mamayoyo1
JF-Expert Member
- Jul 25, 2018
- 1,011
- 1,019
Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) wametia saini mikataba wa miradi mikubwa sita ya usambazaji maji kwa mkoa wa Dar es Salaam na Pwani wenye thamani ya Bilion 114.5. Utiaji huo wa saini umefanyika leo Julai 2, 2019 katika ofisi za Mamlaka hiyo huku ukishuhudiwa na Waziri wa Maji Prof Makame Mbarawa, Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso, Waziri wa TAMISEMI Selemani Jaffo, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega, Bodi ya DAWASA ikiongozwa na Mwenyekiti Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange na Wakuu wa Wilaya kutoka Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani.
Kabla ya utiaji saini, Waziri wa Maji Prof Makame Mbarawa amewataka Mamlaka hiyo kusimamia vizuri miradi yote na kutafuta wakandarasi watakaofanya kazi kwa uweledi na kumaliza kwa wakati na muda mfupi ili wananchi wapate majisafi na salama. “Mamlaka mnaposimamia vizuri miradi ya maji, na kupata mkandarasi atakayefanya kazi kwa weledi na kumaliza ujenzi wa mradi kwa muda mfupi basi wananchi watapata majisafi na salama,” amesema Prof. Mbarawa.
Profesa Mbarawa amesema, li kufikia lengo la serikali la kumtua mama ndoo kichwani kwa asilimia 95 kwa mijini na asilimia 85 kwa vijijini na hilo linawezekana iwapo miradi midogo na mikubwa kusimamiwa vizuri na wakandarasi kumaliza kazi kwa wakati. Akitoa taarifa fupi ya miradi hiyo, Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema kwa sasa mkoa wa Dar es Salaam unapata maji kwa asilimia 85 na kukamilika kwa miradi hiyo mikubwa itafikia malengo ya serikali ya asilimia 95 kufikia mwaka 2020.
Amesema, katika kutekeleza miradi hiyo fedha zinazotumika ni za ndani zinazotokana na makusanyo ya mapato ya kila mwezi ambapo ndani ya miaka nne wameweza kuongeza ukusanyaji kutoka bilioni 3.2 hadi 11.2 kwa mwezi na asilimia 35 za mapato zinatumika kwenye ujenzi wa miradi ya maji. Nae Mwenyekiti wa Bodi ya DAWASA Jenarali Mstaafu Davis Mwamunyange ameeleza changamoto mbalimbali ndani ya mamlaka hiyo ila ameahidi kushirikiana na menejimenti kukabiliana nazo ikiwemo upotevu wa maji na wateja kupewa ankara za maji tofauti na matumizi yao.
Miradi iliyowekewa saini ni mradi wa bomba la kusafirisha maji kutoka Jeti hadi Buza wenye wenye urefu wa Km 7.5 na litahudumia maeneo ya Kiwalani Vituka, Buza, Mashine namba 5 – Tandika na Mwanagati na wakazi 173,810 wa kata za Vituka na Buza watapata huduma ya maji kwenye awamu ya kwanza.
Mradi mwingine ni mradi wa usambazaji maji utakaoanzia matanki ya Chuo Kikuu mpaka Bagamoyo awamu ya pili, mradi wa kuchimba visima 20 vya Kimbiji Mpera, mradi wa usambazaji maji Kisarawe hadi Pugu, mradi wa maji katika mji wa Mkuranga na mradi wa bomba la kusafirisha maji kutoka Mlandizi (Ruvu juu) hadi Kijiji cha Mboga Chalinze.
Viongozi mbalimbali hususani wawakilishi wa wananchi wameishukuru Serikali ya awamu ya tano chini ya Dkt John Pombe Magufuli kwa kuwezesha miradi mikubwa kama hiyo kwenda katika maeneo mbalimbali nchini pamoja na kutekeleza ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM).Na Zainab Nyamka na Cathbert Kajuna, Michuzi TV.