Billy Graham alimsaidia Rais George Bush kuacha Pombe

Baraka21

JF-Expert Member
Mar 15, 2021
1,265
3,177
Laura Bush anasema mume wake yaani George W. Bush alikuwa mlevi sana. Ikafika kipindi akaogopa akaona hata Urais utamshinda. Lakini Laura Bush hakuwahi kuthubutu kuita press conference kusema "ninyi wamarekani mnamheshimu na kumsikiliza huyu mshenzi mlevi mkubwa? Hamumjui tu". Hakuthubutu.

Alichokifanya alimtafuta Billy Graham amsaidie mumewe George Bush kuacha ulevi kimyakimya.

Leo mume wako kurudi asubuhi umeshapost Instagram. Unataka dunia nzima ije kumshauri?

Mke amekutukana umeshapost facebook. Watu wa facebook walikuchagulia mke? Tatua mambo yako faragha.Kila kitu kina faragha.

George Bush mwenyewe asingekiri kuwa alikuwa mlevi ungeamini? Si ungejua Laura anaenjoy! Lakini Laura alikuwa na changamoto ndani ya Ikulu. Lakini aliifanya ikawa faragha na Bush akasaidika akaacha pombe
 
Bush kipindi cha uongozi wake ilikuwa balaa alikuwa anatoa hotuba mashariki ya kati yote inaingia wenge ukiangalia jicho jekundu suti haijanyooshwa wala nywele hajaenda saloon yule mzungu ndio toleo la mwisho la urais wa USA waliofuata wameshindwa kuitendea haki USA
 
Hapo tunajifunza kutunza siri za ndoa zetu,Raula Bush ni mfano wa kuigwa !wanawake wengine hawajui kutunza au kuvumilia mambo ya ndani,yeye ni kutangaza hadi sokoni,stand,nk utadhani hao anaowatangazia wanamuona yeye ndo wa maana!kumbevwanaona ni mshenzi tuu.
 
Back
Top Bottom