Elections 2015 Binafsi nasherehekea kuondoka Kikwete na siyo kuapishwa Magufuli

Kipigo nilichokipata tangu Kikwete aingie madarakani na 'declare' siku ya leo kama sikukuu kwangu, nasherehekea kwa sababu zifuatazo,

- Naachana na rais ambaye hakuwa serious kulingana na umuhimu wa ofisi yake,

- Rais aliyetumia zaidi ya nusu ya uongozi wake akiwa nje akitumia kodi yangu badala ya kuwatumikia wananchi wake,

- Rais asiyethamini taaluma za watu wakiwemo waalimu, wauguzi yeye ni siasa tu,

- Rais asiyejali mihimili mingine,

- Rais aliyetuhumiwa kwa kila dili EPA yumo, Richmond yumo, Merameta yumo, Escrow yumo, what type of a president,

- Hakuipenda nchi nchi yake kwa dhati, tangu aseme pesa zetu siyo za umma niliumia sana,

- Maliasili zinahamishwa yeye hakujali,

- Rais aliyekuza udini na ukanda "rais hawezi toka kaskazini" hakuonekana kukemea,

- Rais aliyetuambia anayo majina ya wauza unga hadi leo anaondoka nayo,

- Rais anayesamehe wezi wakubwa wa EPA wakati wadogo wakiozea jela,

- Rais aliyependa vijembe kwa wananchi wanaotofautiana naye,

- Rais aliyetumia ofisi kwa maslahi yake na familia yake.

Nikuyakumbuka haya na mengine mengi hakika leo nasherehekea kuondoka kwake na wala siyo kuapishwa kwa Magufuli.
Haya sasa tuambizane kwa huyu

Td mkali
 
Back
Top Bottom