Billnass: Hata Uwe na Pesa Kumzidi Bill Gates Bado hutaweza kuibeba maiti yako wala kujizika mwenyewe, heshimu watu

Shadow7

JF-Expert Member
Sep 28, 2020
13,591
20,039
#TATIZO Kwenye Maisha hakuna Kumaliza ama kuyaweza mpaka siku unazikwa chini,
Jiulize ni watu wa ngapi umewahi kuwajua walikuwa Maaarufu mpaka ukadhania wamemaliza lakini leo huyakumbuki majina yao kwa ukubwa huo??

billnass_1671817531522824967863023668511585035152500n.jpg


Je ni wangapi walikuwa na Biashara zilizoshamiri na leo wamefilisika??
Wangapi walikuwa na Nguvu kiasi cha kuona hakuna anaemuweza lakini leo hawana tena ??

Wangapi walikuwa na Nyumba ama gari za kifahari na leo hawana hata kimoja??
Hakuna Utajiri Mzuri kama Kuishi na Watu Vyema…Hata Uwe na Pesa Kumzidi Bill Gates Bado hutaweza kuibeba maiti yako wala kujizika mwenyewe…

Hata Uwe Maarufu kumzidi Michael Jackson Bado utahitaji watu ! Ukiwa Mwizi utawaibia Watu,ukiwa Muimbaji Utawaimbia Watu,ukiwa Muhubiri Utahubiria Watu,So Heshimu sana Watu….hakuna Dunia Bila Watu 🙏🏿
 
Hakuna aliewahi kufa akaachwa juu, Hata wale wanaotekelezwa mochwari sababu ya gharama za kuilipia maiti 'Mamlaka za miji huzika hao watu. hivyo tumia muda wako kurahisisha maisha yako.Ukifa utazikwa tu.
 
Kwani ukifa kuzikwa ni lazima mkuu!? Kuna Jamii ya watu wengine wakifa hawazikwi na pia sio Kila mtu akifa huwa anazikwa Wengine huwa wanauwawa na maiti zao kutupwa wengine huwa wanaliwa na wanyama wakali ..so acha kukarili mkuu
 
Ukiwa mwizi, lazima uwaibie watu
Ukiwa mwimbaji utawaimbia watu
Hivyo heshimu sana watu
 
Kwanj hapa tatizo ni nini?
Au wewe ndo huyo uliyemfunga tai umekasirika baada ya kupost ukimfunga tai?
 
Sa hvi ndo anayajua hayo ...... Wakat mnapitia magumu ndo mnajifanya kuwa na busara ....
 
Tafuta hela mkuu acha kumuonea wivu, huoni hapo ametengeneza ajira kwa huyo jamaa?
Masikini mna matatizo sana.
Billnas akifa lazima atazikwa tu, siyo lazima umzike wewe.
👊👊
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom