Bilawal Butto kusimikwa rasmi kesho kuwa mwenyekiti wa PPP | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bilawal Butto kusimikwa rasmi kesho kuwa mwenyekiti wa PPP

Discussion in 'International Forum' started by Richard, Aug 7, 2010.

 1. Richard

  Richard JF-Expert Member

  #1
  Aug 7, 2010
  Joined: Oct 23, 2006
  Messages: 8,253
  Likes Received: 4,276
  Trophy Points: 280
  Kesho jumamosi ni siku ambayo mtoto wa kwanza wa kiume wa Waziri mkuu wa zamani wa Pakistan marehemu Benazir Butto bwana Bilawal Butto anasimikwa rasmi kuwa mwenyekiti wa chama cha Pakistan People's Party katika sherehe itakayofanyika mjini Birmingham nchini Uingereza.

  Sherehe hio ambayo imeandaliwa sambamba na ziara ya baba yake Bilawal Asif Ali Zardari, waziri mkuu wa sasa wa Pakistan ambae hivi sasa yupo Uingereza kikazi imekuwa ikipingwa sana na wananchi wenye asili ya Pakistani waishio Uingereza ikizingatiwa kwamba hivi sasa nchi hio imekumbwa na madhara makubwa ya mafuriko ambayo yamesababishwa na mvua kubwa ziitwazo "Monsoon" zinazoendelea kunyesha hadi wakti huu.

  Marehemu Butto alipofariki aliacha chama cha PPP alichokianzisha mwenyewe nchini Uingereza alipokuwa akisoma chuoni Oxford, na bwana Bilawal akawa ni mrithi anaefuata lakini kwa wakti ule kwakuwa alikuwa na miaka 19 tu na alikuwa bado masomoni katika chuo kikuu cha Oxford, chama kikakabidhiwa kwa baba yake bwana Zardari kuwa mlezi kwa miaka miwili hadi hapo bwana Bilawal Butto atakapomaliza masomo.

  [​IMG]
  Bilawal Bhutto

  Sasa Bwana Bilawal Butto amemaliza masomo yake ya sheria na ana miaka 22 na atasimikwa rasmi kuchukua majukumu yote ya uendeshaji wa chama hicho ambacho kimekuwa kikionekana kama ni cha familia na ukoo mzima wa jina la Butto.

  Akizungumza wakti wa msiba wa mama yake bwana mdogo Bilawal Butto alisema kwa kiingereza kwamba, "My mother always said: democracy is the best revenge." akimaanisha kwamba mama yake alisema siku zote kuwa demokrasia ni kulipiza kisasi.
   
 2. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #2
  Aug 7, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Mbona mdogo sana ata ubwabwa wa shingo haujamtoka huyu atakwenda kufa bure tu...akumbuke na Rajiv Ghandhi naye aliacha usukani wa ndege kwenda kuongoza chama cha marehemu mama yake Bi Indira Gandhi, aliyeuwawa kama bibi Butho....na yaliyomkuta Rajiv naye akauwawa na Watamil....mjane wake mama Sonia Gandhi...aliposhika madaraka ya chama na kukiongoza kwenye ushindi alikataa kupewa uwaziri mkuu kwa sababu alizozijuwa yeye lakini wataalamu wakatwambia kuondoa 'nuksi' ya ukoo...so Bw. Bilawal Bhuto becareful...!
   
Loading...