Bilionea wa mpunga mkulima aliyeitwa na Bill Gate, gari za kifahari, jumba kiwanda

Pascal_TZA

Member
Mar 25, 2014
17
36
Karibu nikukutanishe na mkulima kutoka Jijini Mbeya Rafael Saimon Ndelwa, Mmiliki wa Kampuni ya Rapha Group iliyo Uyole Mkoani hapo.

Rapha ni miongoni mwa Mabilionea wa Mkoa wa Mbeya na utajiri wake unatokana na Kilimo cha mpunga, kilimo ambacho kilimfanya Bilionea Bill Gate amuite ili waweze kujadili amewezaje kufanikiwa katika kilimo hicho.

Uwezo wake wa kukopesheka na Benki ni zaidi ya BILIONI 3

Raphael Saimon ameelezea kuwa alianza kwa kulima kwa kutumia jembe na kuanza kufanya biashara ya kuuza mpunga katika Mikoa mbalimbali Tanzania na kupelekea kuwa mzalishaji bora wa zao la mpunga kutoka jijini Mbeya.

"Nilikuwa nauza zao la mpunga katika Mikoa ya Tanga, DSM, Morogoro na kuanza kupeleke zao hilo hadi nje ya Tanzania na sababu kubwa iliyopelekea kufanikiwa mpaka hapa ilikuwa nikununua mashine kubwa za kukoboa mchele kutoka nchini India na kuongezeka kwa uzalishaji". Rapha

Rapha anasema Balozi kutoka nchini Marekani ndiye aliyefanya mpango wa kumkutanisha na Bill Gate baada ya kuona mafanikio aliyofikia na kupewa tunzo ya kuwa Mfanyabiashara mdogo na alishindanishwa na wafanyabiashara kutoka Afrika Kusini, Nigeria lakin kupitia kampuni yake RAPHA GROUP akafanikiwa kutwaa tunzo ya mfanyabiashara bora barani Afrika.

Katika maisha nimuhimu kujituma ilikufanikisha ndoto za maisha yetu Pia na serikari iwena msaada kwa wafanyabiashara ilikufanikisha malengo ya wananchi wake wanafanikiwa.

 
Kwako wewe bilionea Lina maanisha mtu aina gani? Ikiwa uwezo wake wa kukopesheka ni zaidi ya 3b manake turnover yake ni zaidi ya hapo. Labda utuambie jinsi wewe unavoifahamu je biashara yake haina hiyo thamani?
Bilionea ni mtu ambaye total wealth yake ipo above 1bilion for all major Currencies in world ($£€).
Ndio maana hata Messi na Neymar sio mabelione
 
Karibu nikukutanishe na mkulima kutoka Jijini Mbeya Rafael Saimon Ndelwa, Mmiliki wa Kampuni ya Rapha Group iliyo Uyole Mkoani hapo.

Rapha ni miongoni mwa Mabilionea wa Mkoa wa Mbeya na utajiri wake unatokana na Kilimo cha mpunga, kilimo ambacho kilimfanya Bilionea Bill
Huyu jamaa amewekwa juu sana bila sababu,kiasi mnataka kumfarakanisha na TRA.Hebu tuambie utajiri wake ni kiasi gani.(Chukua mali zake zote toa Madeni yote)
 
Kwako wewe bilionea Lina maanisha mtu aina gani? Ikiwa uwezo wake wa kukopesheka ni zaidi ya 3b manake turnover yake ni zaidi ya hapo. Labda utuambie jinsi wewe unavoifahamu je biashara yake haina hiyo thamani?
Billioni 3 dola au shillingi? Maana kama ni shillingi, hiyo ni dola millioni moja na laki tatu. Kuna watanzania wanapata mshahara wa zaidi ya $ millioni moja. Ila kama ni $ basi mwenzetu yuko mbali na sisi.
 
Raphael Group ni kweli ana pesa na ata uwekezaji wake pale uyole ni mkubwa ila sio kusema ni billionea wa kutisha vp kuhusu Machemba alaf Raphael halimi sana mpunga yeye ananunua na kukopesha wakulima wakubwa wa mpunga mbeya wapo mbarali na kwenye list yeye hayupo kabisa
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom