Bilioni 18.77 zatumwa kwenye akaunti za Shule za Msingi na Sekondari za Halmashauri zote nchini

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,811
Bilioni 18.77 Zimetumwa Kwenye Akaunti Za Shule Za Msingi Na Sekondari Hapa Nchini Kwa Ajili ya Wanafunzi Kusoma Bure

KIASI cha shilingi bilioni 18.77 zimetumwa kwenye akaunti za shule za Msingi na Sekondari za halmashauri zote hapa nchini kwaajili ya wanafunzi kusoma bure.

Hayo yamesemwa na Waziri wa fedha na Mipango, Dk. Philip Mipango wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.

Pesa hizo zimegawanywa kwenye akaunti za shule za shule za Msingi na Sekondari katika halmashauri zote kiasi cha shilingi bilioni 15.7 na bilioni 3 kwenye akaunti vyombo vya usimamizi wa mitihani katika Halmashauri zote hapa nchini.

Dk.Mipango amewatahadharisha wakuu wa Mikoa, wakuu wa Wilaya na wakurugenzi wa Halmashauri zote kutumia ipasavyo pesa hizo kwa kuwa zikitumika kwa matumizi mengine watalala nao mbele kwa kula jasho la wananchi.

Pia Waziri wa fedha na Mipango, Dk. Mipango amewaomba waalimu wakuu wa shule zote za Msingi na Sekondari katika halmashauri zote hapa nchini waweke wazi matumizi ya fedha hizo katika mbao za matangazo kwa kila shule ili kila mzazi aweze kujua kiasi
gani kimetumika.

Gavana wa Benki kuu ya Tanzania, Beno Nduru akifafanua jambo kwenye mkutano wa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. Kulia Katibu Mkuu wa wizara ya Fedha na Mipango, Servacius Likwelile.

Kaimu kamishna mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), Alfayo Kidata akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, kuhusiana na ukusanyaji wa mapato katika Malaka ya Mapato Tanzania kwa kila robo mwaka.

 
Last edited by a moderator:
Mwanzo mzur tukishirikiana kwa pamoja inaezekana,,,rai kwa wale wanaopenda majaribu maana hizo pesa wakicheza nazo kwa manufaa binafs wataishia magerezan
 
Nina mashaka na utekelezaji wa mpango huu ila iwapo utekelezaji utafanikiwa hii itakuwa nafuu ya kwanza ktk elimu kwa wananchi wa hali ya chini! naomba kujua iwapo pesa hii inahusu maslahi ya walimu na vifaa ama vitendea kazi mashuleni!
 
Mwnzo mzuri magufuli tumethubutu tumeweza na sasa tunasonga mbele chapa kazi Rais wetu.
 
Nina mashaka na utekelezaji wa mpango huu ila iwapo utekelezaji utafanikiwa hii itakuwa nafuu ya kwanza ktk elimu kwa wananchi wa hali ya chini! naomba kujua iwapo pesa hii inahusu maslahi ya walimu na vifaa ama vitendea kazi mashuleni!
Kwa magufuli itawezekana tu hakuna mchezo wa kuchekeana hapa lazima sheria zifuatwe hayupo mshenzi yoyote wa kucheza na serikali ya magufuli.
 
sasa jmn tuwe wa kweli tu shule inamlinzi na mshahara wake ni 60 elfu jmn kwahy chaki hapo zitatosha au inakuwaje au mchanganuo wake umezingqtia mambo ya msingi!?
 
Ni safi sana hiyo ya kesema kila shule ikipokea kiasi fulani cha hela kiwe wazi ili hadi wazazi waweze kuona jinsi hela zilivyo tumika
 
thanks, time will tell!

Watanzania tusie na roho mbaya na akili finyu na kua negative. Raisi peke yake hawezi kufanikisha, anahitaji support ya wananchi pia. Sio kusema tu time will tell, ujue aidha ni wewe au mtoto wako au mjukuu wako atakae nufaika.
 
Hizi pesa ni kama chambo na hakika kitawavua wengi na wengi watalia sana ( kwa jinsi ninavyomjua Magufuli na mawaziri wake)
 
sasa jmn tuwe wa kweli tu shule inamlinzi na mshahara wake ni 60 elfu jmn kwahy chaki hapo zitatosha au inakuwaje au mchanganuo wake umezingqtia mambo ya msingi!?
Pesa zinatolewa kwa awamu. Kama una kumbukumbu, rais alitangaza kuwa kiasi cha zaidi ya bilioni 130 kimetengwa kwa ajili ya mashule...Hivyo hii pesa ni awamu ya kwanza, usitarajie pesa yote kiasi cha bilioni 130 kitolewe kwenye halmashauri zetu, ndio utakuwa mwanzo wa ufisadi.
 
Halafu wasiweke tu taarifa za matumizi kwenye mabango mashuleni bali pia wahakikishe wanafanya kwa maandishi na kuwapa wanafunzi wote barua ili wazazi wawe na nakala za barua hizo kama ushahidi.
 
Ukisema hivyo zinaweza kuonekana nyingi...., ila ukiangalia ni Kiasi gani per head, kwa Primary, Secondary na Shule za Bweni na za Kutwa utagundua kwamba mzigo kwa mzazi bado upo pale pale.... Matumizi mengine ni maradufu ya hayo na ukizingatia ufanisi duni hapo ukiongezea pesa ya Tuition ndio mzazi anajikuta anatoa pesa zaidi kwenda Tuition
 
Back
Top Bottom