Binadamu wote walio hai leo, walitoka kusini mwa mto Zambezi Botswana

Alvin A.

JF-Expert Member
Oct 14, 2016
2,868
3,624
Wanasayansi wamelitaja eneo la kusini mwa Mto Zambezi kuwa ndiko binadamu wote walio hai hii leo wanatokea. Eneo hilo sasa limegubikwa kwa chumvi lakini kwa wakati mmoja lilikuwa ni ziwa kubwa, ambalo huenda likawa ndio chimbuko letu wanadamu tangu miaka 200,000 iliyopita.

Wazee waliotangulia waliishi huko kwa miaka 70,000, hadi hali ya hewa ya huko ilipobadilika, watafiti wanapendekeza. Walianza kusogea wakati ardhi yenye rutuba ilipozidi kugunduliwa, na kuchangia uhamiaji wa vizazi viilivyofuata kutoka Afrika.

"Limekuwa wazi kwa muda fulani sasa kwamba kimaumbile, binadamu wa leo waliokuwepo Afrika kwa kadiria miaka 200,000 iliopita," anasema Prof. Vanessa Hayes, mtaalamu wa masuala ya jeni kutoka Chuo cha Utafiti Garvan Institute of Medical Research nchini Australia.

"Kile ambacho kimejadiliwa kwa muda mrefu ni eneo maalum la wapi walikozuka na kufuatia na kutawanyika kwa mababu waliotangulia."

Hata hivyo, kauli ya mwisho la Profesa Hayes limevutia shaka kutoka kwa watafiti wengine kwenye nyanja hiyo.

Ngome kuu ziwani, Eneo linalotajwa ni kusini mwa Mto Zambezi kaskazini mwa Botswana. Watafiti wanadhani mababu zetu, walitua karibu na mfumo mkubwa Afrika wa ziwa, Ziwa Makgadikgadi, ambalo sasa ni eneo lililo na chumvi nyingi.

"Ni eneo kubwa mno, huenda lingekuwa na maji maji sana, na ardhi yenye kuvutia," anasema Prof Hayes. "Na huenda lingekuwa eneo zuri la kuishi kwa binaadamu wa leo na pia wanyama."

Baada ya kuishi hapo kwa miaka 70,000, watu walianza kuondoka. Mabadiliko katika namna mvua inavyonyesha katika eneo hilo yalichangia mawimbi matatu ya uhamisho miaka 130,000 na 110,000 iliopita, yaliochangiwa kwa kufunguka kwa ardhi zaidi yenye rutuba.

Prof Hayes anajifunza namna ya kuwasha moto na wawindaji wa Jul'hoansi katika eneo la Kalahari Namibia
Wahamiajiwa kwanza walielekea kaskazini mashariki, na kufuatwa kwa wimbi la pili la wahamiaji waliosafiri kueleka kusini magharibi na idadi ya tatu ya watu walisalia katika eneo hilo mpaka hii leo.

Taswira hii imetokana na kuangalia nyuma muundo wa familia za binaadamu kwa kutumia mamia ya sampuli za chembechembe za DNA zinazotoka kwa kizazi cha mama kutoka kwa Waafrika walio hai.

Utafiti: Malazi ya Sokwe watu ni masafi kuliko ya binadamu
Ushahidi wa zamani kuhusiana na maisha 'wapatikana'
Hii ndio sura ya kizazi cha Uingereza
Kwa kuchanganya elimu ya Jeni na jiolojia na kwa kuiga kwa kutumia kompyuta na hali ya hewa, watafiti walifanikiwa kutoa tasiwra ya namna bara la afrika lilivyokuwa miaka 200,000 iliopita.

Kuijenga upya hadithi ya binaadamu
Hatahivyo, utafiti huo uliochapishwa katika jarida la Nature, umetazamwa kwa uangalifu na mtaalamu mmoja, anayesema huwezi kuunda upya hadithi ya chimbuko la binaadamu kutokana na DNA pekee.

Uchambuzi au tathmini nyingine imetoa majibu tofuati kwa kutumia ugunduzi wa mabaki ya kiumbehai kuashiria chimbuko lao limetokea Afrika mashariki.

Profesa Chris Stringer wa jumba la kitaifa la ukumbusho wa historia mjini London, ambaye hahusiki na utafiti huu amesema mageuzi ya binaadamu wa kale Homo sapiens ulikuwa ni mfumo mgumu.

"Huwezi kutumia usambazaji wa DNA mitochondrial peke yake kutambua eneo moja la chimbuko la binaadamu wa leo," ameiambia BBC.

"Nadhani inapita kiwango cha data kwasababu unatazama sehemu moja tu ya muundo huo kwahivyo hauwezi kukupa taarifa kamili ya chimbuko letu."

Hivyo basi, huenda kukawa na machimbuko mengi au maeneo walilkotoka binaadamu wa leo kuliko hilo moja, ambayo yangali kutambuliwa.

Hatua zilizopigwa katika mageuzi ya binaadamu kihistoria
Miaka 400,000 iliyopita: Neanderthal - binamu zetu - waanza kuonekana na kusogea Ulaya na Asia.
Miaka 300,000 hadi 200,000 iliyopita:Homo sapiens - binaadamu wa leo - waonekana Afrika.
Miaka 50,000 hadi 40,000 iliyopita: Binaadamu wa leo wafika Ulaya.

BBC/swahili

*** Hawa jamaa wanatuchezea akili sasa***

Screenshot_20191029-203650.jpeg
 
Kwamba binadamu ameishi ulaya miaka 50,000 tu iliopita!

Kwamba binadamu ameishi afrika miaka 400,000 iliopita!

Kwa hizi sentesi mbili mi kwa uelewa wangu, wanatufanya waafrika mabwege!

Kama kuna mahali ktk dunia hii ambapo ndo chimbuko la binadamu,
Mbona hawasemi na machimbuko ya wanyama wengine mf: swala tembo simba nk.!?

dunia imeiubwa kwa ajili ya kukaa viumbe vyote vionekanavo duniani

Unaanzaje kutafuta chimbuko la binadamu hapa duniani!?

Kama ni kweli wanatafuta chimbuko la binadamu kwa nini wasiende kwenginewe huko wakatafute?

Kwa nn kwanza wasitafiti chimbuko la dunia ndo wafuatie kutafiti chimbuko la binadamu waliopo duniani?

Utaanzaje kutafuta chimbuko la mtoto ambae mama yake (land) hitaki kumjua kbsa!!?
 
Kwamba binadamu ameishi ulaya miaka 50,000 tu iliopita!

Kwamba binadamu ameishi afrika miaka 400,000 iliopita!

Kwa hizi sentesi mbili mi kwa uelewa wangu, wanatufanya waafrika mabwege!

Kama kuna mahali ktk dunia hii ambapo ndo chimbuko la binadamu,
Mbona hawasemi na machimbuko ya wanyama wengine mf: swala tembo simba nk.!?

dunia imeiubwa kwa ajili ya kukaa viumbe vyote vionekanavo duniani

Unaanzaje kutafuta chimbuko la binadamu hapa duniani!?

Kama ni kweli wanatafuta chimbuko la binadamu kwa nini wasiende kwenginewe huko wakatafute?

Kwa nn kwanza wasitafiti chimbuko la dunia ndo wafuatie kutafiti chimbuko la binadamu waliopo duniani?

Utaanzaje kutafuta chimbuko la mtoto ambae mama yake (land) hitaki kumjua kbsa!!?
Waache wahangaike wakipoteana ndo watajua yupo MUNGU
 
Hawa watafiti hawajawahi kuja na jawabu moja la uhakika! Kila baada ya muda wana wanasimulia Watu hadithi mpya! Ifike wakati wapuuzwe kwa uongo wao.
Huwa wanaandika pepa zao kwa ajili ya PhD so huwa wanatakiwa wagundue kitu kipya ndio wana force na tafiti za kifigisu kama hivi ha ha ha ha ha ha
 
Hawa Wazungu ni waongo sijapata kuona. Leo wanasema wanadamu walitoka kusini mwa mto Zambezi. Kuna wakati nasoma historia walituambia sisi watu weusi tulitokea misitu ya Congo karibu na Cameroon, kuna siku tena wakatuambia chanzo cha mwanadamu ni kule Oldupai gorge Arusha, hatujapumzika wakasema chanzo cha mwanadamu ni Ethiopia.

Sasa sijui kipi ni kipi. Maana Darwing naye anasema tulitokana na masokwe na Biblia inasema Mungu alituuumba akatuweka Eden ambayo labda ni Mesopotamia...
 
Huwa wanaandika pepa zao kwa ajili ya PhD so huwa wanatakiwa wagundue kitu kipya ndio wana force na tafiti za kifigisu kama hivi ha ha ha ha ha ha
Unacho kisema ni sahihi coz hii mambo inachanganya! Watu wa Theology nao wanasema Makanisani kuwa Dunia ina miaka 9000+ tangu iumbwe!
 
Mimi ninavyojua watu wa kusini wengi walitokea huko Zambezi lakini huku kaskazini origin yetu ni pale Eden....!
 
Mimi naona tuwasikilize wazungu tu .... maana hata ukisema chumbuko letu ni middle east kwa Adam na Eve hio story nayo ni wazungu ndo walikuja nayo...
 
Wakae wote sasa wakubaliane tupate jibu moja sio kuyumbishwa kila siku
 
Back
Top Bottom