Binadamu anapokufa ni lazima atoe kinyesi , mkojo, mbegu za kiume ama za kike

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,554
8,552
Kifo ni kitu kibaya sana! Maumivu wakati wa kukata roho ni siri ya marehemu na Mungu wake... ( Hakuna wa kuthibitisha hili )!!

Kila mtu atakufa , utake usitake ! Kwa kifupi sisi ni marehemu watarajiwa.

Binadamu anapokata roho ni lazima atoe uchafu wote mwilini.

Uchafu maana ake kinyesi (mavi) , mkojo na mbegu za kiume au za kike ( kama anazo)!

Sijajua ni mechanism ipi inayosababisha binadamu anapokata roho ni lazima atoe mbegu zake za kiume au kike.

Swali fikirishi sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uliposema sote tutakufa nikaona tayari upo chaka hakuna ukweli kwamba wote tutakufa hasa kwetu sisi tunaoamini katika kitabu kitakatifu biblia inatuambia

1 KOR. :15:51
Angalieni, nawaambia ninyi siri; hatutalala sote, lakini sote tutabadilika,

Kwa hiyo siyo kweli binadamu wote watakufa

Lakini kwenye hoja yako pia juu ya utoaji wa uchafu napo sidhani kama ni sahihi maana kuna wale wanaolala wakapitiliza hukohuko nao wanatoa uchafu? Wanaofia kwenye operation nao wanatoa uchafu? Umefanya generalization ambayo haina uhalisia
 
Mimi najua mtu akijinyonga ndio kifo chake huambatana kua na hizo conditions ulizotaja sabu ya kukosa oksijeni.... Lakini wewe umegeneralize kifo chochote, hapo sina uhakika.... Ndio maana wanasema "Siri ya maiti anaijua mwoshaji" inabidi waoshaji waje tupa eksipiriensi ya hii.....
 
 
Back
Top Bottom