Bilionea wa Japan anatafuta watu 8 kwenda naye mwezini

Sam Gidori

Senior Member
Sep 7, 2020
165
414
Hii ni bahati ya mtende kuota jangwani! Bilionea mmoja nchini Japan anatafuta watu 8 kutoka kote duniani watakaomsindikiza kwenda mwezini mwaka 2023 katika safari ya kibinafsi.

Bilionea huyo, Yusaku Maezawa mwenye umri wa miaka 45 aliyejipatia utajiri wake kupitia fasheni mtandaoni, alitangazwa mwaka 2018 kuwa mtu wa kwanza kushika nafasi katika chombo cha anga kinachotengenezwa na kampuni ya SpaceX.

Bilionea.jpg


Awali, Maezawa alikuwa amewaalika wasanii watano katika safari yake hiyo, ambayo kiasi cha pesa alicholipa kugharamia safari hakijawekwa wazi, lakini akaamua kuongeza wigo hadi kufikia watu wanane akisema anaamini kuwa mtu yeyote anayefanya jambo lolote la kibunifu anaweza kuitwa msanii.

Ameweka wazi vigezo viwili vya mtu yeyote kumwezesha mtu kupata nafasi ya kusafiri naye kwenda mwezini: kuwa mbunifu na kuweza kuwasaidia wasafiri wengine kuwa wabunifu. Hii ni kusema kuwa kigezo cha kusafiri na Maezawa ni kufanya jambo lolote la kibunifu!

Mwisho wa kutuma maombi ili kupata nafasi ya kwenda mwezini ni Machi 14, ambapo usaili wa awali unaweza kuanza Machi 21. Bilionea huyo hajatangaza muda wa kupitia hatua zingine, lakini hatua za mwisho kufikia vipimo vya afya kwa wale watakaofanikiwa itakuwa mwisho wa mwezi Mei, kwa mujibu wa tovuti yake.

Hii si mara ya kwanza kwa bilionea huyo kutangaza kutafuta watu wa kwenda naye mwezini. Maezawa aliwahi kugonga vichwa vya habari duniani kwa kutangaza kumtafuta 'mpenzi' wa kwenda naye mwezini ambapo zaidi ya wanawake 30,000 walivamia ofa hiyo kabla ya kusitisha utafutaji ghafla bila kutoa maelezo zaidi.

Maezawa anajulikana kwa kauli zake zenye utata na kupenda maisha ya anasa. Utajiri wake ulikadiriwa kufikia dola bilioni 1.9 (sawa na Tsh. 4,406,100,000,000) mwaka jana, hivyo kumfanya mmoja ya watu tajiri zaidi nchini Japan. Aliuza kampuni yake ya fasheni mtandaoni ya Zozo kwa Yahoo! Japan mwaka 2019.

Ikiwa chombo cha anga cha SpaceX kitafanikiwa kufika mwezini, Bilionea huyo anatarajiwa kuwa mtu wa kwanza katika karne ya 21 kufika mwezini, na hii ni baada ya safari ya mwisho ya chombo cha anga cha Marekani, Apollo mwaka 1972.

Jaribio la chombo cha anga cha SpaceX limeshindwa mara mbili, na mara ya mwisho chombo hicho kilianguka na kulipuka mwezi uliopita kikijaribu kutua kwa kusimama wima wakati wa majaribio. Lakini kampuni hiyo inaamini kuwa chombo chake kitafanikuwa kumpeleka mwanadamu mwezini, sayari ya Mars na kwingineko katika anga za juu, safari ya karibuni zaidi ikitarajiwa kufanyika mwaka 2023.
Safari hiyo inatarajiwa kuwa ya kwanza ya kibinafsi kumpeleka mwanadamu nje ya dunia.

Chanzo: Al Jazeera
 
Wenzetu wanapenda kujaribu yale wengine tunayaona ni impossible maishani na wakifanikiwa waafrika tunabaki kuwasoma tu hao jamaa kwenye vitabu na kwenye mitandao.
 
Chombo tupu bila binadamu ndani kime feli na kulipuka, je hicho kitakachobeba binadamu itakuwaje.wazungu bana wakisha collect money at excess Basi huanza vituko na mbwembwe.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom