Bima ya NSSF haihudumii mimba ya miezi sita kushuka chini?

Mtanzatozo

JF-Expert Member
Mar 2, 2016
972
1,163
BIMA YA NSSF HAIHUDUMII MIMBA YA MIEZI SITA KUSHUKA CHINI.

Habari zenu ndugu zangu!

Kuna ukweli au milolongo tu ya hpa na pale, nilimpeleka mke wangu hospital ya DAR GROUP pale tazara kwa matibabu ya tumbo yaliyodumu kwa siku mbili akiwa kwenye hali ya ujauzito, lakini cha kushangaza hakupatiwa matibibabu kisa mjamzito!

Mpokea kadi alihoji tu kama mjamzito na hakufikisha miezi sita na kuendelea bima haina dhamana naye. Nilimuuliza sasa kama ana mimba na maradhi alokuwa nayo tumboni hayahusiani na mimba wewe unajuaje?

Yule dada alikataa kabisa, msaada jamani wa kuelimishwa juu ya hili na kama kuna list pengine ya matibabu ambayo hyatolewi na bima ya NSSF please nijuzwe!
 
Back
Top Bottom