Malcolm X5
JF-Expert Member
- Jun 3, 2013
- 1,637
- 2,747
Maneno hayo yamesemwa na Mmiliki wa Microsoft Na tajiri namba moja duniani Bwana Bill Gates,
Anasema,"inabidi kuwe na kodi iendanayo na Ujiendeshaji,kwa sasa,mfanyakazi binadamu,anayefanya kazi kiwandani,anayelipwa dolla za kimarekani 50,000,mapato hayo yanakatwa kodi,unapata kodi ya mapato,kodi ya mafao,vitu vyote hivyo.kama Robot anakuja kufanya kazi ile ile ya binadamu yule,utafikiria kuwakata kodi katika mlinganisho ule ule.Tajiri huyo alisema alipokuwa akihojiwa na kituo cha news website quarts,
Anaendelea kusema,"Serikali inabidi kuwakata kodi makampuni yanayotumia robots angalau kwa dharura kupunguza kutawanywa kwa matumizi ya Ujiendeshaji na kuwekeza aina nyingine za ajira.
"Mapato yanayoweza kukusanywa kutoka katika kodi hii,yanaweza kugharamia sehemu nyingine ambazo bado itakuwa inamtegemea binadamu,kama,Elimu,Huduma ya Afya na matunzo ya watoto na uzeeni",Bill alisema
Ingawaje wazo hilo la bilionea huyo si jipya,wiki mbili zilizopita watunga sheria wa umoja wa ulaya uliandaa plani kwa ajili ya kodi kwa wamiliki wa robot.Muswada huo ulilenga kuwapa nafasi mbadala kuwalipa wafanyakazi waliopoteza kazi zao kutokana na kuchukuliwa na marobot hao,au ROBOTIZATION,Hata hivyo,Muswada huo ULIPINGWA.
Tafsiri isiyo rasmi
Chanzo.RT Robots that take human jobs should pay taxes - Bill Gates