Bima ya afya (NHIF) inagharimia hii operation hapo Muhimbili Hospital?

Thailand

JF-Expert Member
Nov 15, 2019
262
779
Habari za wakati huu,

Kuna mpendwa wangu (mama) kapatwa na tatizo la mfupa mdogo kuota kuelekea kwenye kiganja cha mguu, hali inayosababisha kupatwa na maumivu makali pindi anapotembea au kusimama maana huwa kama mwiba mkali umchomao miguuni.

Hi ilikuja baada ya maumivu hayo kuzidi tukampeleka hospital ya mkoa wa Mara (MRRH) wakamfanyia X-ray ndio wakaona hako ka mfupa kanakoota, ila tatizo wakadai wao hawawezi kufanya huduma hiyo. Wakatuelekeza mahala sahihi mama huyo kupata huduma ni kwenda Muhimbili Hospital.

Sasa tupo kama familia tunataka tumtume hapo Muhimbili lakini gharama tunapenda ziwe covered by NHIF kwa sababu mama ana bima hiyo na mimi hao jamaa hupata mchango wangu kila mwezi.

Nimeomba nifahamishwe kwanza kama NHIF wanagharimia operation hiyo kwa sababu juzi nimeenda hospital kutibiwa macho baada ya kuwa yananisababishia kichwa kuuma sana, iligundulika kwamba kwa tatizo la mwanga kwenye macho linalopelekea tatizo hilo nahitaji miwani kwa ajili ya kupunguza maumivu kwenye macho.

Lakini kuomba miwani hiyo wakanijibu bima yako ya afya hailipii miwani hiyo unatakiwa ujinunulie mwenyewe. Basi nikabaki nashangaa iweje hawa jamaa hela zangu zinakwata kila mwezi na mimi namshukuru Mungu sina mahudhurio ya mara kwa mara hospitalini kwa kuugua ila wanashindwa ku cover baadhi ya changamoto zangu za afya? Basi nikakosa majibu.

Sasa wadau nimeomba mnisaidie kujua kama hiyo operation ya kuondoa hako ka mfupa inaweza kulipwa na NHIF ili iwe rahisi kumtuma mzazi huyu kutoka Musoma to Muhimbili hospital ili aje apate huduma hiyo. Isije ikawa tumemtafutia nauli amekuja huko halafu akaambiwa huduma hiyo hailipiwi na NHIF.

Asanteni.
 
Bima ya afya haihusu gharama za miwani na neno. Hata hivyo kama ulipima macho pia ni msaada mkubwa miwani anunue. Kuna waajiri huwa wanakurudishia pesa kidogo za gharama ya miwani ukipeleka stakabadhi ofisini.
 
Bima ya afya haihusu gharama za miwani na neno. Hata hivyo kama ulipima macho pia ni msaada mkubwa miwani anunue. Kuna waajiri huwa wanakurudishia pesa kidogo za gharama ya miwani ukipeleka stakabadhi ofisini.
Asante
Na vipi kuhusiana na hiyo operation?
 
Nilikuwa na shida hiyo toka mtoto kilipotea nilipokuwa mkubwa kikaanza tena kuota nilikuwa na nhif nilitibiwa kwa kuchomwa sindano hapo hapo panapouma nikapona ila ngozi ikababuka kuwa nyeupe kwa sasa imerudi kawaida
 
Bima ya afya haihusu gharama za miwani na neno. Hata hivyo kama ulipima macho pia ni msaada mkubwa miwani I anunue. Kuna waajiri huwa wanakurudishia pesa kidogo za gharama ya miwani ukipeleka stakabadhi ofisini.
Mbona niliziba jino muhimbili kwa kutumia NHIF? au umemaanisha kuweka meno bandia?
 
Back
Top Bottom