Bilioni moja papu iko kwa account

Mnyongeni Mnyonge

JF-Expert Member
Mar 13, 2015
628
726
Wana jf nawasalimu kwa moyo mnyoofu(hivi mkunjufu ndo sawa eeh)

Turudi kwenye mada kimsingi bilioni moja sio pesa ya mchezo mchezo kwa mfano nkiipata mimi ntaifanyia nini??
Kwanza:kuipata hiyo bilioni moja najua siwezi ila kwa wastani nkiwaalika wapelelezi watatu kutoka scotland yard police naiweza kuipata kirahisi kwan gawiwo lao ni milion mia nne keshi ntawapatia ambzo watajua wao wafanyie nn
Pili: kimahesabu ntabakiwa na milioni mia sita ambazo kwenye biashara yangu nahitaji milioni mia mbili tuu kwa kuanzia so milion 200 ztaingia kwenye biashara yangu chapu kwa haraka
Tatu: ntabakiwa na milioni mia nne kwanza ntafanya sherehe ya kuuaga umaskini ntavuruga kama milioni 20 afu milion 80 zitakuwa nmezimwaga kwenye nyumba ntakayotaka kuishi ambapo kale kakiwanja kangu pale kigamboni ntaweka mjengo wangu wakisasa kupumzika na dada yenu nkiwa natafuta usingizi kila iitwayo leo asubuhi viwili mchana viwili usiku vinne kwa raha zangu
Nne:nisikufiche lazima ninunue usafiri wakutembelea bhana wakati ndo huo wife atapata noah yake ya milioni kumi na mm ntachukuwa Land cruser yangu mayai wenyewe mnaita shangingi ili nkitaka kwenda hapo home chapu mbeya hii hapa saa tisa nakula ugali kwa bimkubwa hii nachukua second hand milioni 60 jumla milion 70 zitakatika hapo wife na mimi milion 30 nanunua mahitaji ya nyumbani kwanza mtv mmoja wa maana wenyewe mnaita smati tivi inchi 60 ili niangalie taarifa ya habari(nmechoka kuangalia kwa jirani)
Nne:Bi mkubwa na mshua pale mbeya sitawaacha hivi hvi nao nitawapatia milioni 25 na milioni nyingine 25 ntawarekebishia nyumba yao ile inayoezuliwa na upepo ikae sawa mshua anafuga sana mifugi ntampa kagari kirikuu na passo yakuendea kanisani kuabudu na dogo langu atakula 50milioni keshi afanyie mambo yake mana ndo anaanza maisha
Tano na mwisho:nabakiwa na milioni mia hizi ndo zakuanzia maisha na kubaki apu ile bizinesi maisha murua mustarehe

Kama ndoto eeh lakini ni kweli bilioni moja mkononi

Mipango Matumizi buana
 
Back
Top Bottom