Bima ya Afya kwa Wote (Universal Health Care)Rais Samia atoa TZS 149BL

Jabali la Siasa

JF-Expert Member
Jul 10, 2020
2,530
2,141
Bima ya Afya kwa Wote Tanzania yaani ( Universal Health Care-UHC ) Rais Samia Suluhu Hassan ametoa Jumla ya TZS 149BL ili kila Mtanzania ifikapo 2030|35 awe na bima ya afya,

" Hakuna kama Samia "


Pamoja na kwamba Bima ya Afya kwa wote iko kwenye Ilani ya CCM ya mwaka 2020-2025 Ukurasa wa 136 aliyekuwa Mgombea Urais wa Chadema Tundu Lissu aliidukua kipengele hiki na kukinadi kwa nguvu kubwa wakati flani, ikaonekana kana kwamba hilo wazo|agenda ya Bima ya Afya kwa Wote au " Universal Health Care " ni lake Watanzania bila kujua kuwa Lissu alilidukua tu toka Ilani kubwa ya chama kikubwa cha CCM, fine yamepita.

Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutambua umuhimu wa "Bima ya Afya na kutekeleza ilani ya CCM tayari ameshatenga pesa ya kuanzia kiasi cha Tshs 149BL kwaajili ya kugharamia mpango huu kupitia Bajeti ya Wizara ya Afya ya FY2021|22.

Mpango huu utatekelezwa kwa awamu awamu hadi kufikia mwaka 2030|35 kila Mtanzania atakuwa na UHC huku katika awamu hii ya kwanza UHC itazihusu kaya masikini zinazokadiriwa kufikia 20% ya kaya zote 12.827M za Tanzania,

Kwa kasi hii Rais Samia nataka nawale wachache waliosalia kule Chadema au vyama vingine vidogo vidogo vya ACT, NCCR, CUF wote waje CCM ili tuungane na Mama Samia Suluhu Hassan katika kuwaletea Watanzania hawa maendeleo endelevu kwakuwa kila walichoahidi kwa maneno kwenye Ilani zao Mama Samia Suluhu Hassan anafanya kwa vitendo.
photo_2021-11-09_03-19-28.jpg

VIVA TANZANIA || VIVA SAMIA VIVA
 
Back
Top Bottom