Bilioni 4 zimetengwa kutatua changamoto za barabara ndani ya manispaa ya Temeke

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,854
930
Mhe. Jokate Mwegelo: ZAIDI YA BILIONI 4 KUBORESHA BARABARA TEMEKE.

Kiasi cha fedha zaidi ya shilingi bilioni nne kimetengwa kwa ajili ya kutatua changamoto za barabara ndani ya manispaa ya Temeke katika bajeti ya mwaka wa fedha 2022/23.

Hayo yameelezwa na Mratibu wa Wakala wa Barabara za Mjini na Vijijini(TARURA) wa Wilaya hiyo Injinia Paul Mhere leo Januari 22,2022 katika kikao cha kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa miradi ya barabara kwa mwaka 2021/22 na mpango wa mapendekezo ya bajeti ya 2022/23 kilichofanyika ukumbi wa Iddi Nyundo.

Akiwasilisha taarifa hiyo mbele ya baraza la madiwani na wataalamu wa manispaa ya Temeke,Mhere amesema kiasi hicho kimetengwa ili kuondoa changamoto za ubovu wa barabara hizo ambazo zitajengwa kwa viwango tofauti ikiwemo changarawe,lami na nyingine kuchongwa tu.

"Mpaka sasa tumeshapokea zaidi ya bilioni moja kati ya hizo bilioni nne ambapo zitakazoenda kupunguza kabisa tatizo hili na tumegusa barabara za kata zote".Alisema Injinia huyo.

Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe.Jokate Mwegelo ameuelezea mpango huo kama mkombozi kwa wanatemeke ambapo utaenda kubadilisha mandhari ya barabara za wilaya ya Temeke ambazo nyingi zimekuwa hazipitiki hasa katika msimu wa mvua.

"Nimpongeze Mheshimiwa Rais mama Samia Suluhu Hassan kwa kutupatia fedha hizi ambazo zitatumika kujenga barabara zetu".Aliongeza Jokate.

Baadhi ya madiwani wamepongeza utaratibu wa ushirikishwaji katika kupanga mipango ya maendeleo hali inayowapa nafasi kuwasilisha changanoto halisi zinazowakabili wananchi katika maeneo yao.

"Kipindi cha nyuma unakuta greda lipo mtaani kwako unapigiwa simu na wananchi wanakueleza kuwa barabara huku inajengwa,mwananchi anashangaa na wewe diwani unashanga.Wote mnabaki kushangaa".Alisema diwani wa kata ya Chang'ombe Mhe.Kelvin Mhedze.

Kikao hicho kilichokuwa mahususi kwa ajili ya kupitia mapendekezo hayo kimemalizika huku pande zote zikitoka na kauli moja huku madiwani wakiunga mkono mapendekezo hayo na wengine wakitoa ushauri wa kunoresha mapendekezo hayo.

IMG-20220122-WA0117.jpg


IMG-20220122-WA0118.jpg


IMG-20220122-WA0119.jpg
 
Back
Top Bottom