Bilal Rehani Waikela ni nani?

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
16,185
2,000
MZEE BILAL REHANI WAIKELA AMELAZWA MOI GOROFA YA 2 CHUMBA NO 2 KITANDA NO. 5

Ndugu zangu leo asubuhi nimejaaliwa kwenda MOI kumjulia hali Mzee Waikela.

Nimemkuta macho na namshukuru Allah kwa hili kwani ningemkuta kalala nisingethubutu kumwamsha ingebidi niondoke.

Mzee wetu amepokelewa jana hapo hospitali akitokea Tabora.
Mzee Waikela ameanza kupata matibabu.

Mzee Waikela ana historia isiyo na mfano kwanza katika kuuendeleza mbele Uislam na pili katika kuunda chama cha TANU Western Province na kupigania uhuru wa Tanganyika bega kwa bega na Julius Nyerere na wazalendo wengine.

Mzee Waikela ni katika wazalendo wachache sana ambao wana historia ya kutukuka katika harakati za Uislam na katika kupigania uhuru wa Tanganyika.

Mzee Waikela alikuwa kiongozi ndani ya East African Muslim Welfare Society (EAMWS) na alikuwa pia mstari wa mbele katika TANU.

Hivi sasa Mzee Waikela ni katika wanachama waasisi wa TANU wachache sana walio hai.
Na kwa hakika wazalendo hawa wanahesabika katika kiganja cha mkono.

Ndugu zangu katika kipindi hiki cha maradhi ya mzee wetu huyu tunahitaji tuwe pamoja katika kumsaidia kwa kila hali na kumuombea dua.

Screenshot_20220114-165621_Phoenix.jpg
 
May Day

JF-Expert Member
May 18, 2018
4,976
2,000
Mungu amfanyie wepesi Mzee wetu Waikela.

Nimepata muda wa kumsoma na kupitia habari za Mzee Waikela nikagundua kuna makubwa ya kujifunza kutoka kwake.

Mara kadhaa nimewahi kumtaja kwenye nyuzi mbali mbali, ni kati ya Watu waliokuwa na misimamo isiyoyumbishwa...haswa kama suala lilihusu Dini yake.

Nina imani Historia ya Nchi haitamuweka kando.
 
Sesten Zakazaka

JF-Expert Member
Sep 10, 2017
10,493
2,000
Mungu Ampe afya, amponye maradhi na aweze kurejea katika hali yake ya kawaida Mzee Rehani Waikela

Hili jina la Rehani hutumiwa sana na Wanyamwezi na Wamanyema. Hawa Wamanyema asili yao ni Kigoma na pia Congo lakini Tabora pia kuna Wamanyema Wanyamwezi!

Wamanyema hasa wale wa zamani ni Waswahili halisi kwa maana ya utamaduni mila na desturi. Ni watu faswaha sana wa lugha ya kiswahili na ni watu wa staha

Sheikh Mohamed, hivi kumbe gazeti la An-nuur bado lipo? Linapatikana wapi? Maana kwenye meza za kuuzia magazeti hulikuti!
 
Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
16,185
2,000
Mungu Amoe afya, amponye maradhi na aweze kurejea katika hali yake ya kawaida Mzee Rehani Waikela

Hili jina la Rehani hutumiwa sana na Wanyamwezi na Wamanyema. Hawa Wamanyema asili yao ni Kigoma na pia Congo lakini Tabora pia kuna Wamanyema Wanyamwezi!

Wamanyema hasa wale wa zamani ni Waswahili halisi kwa maana ya utamaduni mila na desturi. Ni watu faswaha sana wa lugha ya kiswahili na ni watu wa staha

Sheikh Mohamed, hivi kumbe gazeti la An-nuur bado lipo? Linapatikana wapi? Maana kwenye meza za kuuzia magazeti hulikuti!
Ses ...
Liko online.
 
Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
40,518
2,000
MZEE BILAL REHANI WAIKELA AMELAZWA MOI GOROFA YA 2 CHUMBA NO 2 KITANDA NO. 5

Ndugu zangu leo asubuhi nimejaaliwa kwenda MOI kumjulia hali Mzee Waikela.

Nimemkuta macho na namshukuru Allah kwa hili kwani ningemkuta kalala nisingethubutu kumwamsha ingebidi niondoke.

Mzee wetu amepokelewa jana hapo hospitali akitokea Tabora.
Mzee Waikela ameanza kupata matibabu.

Mzee Waikela ana historia isiyo na mfano kwanza katika kuuendeleza mbele Uislam na pili katika kuunda chama cha TANU Western Province na kupigania uhuru wa Tanganyika bega kwa bega na Julius Nyerere na wazalendo wengine.

Mzee Waikela ni katika wazalendo wachache sana ambao wana historia ya kutukuka katika harakati za Uislam na katika kupigania uhuru wa Tanganyika.

Mzee Waikela alikuwa kiongozi ndani ya East African Muslim Welfare Society (EAMWS) na alikuwa pia mstari wa mbele katika TANU.

Hivi sasa Mzee Waikela ni katika wanachama waasisi wa TANU wachache sana walio hai.
Na kwa hakika wazalendo hawa wanahesabika katika kiganja cha mkono.

Ndugu zangu katika kipindi hiki cha maradhi ya mzee wetu huyu tunahitaji tuwe pamoja katika kumsaidia kwa kila hali na kumuombea dua.

View attachment 2081534
Asante kwa hii, imesaidia sana, hadi CCM wamekumbuka na kwenda kumtembelea.
I wish him, to get well soon.
P
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom