BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,007
Bilioni 40 /- za mafisadi zanufaisha wakulima
Mwandishi Wetu
Daily News; Friday,December 19, 2008 @21:15
Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Stephen Wassira amesema wakulima nchini wameanza kunufaika na fedha za Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) kwa kuongeza thamani ya vocha kwa ajili ruzuku za mbolea na mbegu.
Alisema thamani ya vocha hizo zimeongezeka na kufikia Sh bilioni 70.7 ambalo ni ongezeko la Sh bilioni 40 za EPA na tayari mawakala wamewasilisha vocha za malipo za Sh bilioni nne. Rais Jakaya Kikwete aliamuru kuwa fedha zilizorejeshwa na mafisadi wanaotuhumiwa kuchota Sh bilioni 133 katika akaunti hiyo ya Benki Kuu ya Tanzania zitakwenda kusaidia sekta ya kilimo.
Tayari Sh bilioni 70 zimesharejeshwa na watuhumiwa hao ambao kati yao, 21 wameshapandishwa mahakamani wakituhumiwa kwa wizi huo. Akizungumza Dar es Salaam jana kuhusu ufikishwaji wa pembejeo za ruzuku kwa wakulima kwa kutumia vocha, Wassira alisema fedha hizo zinanufaisha wakulima 700,000 huku Benki ya Dunia ikiahidi kusaidia fedha kwa wakulima 300,000 kuanzia msimu huu wa kilimo hivyo kunufaisha jumla ya wakulima milioni moja.
Alisema matumizi ya vocha yatamnufaisha mkulima moja kwa moja bila kupitia kwa wakala mwenye vigezo vya kuwa mkulima mdogo mwenye uwezo wa kufidia tofauti za bei na atakayefuata maelekezo ya Ofisa Ugani. Alisema aina za mbolea zinazopata ruzuku ni mbolea za kupandia na za kukuzia na kuwatoa hofu wakulima nchini kuwa mbolea ya Minjingu inafaa kama kirutubisho cha fosfati kwani imefanyiwa utafiti wa kutosha na kuonekana inafaa.
Tumefanya utafiti katika Wilaya ya Kilombero Morogoro na Igomela na Mbarali Mbeya ambako wakulima wa mpunga wa Kijiji cha Mkula wameweza kuongeza uzalishaji kutoka wastani wa gunia sita kwa ekari hadi gunia thelathini kwa ekari kwa kutumia mbolea hiyo ya Minjingu, alisema.
Kuhusu upungufu wa chakula, Waziri alisema watu 240,000 wanakabiliwa na upungufu huo na serikali inatakiwa kupeleka tani 7,000 za chakula kwa ajili ya kusaidia wilaya kadhaa zinazokabiliwa na upungufu wa chakula. Alitaja baadhi ya wilaya zinazokabiliwa na upungufu wa chakula kuwa ni Longido, Same, Monduli, Mwanga, Rombo, Bunda, Musoma Vijijini, Rorya, Kwimba na Ukerewe, lakini alisema wilaya hizo ni kwa sehemu ndogo na hali ya chakula nchini ni ya kuridhisha.