Bima inayofuata sheria za kiislam (takaful) yashinda nchini kenya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bima inayofuata sheria za kiislam (takaful) yashinda nchini kenya

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by R.B, Sep 2, 2012.

 1. R.B

  R.B JF-Expert Member

  #1
  Sep 2, 2012
  Joined: May 10, 2012
  Messages: 6,168
  Likes Received: 1,103
  Trophy Points: 280
  Bima inayofuata sheria za kiIslam inayojulikana kama (Takaful) imekua mshindi ktk mkutano wa tatu unaofanyika kila mwaka nchini Kenya na ambao umefanyika kwa mara ya tatu mwaka huu. Wakati wanatoa zawadi hiyo waamuzi wa kikao hicho ilibainika kwamba ilikua ni mara ya kwanza ambapo zawadi hiyo imekwenda kwa shirika jipya, shirika ambalo limeanza kazi zake mwezi wa tatu mwaka huu 2012. Ni muhimu kukumbushana kwamba hilo ni shirika la kwanza ambalo linafanya kazi zake kwa kufuata sheria za kiislam. Walisikika wakisema wamiliki wa shirika hilo ‘Tumefurahi na tunahisi faraja kupata zawadi hii. Tukio hili linazungumza kwa sauti ya juu kwamba kazi zetu zimehishimiwa na mashirika mengine ya bima alisema CEO Hassan Bashir’. Kupata zawadi kama hii ni ushahidi wa wazi kwamba masharti muhimu kama vile uwazi, heshima, kukubali majukumu ni muhimu ktk biashara ya bima. Mkutano huo wa mwaka unaandaliwa na business intelligence na publishing house Think Business Limited.
  Fikra ya bima inayofuata sheria za kiIslam ni kushirikiana na kusaidiana na kudhaminiana. Pamoja na mambo mengine bima ya kiIslam inakataza aina zote za mambo ambayo yatakua na uhusiano na riba, kamari na hadaa.


  SOURCE- IJUE BANK YA KIISLAM
   
Loading...