Binadamu wa kwanza kukanyaga katika sayari ya Mihiri "Mars" anatarajiwa kuwa mwanamke

ChikoTz

Member
Feb 26, 2019
37
33
Taasisi inayojihusisha na utafiti wa masuala ya anga nchi Marekani NASA imetangaza kwamba binadamu wa kwanza atakayekanyaga katika sayari ya Mihiri "Mars" anaweza akawa mwanamke .

Rais wa NASA Jim Bridenstine,akiongea katika kipindi kimoja cha redio alichoshiriki alisema kuna uwezekano binadamu wa kwanza atakayekanyaga katika sayari ya Mihiri akawa mwanamke.

Bridenstine alisema bado haijaamuliwa ni mtu gani ataenda katika sayari ya Mihiri, alifahamisha kwamba mipango yao kwa siku zijazo ni kuhakikisha wanawake wanashiriki kikamilifu na kuwa mstari wa mbele.

Bridenstine, alimjibu shabiki mmoja aliyemuuliza kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter kama katika safari ya mwezi ujao ya NASA kutakuwa na nafasi kwa wanawake , kwa kusema “bila shaka”

NASA kwa mara ya kwanza ipo katika maandalizi ya kumpeleka mwanamke katika anga za mbali.

Chanzo:
@MU Blog (Msakaji Udaku Blog)
Mars.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi binadamu watakapoanza kuishi huko kama ilivyopangwa; je, nafasi ya dini itakuwaje huko? Kwa mfano, itahubiriwa kwamba Yesu alikuja duniani? Kumbuka huko ni Mars sio duniani. Au labda hija ni lazima kwenda mji Mtukufu wa Makah? Watahama na vitabu hivi hivi vya dini ambavyo vinazungumzia zaidi mambo ya duniani na sio Mars(ni)? Just want to know.

Kadiri maendeleo ya sayansi yanavyoongezeka naona dini zikipata wakati mgumu sana vizazi vijavyo. Anyway, labda na wenyewe watapelekewa mitume na kitabu cha zama zao.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom