Bill ya Maji DAWASCO Haziendani na Uhalisia wa Matumiz ya maji

DeepPond

JF-Expert Member
Nov 18, 2017
14,268
2,000
Inaletwa bill ya Maji
Inasoma umetumia Unit 50 kwa mwezi,

Unawauliza,
"Kwani unit moja ni sawa na Lita ngapi?"

Wanajibu,
"Unit moja Ni sawa na Lita 1000 za maji Sawa na ndoo 50 za Lita 20"

Unabaki unajiuliza,

Hivi mwezi huu kwa matumizi yangu ni kweli nimezitumia Lita 50,000 za maji ?

Hivi mwezi huu kwa matumizi yangu ni kweli nimetumia ndoo 1000 za maji?

Hapo hapo,
Maji yenyewe yanatoka kwa mgao, wiki Hii yapo wiki nyingine hamna.

Yakitoka Unasema
hebu nijaze Tank maji la Lita 2500, nione litanifikisha wapi.

Unajikuta umelijaza Mara mbili kwa wiki. Sawa na Lita 5,000.
Ambapo endapo ungeenda ivyo ivyo mwezi mzima ningejaza mara 8 kwa wiki 4 tu za mwezi.
Ambapo ungepata jumla Lita 20,00 za maji sawa na unit 20.

SASA UNABAKI UNAJIULIZA,
Hivi hizi unit 50 sawa na lita 50,000 kwa mwezi zimetokea wapi?

hivi Ni kweli Ni Mimi kwa mwezi niliyetumia maji SIMTANK 20 za Lita 2500?

UNAGUNDUA,
bill iko mara mbili zaidi ya matumizi Halisia

Matumizi hayaendani na uhalisia wa bill inayoletwa.

Kiukweli Kuna kitu hakiko sawa kwenye bill za maji DAWASCO.

IMG_20210526_201239.jpg
 
Nafaka

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
6,070
2,000
Inaletwa bill ya Maji
Inasoma umetumia Unit 50 kwa mwezi,

Unawauliza,
"Kwani unit moja ni sawa na Lita ngapi?"

Wanajibu,
"Unit moja Ni sawa na Lita 1000 za maji Sawa na ndoo 50 za Lita 20"

Unabaki unajiuliza,

Hivi mwezi huu kwa matumizi yangu ni kweli nimezitumia Lita 50,000 za maji ?

Hivi mwezi huu kwa matumizi yangu ni kweli kwa mwezi huu nimetumia ndoo 1000 za maji?

Hapo hapo,
Maji yenyewe yanatoka kwa mgao, wiki Hii yapo wiki nyingine hamna.

Yakitoka Unasema
hebu nijaze Tank maji la Lita 2500, nione litanifikisha wapi.

Unajikuta umelijaza Mara mbili kwa wiki. Sawa na Lita 5,000.
Ambapo endapo ungeenda ivyo ivyo mwezi mzima ningejaza mara 8 kwa wiki 4 tu za mwezi.
Ambapo ungepata jumla Lita 20,00 za maji sawa na unit 20.

SASA UNABAKI UNAJIULIZA,
Hivi hizi unit 50 sawa na lita 50,000 kwa mwezi zimetokea wapi?

hivi Ni kweli Ni Mimi kwa mwezi niliyetumia maji SIMTANK 20 za Lita 2500?

UNAGUNDUA,
bill iko mara mbili zaidi ya matumizi Halisia

Matumizi hayaendani na uhalisia wa bill inayoletwa.

Kiukweli Kuna kitu hakiko sawa kwenye bill za maji DAWASCO.

View attachment 1798665
Duh mkuu mimi na kumwaga mwaga maji bill uwa haizidi 38000 wewe watakuwa wanakupiga.
 
Joseph lebai

JF-Expert Member
Jul 19, 2017
6,022
2,000
Wewe kuwa makini na mita yako , labda mita waichokonee kijanja, kila mwezi angalia umefikia unit ngapi, waulize unit moja ni sh, ngapi? Zidisha na hizo unit utapata jibu. Kwangu haibiwi mtu!!
 
Faana

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
17,697
2,000
Ndiyo tatizo la kuwa wategemezi kwenye teknolojia, moja ya changamoto tanazopata wateja wa maji ni bills kuwa kubwa na kutotafuta sababu, kuna mtaalamu alisema kwenye moja ya vipindi vya TV, maji yakikatika, yanaporudi kunakuwa na upepo ambao huzungusha mita.

Nilitegemea vyuo vyetu vikuu na vile vya ufundi vingetafuta namna ya kushughulika na changamoto hiyo, ikibidi waje na mita za kikwetu zisizozungushwa na upepo isipokuwa maji tu.
 
Canon 2021

Member
Apr 10, 2021
41
150
Bili za maji ni changamoto.mim nlikuwa najiuliza maswali kama ya muuza mada pale nlipoletewa bill za 65 k kwa mwez.nna tank la lita 3000 na la 2000 na huwa sijazi mara kwa mara coz sina matumiz makubwa ya maji.Ila bill kwa mwezi ni kubwa sana.Hawa watu walitaka sifa sana kwa ukusanyaji wa mapato so wanaibia wananchi ili waonekana wanakusanya mapato vizuri
 
DeepPond

JF-Expert Member
Nov 18, 2017
14,268
2,000
Wewe kuwa makini na mita yako , labda mita waichokonee kijanja, kila mwezi angalia umefikia unit ngapi, waulize unit moja ni sh, ngapi? Zidisha na hizo unit utapata jibu. Kwangu haibiwi mtu!!
Nahisi mita zao Zina michezo ya ajabu,

Kuna mda wanakata maji kwa saa kadhaa alafu baadae wanarudisha.

Ukifungua bomba,
Unatoka upepo mkali na matone kidogo ya maji nkaribu nusu saa nzima.

ukivizia mita unaona inazunguka kwa kasi ya ajabu, unit zinatembea.
Na upepo nao unatoka kwa Kasi ya ajabu.

Nilipowaita,
wakaikagua mita wakasema mita yao MBONA iko sawa kabisa na tena imethibitishwana TBS.

Unabaki unajiuliza,
Ni Nini hiki kinaendelea hapa
 
DeepPond

JF-Expert Member
Nov 18, 2017
14,268
2,000
Bili za maji ni changamoto.mim nlikuwa najiuliza maswali kama ya muuza mada pale nlipoletewa bill za 65 k kwa mwez.nna tank la lita 3000 na la 2000 na huwa sijazi mara kwa mara coz sina matumiz makubwa ya maji.Ila bill kwa mwezi ni kubwa sana.Hawa watu walitaka sifa sana kwa ukusanyaji wa mapato so wanaibia wananchi ili waonekana wanakusanya mapato vizuri
Hawa jamaa wanafanya wizi wa mchaa kweupe kabisa
 
Mad Max

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
7,746
2,000
Tatizo nadhani ni sisi wenyewe. Wasomaji wa bili wanapewa kazi kwa kupewa target ya hela sio idadi ya mita.

Mfano: Mad Max hakikisha mwezi huu umekusanya shilingi Milion 10 kama bili ya maji.

Sasa hapo nikifika nakuta umetumia units 10 naweka 24 watu wenyewe hata hamfatilii.

Cha kufanya:

Kila mwisho wa mwezi mfano Tarehe 31/05 piga picha ya ile mita na zile namba, kisha ikifika tarehe 30/06 piga tena. Hafu tafuta tofauti.

Ukipata labda tofauti ni units 50.

Then zidisha mara gharama kwa unit moja (nadhani kama elfu 1 mia nane hivi kwa DSM).

Nyingine ikizidi labda gharama za uendeshaji ila haitazidi elfu 2.
 
TODAYS

JF-Expert Member
Apr 30, 2014
8,529
2,000
Hawa jamaa ni wezi sana, hasa kwa kuchokonoa meter kama haupo nyumbani na watakupa visingizio vilivyoenda shule.

👉🏾 Unit moja sawa na tshs 1660/-

But kuna wizi unaofanywa na wasoma meter wakishirikiana na mafundi wa idara za maji wa eneo husika. Kitu wanafanya ni kusogeza mshale au zile namba mpaka wanapoona hapa tutapata shs kadhaa, then wanafunga wanaenda kwa mwingine.

Yaani nchi hii mpaka Mwana wa Adam anarudi kila mtu lazima ataonja joto la jiwe!.
 
DeepPond

JF-Expert Member
Nov 18, 2017
14,268
2,000
Tatizo nadhani ni sisi wenyewe. Wasomaji wa bili wanapewa kazi kwa kupewa target ya hela sio idadi ya mita.

Mfano: Mad Max hakikisha mwezi huu umekusanya shilingi Milion 10 kama bili ya maji.

Sasa hapo nikifika nakuta umetumia units 10 naweka 24 watu wenyewe hata hamfatilii.

Cha kufanya:

Kila mwisho wa mwezi mfano Tarehe 31/05 piga picha ya ile mita na zile namba, kisha ikifika tarehe 30/06 piga tena. Hafu tafuta tofauti.

Ukipata labda tofauti ni units 50.

Then zidisha mara gharama kwa unit moja (nadhani kama elfu 1 mia nane hivi kwa DSM).

Nyingine ikizidi labda gharama za uendeshaji ila haitazidi elfu 2.
Wameshapandisha bei
2021-05-26-21-43-11.jpg
 
DeepPond

JF-Expert Member
Nov 18, 2017
14,268
2,000
Ndiyo tatizo la kuwa wategemezi kwenye teknolojia, moja ya changamoto tanazopata wateja wa maji ni bills kuwa kubwa na kutotafuta sababu, kuna mtaalamu alisema kwenye moja ya vipindi vya TV, maji yakikatika, yanaporudi kunakuwa na upepo ambao huzungusha mita.

Nilitegemea vyuo vyetu vikuu na vile vya ufundi vingetafuta namna ya kushughulika na changamoto hiyo, ikibidi waje na mita za kikwetu zisizozungushwa na upepo isipokuwa maji tu.
Vyuo havifanyi tafiti,
maprofesa wamehamia Kwenye siasa
 
Crimea

JF-Expert Member
Mar 25, 2014
17,841
2,000
Ndiyo tatizo la kuwa wategemezi kwenye teknolojia, moja ya changamoto tanazopata wateja wa maji ni bills kuwa kubwa na kutotafuta sababu, kuna mtaalamu alisema kwenye moja ya vipindi vya TV, maji yakikatika, yanaporudi kunakuwa na upepo ambao huzungusha mita.

Nilitegemea vyuo vyetu vikuu na vile vya ufundi vingetafuta namna ya kushughulika na changamoto hiyo, ikibidi waje na mita za kikwetu zisizozungushwa na upepo isipokuwa maji tu.
Mkuu hata kama lakini hiyo hela ni nyingi mno.

Kwa sababu kama ni kuzungushwa na upepo huo upepo unazungusha kwa siku ngapi hadi kufikia unit zote hizo.?

Inawezekana hivi vi mita vinakuwa na matatizo
 
Crimea

JF-Expert Member
Mar 25, 2014
17,841
2,000
Bili za maji ni changamoto.mim nlikuwa najiuliza maswali kama ya muuza mada pale nlipoletewa bill za 65 k kwa mwez.nna tank la lita 3000 na la 2000 na huwa sijazi mara kwa mara coz sina matumiz makubwa ya maji.Ila bill kwa mwezi ni kubwa sana.Hawa watu walitaka sifa sana kwa ukusanyaji wa mapato so wanaibia wananchi ili waonekana wanakusanya mapato vizuri
Kwani mita si iko kwako? Kwanini usiwe unasoma mwenye kujiridhisha unit ulizotumia?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom