Bilioni 20 alizotoa mwekezaji MO Dewji kwenye club ya simba ni changa la macho?

Nyie uto ndio mnajifanya kuhangaika na hizo b20 kuliko Simba?
Simba wanajua vema wanachokifanya hivyo acheni kudandia mbele biashara msiyoifahamu.
Endeleeni kushona madela.
 
Nimefuatilia kwa ukaribu mahojiano ya mwenyekiti mpya wa bodi ya club ya simba bw. Salum Abdallah katika kipindi cha sports HQ kinachorushwa na kituo cha redio cha E-fm, nimegundua kuna ukanjanja mkubwa kuhusu bilioni 20 alizotoa mwekezaji Mo Dewji katika club yake hiyo ya simba.

Kama mtakumbuka siku Mo dewji ameitisha mkutano na waandishi wa habari 'press conference' kukabidhi kitita hicho cha pesa aliwatolea uvivu na kuwashukia vikali wale wote waliokuwa wanasema kuwa hana pesa.

Katika kuwathibitishia kwamba anazo, mwekezaji Mo Dewji alisema maneno machache yafuatayo, nanukuu "Lakini kuna watu wanasema Mohammed Dewji hana pesa, leo hii nakabidhi cheki ya Sh 20 Bilioni za hisa asilimia 49 kwa klabu ya Simba," hivyo Mo dewji alithibitisha kwamba ana pesa kwa kuonyesha checki hiyo yenye thamani ya bilioni 20 za kitanzania kama malipo ya 49% ya hisa alizowekeza katika club ya simba.

Lakini katika hali isiyo ya kawaida katika mahojiano ya jana, mwenyekiti mpya wa simba bw. Salum abdallah "Mr Try again" alikanusha vikali kwamba mwekezaji Mo dewji hakutoa cheki bali alitoa Transaction notes. Sasa kwa kuanzia ili kupata undani na ukweli wa hizo bilioni 20 tujiulize ni kwanini watu hawa wawili kauli zao zina kinzana? Mwingine anasema ni cheki, mwingine anasema ni transaction notes, je ukweli kuhusu hili ni upi?

Kuhusu benki kilipowekwa kiasi hicho cha pesa, mwenyekiti anasema pesa zimewekwa kwenye akaunti maalum ila hataji jina la benki kwa mdai kuwa ndivyo walivyokubaliana. Je, hayo makubaliano ya kutotaja jina la benki ni kati ya nani na nani? Mwekezaji na benki au mwekezaji na uongozi wa club? Je, kwanini benki kilipowekwa kiasi inafanywa kuwa siri? Nani ana monitor hiyo akaunti maalum kilipowekwa kiasi hicho cha pesa? Kwanini kiasi hicho cha pesa kiliwekwa kwenye akaunti maalum na sio akaunti za kawaida za club ya simba?

Hatahivyo, kupitia jicho langu la tatu la kimchezo nimegundua kuna changa la macho katika hizo bilioni 20 zilizotolewa na mwekezaji 'Mo'.

kwakuwa amesoma upepo wa club katika msimu huu kuwa sio mzuri ameona ajivue mapema uenyekiti na kumwachia swahiba wake amtunzie siri ili ukanjanja huu usibumbuluke kwani kama simba ikiendelea kufanya vibaya uwanjani, mashabiki na wanachama watataka kujua mapato na matumizi ya club hasa kujua matumizi ya hizo bilioni 20 hewa alizozitoa mwekezaji kanjanja 'Mo' na kama itatokea wanachama wakahoji matumizi ya hizo bilioni 'hewa' ndio utakuwa mwanzo wa mwekezaji huyo kanjanja kutangaza kujiuzulu kuwa mwekezaji wa club hiyo. MUDA UTASEMA...
Naona msuko wa mudi kuweka lile bango simba ni kujitetea juu ya msimu unavyo kwenda kuwa wa ovyo kwa simba
 
Kwani GSM ni mwekezaji? Kwa Elimu yako ndogo ya kikolo uliyonayo
Safi kabisa kama ile mlionayo manyani fc

3ECCD243-D478-4A80-AEBF-AF46D92F6BEF.jpeg
 
Hawana majibu labda wataishia kunitukana tu ndicho wanachoweza
Acha wenge mkuu, zile pesa kabla hazijatoka walisema kabisa kuwa zitawekwa akaunti maalum then kitakachotumika sio zile pesa bali faida itakayotokana na zile fedha,
 
Back
Top Bottom