Bin Laden apongeza mapinduzi ya wananchi katika nchi za Kiarabu

mdau wetu

JF-Expert Member
Apr 20, 2011
548
58
Bin Laden apongeza mapinduzi ya wananchi katika nchi za Kiarabu
bin%20laden.jpg
Kiongozi wa mtandao wa al Qaida Usama bin Laden amepongeza mapinduzi ya wananchi katika nchi za Kiarabu katika mkanda wa sauti uliorushwa hewani baada ya kuuawa na jeshi la Marekani.
Katika mkanda huo Bin Laden amewataka wafuasi wake kufanya jitihada kubwa zaidi za kuwaondoa madarakani viongozi waovu katika nchi za Kiislamu. Usama bin Laden ambaye Wamarekani wanadai kuwa walimuua katika shambulizi la kushtukiza nchini Pakistan mapema mwezi huu, amewataka wafuasi wa al Qaida kuanzisha kitengo cha operesheni maalumu kitakachofanya kazi za kukidhi haja za umma sambamba na mapinduzi ya wananchi wanaopambana kuangusha tawala za kidhalimu.
Marekani inasema kuwa kiongozi wa mtandao wa al Qaida Usama bin Laden aliuawa katika shambulizi lililofanyika tarehe pili Mei dhidi ya nyumba moja nje ya jiji la Islamabad huko Pakistan ingawa hadi sasa haijaonyesha maiti yake au kutoa ufafanuzi kamili wa jinsi alivyouawa.

Kwa hisani ya Idhaa ya Kiswahili ya Radio Tehran, Iran (kiswahili.irib.ir)
 
Tangu wawapindue wanaoitwa vibaraka paka sasa hawajatulia, faida iko wapi???
 
Back
Top Bottom