyingi za serikali udini udini {wakurugenzi wengi are muslims mfano nssf Christians hupati kazi kwa sasa jaribu}
rais ambaye watoto wake na familia yake wanajiona kuwa na power Zaidi ya mawaziri na viongozi wengine
 
Zote hizo ni hasira za kushindwa na mtalia sana
Mkuu kama ni kulia tutalia wote hakuna hospitali ya wanaCCM pekee, au nauli ya daladala ya wana CCM ni tofauti na ya ACT-Wazalendo.

au mwenzetu ukienda kwenye bucha ukionyesha kadi ya CCM huwa unapunguziwa bei?
 
Subiri nikishaapishwa kama Magufuli....Magufuli akiamua sasa hivi anajipendekeza fasta anakwepia pipa mpaka DC....ila mambo hayo wanayo waswahili tu....

Thubutu ujipeleke tu kumuona Obama bila mualiko rasmi. White House utaiona paa tu kama anavyoiona Ikulu Lowassa, kama anahamu hata ya kupita njia ile.
 
Thubutu ujipeleke tu kumuona Obama bila mualiko rasmi. White House utaiona paa tu kama anavyoiona Ikulu Lowassa, kama anahamu hata ya kupita njia ile.
Mwambie leo Kikwete amwalike Obama kama hata kusikilizwa atasikilizwa.
 
Thubutu ujipeleke tu kumuona Obama bila mualiko rasmi. White House utaiona paa tu kama anavyoiona Ikulu Lowassa, kama anahamu hata ya kupita njia ile.
Mswahili alikwenda US kwa mambo mengine kabisa baadae akaomba kuonana na Obama akakubaliwa...hakukuwa na mwaliko kama unavyofikiri....

Hivi ile ofisi ya waziri mkuu si ipo ndani ya maeneo ya ikulu..ama? Kuna kitu gani Lowassa hakijui mle?

Kwanini Mswahili alimualika Lowassa kuonana na Obama Ikulu-Dsm akamsahau Magufuli?...
 
Kama kuna kitu kibaya alicho waachia Watanzania ambacho binafsi nachukia ni kauli ya kibaguzi dhidi ya watanzania walioitwa wa kaskazini ambao kwa mujibu wa kauli za wapambe wake hawastahili kutoa mtu wa kuliongoza Taifa hili.
Kauli hii itakuwa na athri za muda mrefu na sioni wa kuifuta katika mawazo ya Wataznia.
 
If I speak I will speak a lot let me spear my words until further
times. Within a month if not three months time I will be able to talk on this topic otherwise at the moment am puzzled.

Take all the time you need.
 
Kwa wachangiaji kwenye huu Uzi bila ya kujali itikadi zao wameandika kama Watz inabidi Kikwete ajipime sana, vinginevo tunaweza kusikia vilio vya Watz muda si mrefu.
 
Ndiyo maana nikasema nasherehekea kuondoka kwake,

Pole pole mtanielewa tu..

Wanajamii kichwa cha habari cha jieleza, nimeshitushwa na kichwa cha gazeti hili na maneno ya chini yake maana kwa kiasi kikubwa yanamuhusu Rais mstaafu, Je! Yana ukweli wowote, vipi jawa jamaa hawatapigwa rungu tena kwa maneno yao haya??

attachment.php

 
Kipigo nilichokipata tangu Kikwete aingie madarakani na 'declare' siku ya leo kama sikukuu kwangu, nasherehekea kwa sababu zifuatazo,

- Naachana na rais ambaye hakuwa serious kulingana na umuhimu wa ofisi yake,

- Rais aliyetumia zaidi ya nusu ya uongozi wake akiwa nje akitumia kodi yangu badala ya kuwatumikia wananchi wake,

- Rais asiyethamini taaluma za watu wakiwemo waalimu, wauguzi yeye ni siasa tu,

- Rais asiyejali mihimili mingine,

- Rais aliyetuhumiwa kwa kila dili EPA yumo, Richmond yumo, Merameta yumo, Escrow yumo, what type of a president,

- Hakuipenda nchi nchi yake kwa dhati, tangu aseme pesa zetu siyo za umma niliumia sana,

- Maliasili zinahamishwa yeye hakujali,

- Rais aliyekuza udini na ukanda "rais hawezi toka kaskazini" hakuonekana kukemea,

- Rais aliyetuambia anayo majina ya wauza unga hadi leo anaondoka nayo,

- Rais anayesamehe wezi wakubwa wa EPA wakati wadogo wakiozea jela,

- Rais aliyependa vijembe kwa wananchi wanaotofautiana naye,

- Rais aliyetumia ofisi kwa maslahi yake na familia yake.

Nikuyakumbuka haya na mengine mengi hakika leo nasherehekea kuondoka kwake na wala siyo kuapishwa kwa Magufuli.
Vp hii miaka mitatu ya jiwe?
 
14 Reactions
Reply
Back
Top Bottom