Bilioni 185 za DOWANS ni hela chache sana kwangu - Rostam Aziz | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bilioni 185 za DOWANS ni hela chache sana kwangu - Rostam Aziz

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Malafyale, Jan 6, 2011.

 1. Malafyale

  Malafyale JF-Expert Member

  #1
  Jan 6, 2011
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 11,214
  Likes Received: 3,626
  Trophy Points: 280
  Tanzania Daima(January 6,2011)

  Rostam alisema jambo pekee analokiri kupata kulifanya ni kuwashawishi wamiliki wa kampuni ya Dowans Holdings SA iliyorithi mkataba wa Richmond kuja kuwekeza nchini katika sekta ya umeme.

  “Mimi nilishiriki katika kuwashawishi Dowans kuja nchini. Nitaendelea kushawishi wawekezaji waje nchini ili nchi iendelee, ajira ipatikane na kodi ziongezeke. “Juzi tu nimetoka Singapore, Malaysia na UAE (Falme za Kiarabu) kuwashawishi wawekezaji kuwekeza kwenye usafiri wa anga,” alisema Rostam.


  Alipotakiwa kueleza iwapo yeye ni mmoja wa watu wanaotarajia kufaidika na malipo ya shilingi bilioni 185 ambazo TANESCO inatakiwa kuilipa fidia Dowans, mfanyabiashara huyo alikana kuimiliki kampuni hiyo.
  Mbali ya kukanusha hilo, Rostam aliyabeza madai ya baadhi ya wanasiasa wanaohusisha fedha hizo na yeye akisema katika mkusanyiko wa biashara zake anazofanya ndani na nje ya nchi kiasi hicho cha fedha wanazotarajiwa kulipwa Dowans ni sawa na mapato yake ya miezi minne tu.
   
 2. marejesho

  marejesho JF-Expert Member

  #2
  Jan 6, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 6,539
  Likes Received: 830
  Trophy Points: 280
  Vijisenti
   
 3. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #3
  Jan 6, 2011
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo yeye ni BIG TAX PAYER HAPA TANZANIA? Forward Hotuba yake TRA ili wakakusanye mapato ya kodi ya mapato
   
 4. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #4
  Jan 6, 2011
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,004
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  Natafuta uchawi kwa gharama yeyote niweze kuwafikia watu km ra usiku kuwageuza sambusa
   
 5. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #5
  Jan 6, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  I hope TRA wana hii habari ili waifanyie kazi na kuhakikisha kuwa Kodi anazolipa zinaendana na hayo mapato.
   
 6. T

  Tsidekenu Senior Member

  #6
  Jan 6, 2011
  Joined: May 7, 2009
  Messages: 141
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  hahahaaaaa, uminichekesha, kweli watanzania wamechoka na hii mijitu!!!! yani unataka kuwageuza sambusa?:wink2:
   
 7. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #7
  Jan 6, 2011
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135

  Anauza bangi ile ya Afghanistan?
   
 8. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #8
  Jan 6, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Mshenzi sana huyu jamaa anatuibia halafu anatutusi hadharani na tunamchekea hivi hii serikali ya JK kaiweka mfukoni kwake?
   
 9. kaburunye

  kaburunye JF-Expert Member

  #9
  Jan 6, 2011
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 675
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Haya ndo maneno ya Rostam Aziz kama alivyonukuliwa na gazeti la TZ daima leo:

  “Mimi nilishiriki katika kuwashawishi Dowans kuja nchini. Nitaendelea kushawishi wawekezaji waje nchini ili nchi iendelee, ajira ipatikane na kodi ziongezeke.
  “Juzi tu nimetoka Singapore, Malaysia na UAE (Falme za Kiarabu) kuwashawishi wawekezaji kuwekeza kwenye usafiri wa anga,” alisema Rostam.

  Huyu jamaa anafanya haya kama nani??? Hivi kweli ana mapenzi mema na nchi yetu anaposhawishi wawekezaji kuja hapa nchini??? au ndo kutuletea makampuni ya kifisadi kuja kuiba rasilimali zetu!!! RA si mzalendo kiasi hicho na ninaomba aiache nchi yetu. Madudu aliyotufanyia (Kagoda, Richmond, Dowans) yanatosha jamani. Hii kazi amwachie waziri husika
   
 10. YanguHaki

  YanguHaki Senior Member

  #10
  Jan 6, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 129
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Aiseh, analipa kodi ya mapato kiasi gani kwa Taifa hili? Ninavyojua mimi anaweza asilipe hata bilioni moja kwa mwaka! Bongo hii na UFISADI!
   
 11. andrewk

  andrewk JF-Expert Member

  #11
  Jan 6, 2011
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 3,103
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Tra kazi hiyooo
   
 12. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #12
  Jan 6, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,167
  Likes Received: 1,251
  Trophy Points: 280
  Katumwa na swahiba wake JK ili alete wachotaji wengine
   
 13. kaburunye

  kaburunye JF-Expert Member

  #13
  Jan 6, 2011
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 675
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Kwa hiyo inawezekana JK ana mabaraza 2 ya mawaziri. Mawaziri wa kuhudhuria vikao formal za baraza na wale underground!!! Nadhani EL bado ni waziri mkuu underground
   
 14. O

  Ogah JF-Expert Member

  #14
  Jan 6, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Kweli RA ni SMART sana.............unajua nini!...............ni kweli kabisa anachosema RA............tena hapo kajumuisha tu na biashara za nje........biashara zake za ndani tu kwa mwezi mmoja au miwili anapata hizo pesa.......pesa hizo ni ndogo sana kwake
   
 15. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #15
  Jan 6, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Pesa zote hizo za kazi gani wakati unaendelea kuona mafukara na vumbi nyumba ya pili kutoka kwako!
   
 16. S

  S.M.P2503 JF-Expert Member

  #16
  Jan 6, 2011
  Joined: Nov 25, 2008
  Messages: 463
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Kama kweli ana uchungu na Tanzania si alilipe deni hilo ...tutamuona wa maana na wananchi wa Igunga watafurahi kwa kumchagua kuwa mbunge wao...
   
 17. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #17
  Jan 6, 2011
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,008
  Trophy Points: 280
  Kama aliwashawishi basi anawajua, kwa nini asiwataje hao wenye hiyo kampuni
   
 18. Kamaka

  Kamaka JF-Expert Member

  #18
  Jan 6, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 565
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Tra ndo hao hao....hawana meno.
   
 19. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #19
  Jan 6, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Kwahiyo yeye ndio aliyoshiriki kuleta huo uozo nchini??? na bado anaendelea kutafuta wengine? Kama idea yake ya wawekezaji ni watu kama Dowans namuomba hiyo shughuli angewaachia wengine.
   
 20. M

  MzeePunch JF-Expert Member

  #20
  Jan 6, 2011
  Joined: Jun 8, 2009
  Messages: 1,412
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Nina hasira sana na fisadi huyu. Atakayemuona akikatiza huko mitaani anishtue.
   
Loading...