singidadodoma
JF-Expert Member
- Nov 11, 2013
- 4,394
- 1,536
Ni upuuzi wa waandishi huu fedha ni za serikaliIweje ziitwe za Magufuli wakati walitakiwa wapewe sio hisani?
Wafikiriwe kuongezwa posho. Kutoka ile buku 7 ifike hata 20 kutokana na ushauri wa Mwenyekiti kule Singida. Ingawa yeye alitaka Pombe awakumbuke kwa kupitia serikali kwani hali ya chama ni dhoofu hilo sidhani kama litakubalikahawa vijana 46 kazi yao kuja na vijaruda tu huku.....
Pamoja na mapungufu yote hayo ya miaka ya nyuma kwa maana ya viporo katika utekelezaji kutokana na ufinyu mkubwa wa bajeti, imekuwaje bajeti ya mwaka huu IKAWA NDOGO KIASI HICHO wakati mipango ya kuanzia mwaka 2012 "ilikuwa haijatekelezwa"?KWA mara ya kwanza Mahakama ya Tanzania imepokea asilimia 100 ya bajeti ya maendeleo kwa ajili ya kuhakikisha wanafanikisha huduma za utoaji wa haki kwa wananchi, imeelezwa.
Jaji Mkuu Mohammed Chande Othman alieleza hayo jana Dar es Salaam wakati akimshukuru Rais John Magufuli kwa kutekeleza ahadi yake ya kuwapa Sh bilioni 12.3 aliyoahidi Siku ya Sheria, Februari 4, mwaka huu ili kutekeleza miradi yao ya maendeleo.
Jaji Othman alimshukuru Rais kwa kulipa kipaumbele suala la miundombinu na ujenzi wa mahakama ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya utoaji haki kwa wakati, kwa kuwa katika kipindi cha nyuma bajeti zilikuwa pungufu, jambo lililosababisha washindwe kutekeleza miradi yao ya maendeleo.
Alisema “kutokana na vipaumbele vingi vya serikali katika kipindi cha mwaka 2012/2013 bajeti ilikuwa bilioni 26.6 pungufu ilikuwa asilimia 78, 2013/2014, bajeti shilingi bilioni 42.7 pungufu asilimia 82, 2014/2015 shilingi bilioni 41.5 pungufu ilikuwa asilimia 92 lakini mwaka huu bajeti ni bilioni 12.3 na hakuna upungufu katika bajeti yetu.”
hapo utaambiwa kwenye Kilimo bajeti haitoshi,kwenye Elimu bajeti haitoshi, kwenye utafiti bajeti haitoshi,kwenye Afya bajeti haitoshi, kweli huu ni utawala wa kukurupukaNi upuuzi wa waandishi huu fedha ni za serikali
Katika bajeti ya kila wizara kuna fungu la matumizi na fungu la maendeleo na mgawanyo huwa hivyo hadi kwenye idara, katika idara ya mahakama fungu la maendeleo haliku kidhi kwa kiasi cha Bil.12 ikiwa na maana kulikuwa na deficit ni baada ya Rais kutoa kiasi hicho bajeti yao ya maendeleo sasa imekamilika kwa asilimia100% sijui kama niko sahihi na nime eleweka.hapa hata sielewi,bajeti kutoka bil 41.5 2014/2015 hadi bil 12.3 2015/2016? je,hii asilimia mia moja ya bajeti ya mwaka huu sio asilimia arobaini ya bajeti zilizopita ambazo hazikusaidia kuondoka changamoto zinazoikabili mahakama.
yawezekana ikawa hivyo,maana wanasema bajeti ya maendeleo,hii nafikiri ni tofauti na ile ya matumiszi ya kila siku kama vile mishahara.Ila mkanganyiko ni hapo Jaji aliponukuliwa akisema bajeti za miaka iliypopita,kwa maana kwamba alimaanisha hizohizo za maendeleo au hapo alisema kwa ujumla wa bajeti yote?Katika bajeti ya kila wizara kuna fungu la matumizi na fungu la maendeleo na mgawanyo huwa hivyo hadi kwenye idara, katika idara ya mahakama fungu la maendeleo haliku kidhi kwa kiasi cha Bil.12 ikiwa na maana kulikuwa na deficit ni baada ya Rais kutoa kiasi hicho bajeti yao ya maendeleo sasa imekamilika kwa asilimia100% sijui kama niko sahihi na nime eleweka.
Ni amini kuwa alizungumzia bajeti ya maendeleo tu maana wizara zote kilio ni mapungufu katika bajeti za maendeleo, za matumizi ya chai na vitafunwa huwa hazina kelele sana, na hapo ndio usishangae uchumi kudumaa na nchi kuwa tegemezi.yawezekana ikawa hivyo,maana wanasema bajeti ya maendeleo,hii nafikiri ni tofauti na ile ya matumiszi ya kila siku kama vile mishahara.Ila mkanganyiko ni hapo Jaji aliponukuliwa akisema bajeti za miaka iliypopita,kwa maana kwamba alimaanisha hizohizo za maendeleo au hapo alisema kwa ujumla wa bajeti yote?