Bilionea Laizer asimzoee sana Millard Ayo na waandishi, akumbuke ya Askofu alipoishia na mabilioni

Huyu mmasai hili bilioni 8 haitachukua raundi unajua hela ina watu wake. Hela sio ngo'ombe ina akili zaidi ya ng'ombe.

Futa mawazo haya!

Baada ya kusikia taarifa zake ni kwamba huyu jamaa ni tajiri siku nyingi tu, kama alishaanza kujenga MALL yenye makadirio ya Bilioni 6 tangu 2017 hebu fikiria vizuri.

Amewekeza pesa nyingi mno hadi kufika hapo, na hata huo mgodi anaendesha kwa pesa nyingi tu... kwahiyo hizi 7.8 ni mstuko kwetu ila sio kwake hata kama hajawahi kuzishika kwa mkupuo.

Binafsi hata simjui, nami nimesikia tu!
 
Msichojua ni kuwa production yote inaweza kufanywa kwa siku moja,halafu anaachia vipande wiki nzima
Kingine huyo.Ayo nae ni mmasai,inawezekana na ujamaa na ndio mana aliweza kuwa wa kwanza kufanya exclusive interviewa
Ayo ni mmeru, ila wamasai na wameru ni majirani na kuna baadhi ya mila zao zinafanana.
 
Mwacheni dogo achukue hela kungali mapema, hili laizer akija kushituka basi wawe wamempiga vya kutosha.

Ila unaweza kujiuliza ni story gani kila siku waandishi wanajazana kule mirerani?
Jana wameenda kula nyama kwenye sherehe aliyoandaa laizer kwa ndugu, jamaa na marafiki zake.
 
Ayo naye amezidi sasa habari za nyumba za wake wa bilonea sio inshu kwetu aende basi pale muhimbili aulizie kinachoendelea kati ya wale majeruhi 30 waliosalia ktk ajali ya lorry la mafuta morogoro
 
naona kama ushamba fulani hivi. kama nimepiga hela sasa waandishi wanahusikaje. kwani hii biashara?
watu wanaacha kutangaza mambo ya msingi unafuatilia wake za watu
 
YAAN ANAONESHA NJAA ZA WAZI UKIFUNGUA KUPATA HABARI MPAKA LEOHII N LAISER KACHINJA NGOMBE ULITAKA ACHINKE WAKEZAKE??KILA ANACHOFANYA LAISER MTAKIONA HOPE SIKU TUTAONA KITANDA CHAKE ANACHOLALIA
Ni Mbabaikaji fulani kwnza watu wa mawe hawapendi promo hizo eti anamuliza Vp mzee utanunua hammer???
Kijamaa kinaboa sana ki front front sana

Ova
 
Jamani si nae yupo Kazini Kwake au? Huwa simkubali kivile Milard Ayo kutokana na Nyeti moja Kumhusu Yeye, ila kwa hili naona mnamuonea tu.
Mkuu itoe hiyo nyepesi nyepesi ya Millard ayo ilikuwa vipi
 
Hii ni ushauri kwa aliye karibu na bilionea mpya, Laizer wa Arusha.

Aogope sana maana waandishi wa habari watampamba, watamfurahia mpaka mwisho akiwapa vijisenti wakimtangaza.

Siku akiishiwa huanika kila kitu na kubakia haamini kama ni wale waliokula naye nyama za ng'ombe na kutapakaa.

Namwona kila mara wapo wote, hope wamehamia Arusha kabisa. Kila ukiamka kuangalia taarifa unakutana na mara mke wake, mara mtoto wa Laizer mara nyumba za wake zake.

Nimkumbushe alikuwepo bwana anaitwa Askofu ambaye alinunua hoteli hapo Arusha na timu ya mpira na ni Muarusha.

Ndugu wa karibu fuatilia kilichomtokea mpaka sasa, yupo kama yupo.

Fuatilia yale masheli yake kila kona yaliishia wapi, now wako wanamiliki vijana wadogo.

Waangalie sana waandishi mkuu bilionea, wasikuzoee sana kama familia yako.

Nawatakia la kheri.
Kumbe ule mzigo sio wake peke yake nasikia kuna mchimbaji mwenzake watagawana
 
Back
Top Bottom