Elections 2015 Binafsi nasherehekea kuondoka Kikwete na siyo kuapishwa Magufuli

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,271
47,269
Kipigo nilichokipata tangu Kikwete aingie madarakani na 'declare' siku ya leo kama sikukuu kwangu, nasherehekea kwa sababu zifuatazo,

- Naachana na rais ambaye hakuwa serious kulingana na umuhimu wa ofisi yake,

- Rais aliyetumia zaidi ya nusu ya uongozi wake akiwa nje akitumia kodi yangu badala ya kuwatumikia wananchi wake,

- Rais asiyethamini taaluma za watu wakiwemo waalimu, wauguzi yeye ni siasa tu,

- Rais asiyejali mihimili mingine,

- Rais aliyetuhumiwa kwa kila dili EPA yumo, Richmond yumo, Merameta yumo, Escrow yumo, what type of a president,

- Hakuipenda nchi nchi yake kwa dhati, tangu aseme pesa zetu siyo za umma niliumia sana,

- Maliasili zinahamishwa yeye hakujali,

- Rais aliyekuza udini na ukanda "rais hawezi toka kaskazini" hakuonekana kukemea,

- Rais aliyetuambia anayo majina ya wauza unga hadi leo anaondoka nayo,

- Rais anayesamehe wezi wakubwa wa EPA wakati wadogo wakiozea jela,

- Rais aliyependa vijembe kwa wananchi wanaotofautiana naye,

- Rais aliyetumia ofisi kwa maslahi yake na familia yake.

Nikuyakumbuka haya na mengine mengi hakika leo nasherehekea kuondoka kwake na wala siyo kuapishwa kwa Magufuli.
 
Nakubaliana na wewe 100% ingawa mabadiliko ya kweli hayawezi kupatikana ndani ya CCM hata aje nani.......
 
aisee!
aende tu, miaka hii 10 iliyopita ilikua ndoto mbaya kwa mwananchi.
 
Kipigo nilichokipata tangu Kikwete aingie madarakani na 'declare' siku ya leo kama sikukuu kwangu, nasherehekea kwa sababu zifuatazo,

- naachana na rais ambaye hakuwa serious kulingana na umuhimu wa ofisi yake,
- rais aliyetumia zaidi ya nusu ya uongozi wake akiwa nje akitumia kodi yangu badala ya kuwatumikia wananchi wake,
- rais asiyethamini taaluma za watu wakiwemo waalimu, wauguzi yeye ni siasa tu,
- rais asiyejali mihimili mingine,
- rais aliyetuhumiwa kwa kila dili EPA yumo, Richmond yumo, Merameta yumo, Escrow yumo, what type of a president,
- hakuipenda nchi nchi yake kwa dhati, tangu aseme pesa zetu siyo za umma niliumia sana,
- maliasili zinahamishwa yeye hakujali,
- rais aliyekuza udini na ukanda "rais hawezi toka kaskazini" hakuonekana kukemea,
- rais aliyetuambia anayo majina ya wauza unga hadi leo anaondoka nayo,
- rais anayesamehe wezi wakubwa wa EPA wakati wadogo wakiozea jela,
- rais aliyependa vijembe kwa wananchi wanaotofautiana naye,
- rais aliyetumia ofisi kwa maslahi yake na familia yake.

Nikuyakumbuka haya na mengine mengi hakika leo nasherehekea kuondoka kwake na wala siyo kuapishwa kwa Magufuli.
Hii kweli ni haki kwa Rais wa nchi?
https://www.youtube.com/watch?v=6EHdCPEwFRI
 
kusheherekea kuondoka kwa Dr.JK ni kusheherekea kuingia kwa Dr. Magufuli...
 
Tulipoteza fursa nyingi kama nchi baada ya NEC kumweka madarakani huyu jamaa. Sasa aende zake bhana, hatutamkumbuka na yeye asihangaike kutukumbuka.. rais wa mipasho.. atembee mbele bhana tushachookaaa
 
Kabla hajamaliza ile miwili tu hali ishakuwa tete. Kapumzike kwa amani JMK. Tukipata nauli tutakuja kukusalimu Msoga
 
kusheherekea kuondoka kwa Dr.JK ni kusheherekea kuingia kwa Dr. Magufuli...
Siwezi kusherehekea kuingia kwa Magufuli kwa vile sijui anapotupeleka, 2005 nilifanya kosa la kusherehekea kuingia kwa Kikwete kitu ambacho leo nakijutia.
 
sifikirii kama jf waliingiliwa ili kunyamazishwa,naona ilikua ni plan ili baadhi ya members wawe attacked kama ilivyotokea.."ccm wamewekeza ktk mitandao" hii kauli ina uhusika.,
Toka jk,toka sasa
Mkuu naweza kuungana na wewe inawezekana shekel ilitembea.
 
Nikikumbuka wale waliopandishwa vyeo baada ya lile tukio la Iringa, huwa nashindwa kabisa kumuelewa huyu mtu.
 
Nikikumbuka wale waliopandishwa vyeo baada ya lile tukio la Iringa, huwa nashindwa kabisa kumuelewa huyu mtu.
Sio hiyo tu, baada ya kubakiza siku 2 ofisini kaendelea kuteua maswahiba wake, ni juzi tu kateua m/kiti wa bodi ya wakurugenzi TTCL haya si matumizi mazuri ya ofisi halafu sio busara.
 
JF imeanza taratibu kurudi kwenye mstali wake wa awali. Magufuli akipewa funguo leo watabakia tu wale wenye gubu!
 
Ee mwenyenzi Mungu toa utulivu wa ndani kwa watanzania wote. Leo tunamaliza yote, watu wakae salama mioyoni.
 
Kipigo nilichokipata tangu Kikwete aingie madarakani na 'declare' siku ya leo kama sikukuu kwangu, nasherehekea kwa sababu zifuatazo,

- Naachana na rais ambaye hakuwa serious kulingana na umuhimu wa ofisi yake,

- Rais aliyetumia zaidi ya nusu ya uongozi wake akiwa nje akitumia kodi yangu badala ya kuwatumikia wananchi wake,

- Rais asiyethamini taaluma za watu wakiwemo waalimu, wauguzi yeye ni siasa tu,

- Rais asiyejali mihimili mingine,

- Rais aliyetuhumiwa kwa kila dili EPA yumo, Richmond yumo, Merameta yumo, Escrow yumo, what type of a president,

- Hakuipenda nchi nchi yake kwa dhati, tangu aseme pesa zetu siyo za umma niliumia sana,

- Maliasili zinahamishwa yeye hakujali,

- Rais aliyekuza udini na ukanda "rais hawezi toka kaskazini" hakuonekana kukemea,

- Rais aliyetuambia anayo majina ya wauza unga hadi leo anaondoka nayo,

- Rais anayesamehe wezi wakubwa wa EPA wakati wadogo wakiozea jela,

- Rais aliyependa vijembe kwa wananchi wanaotofautiana naye,

- Rais aliyetumia ofisi kwa maslahi yake na familia yake.

Nikuyakumbuka haya na mengine mengi hakika leo nasherehekea kuondoka kwake na wala siyo kuapishwa kwa Magufuli.
Mimi hili suala la kaskazini huwa linanichanganya. Hivi kwa mujibu wa jiografia ya nchi yetu Makufuli hatoki kaskazini kweli? Maana mimi naona Kagera, Mara na Mwanza zote ziko kaskazini ingawa wao wanapendelea kuita kanda ya ziwa wakiwa wanasahau kuwa ziwa victoria liko kaskazini hivyo nazo ziko kaskazini. Hiyo Mara ndiko alikotoka Nyerere na inapakana na Arusha lakini hawakuiita kaskazini kisiasa na hawasemi kaskazini ndiko alikotoka Nyerere lakini ukitaja Slaa, Mbowe, Lowassa, Mbatia na Sumaye wanasema kaskazini.
 
Back
Top Bottom