Bila ya uvamizi wa Oman, Zanzibar ingekuwa wapi?

Baraghash

JF-Expert Member
Dec 18, 2012
2,713
1,789
Tunasikia lugha za kifidhuli na za kukebehi mwaliko wa Oman ndugu zetu wa kiroho kutusaidia kuwaondoa na kuuzika utawala wa kibeberu wa Kireno Zanzibar uliodumu karne kwa karne.

Tuliiushuhudia utawala wa kisultani ulivyoinyanyua Zanzibar na watu wake.

1. wakati wa vita vya dunia wazanzibari waliojiunga na jeshi laUingereza walikuwa wanapata " special treatment" na hata a chakula walikuwa wanapewa tofauti na watu wa makoloni yake.
2. Uchumi wa Zanzibar ulipanda na ulikuwa nchi ya pili barani Afrika baada ya Ghana
3. Nchi ya kwanza Afrika ya mashariki kuwana nuumba ya ghorofa na "lift".
4.Zanzibar imekuwa na taa za mitaaani kabla hata ya mji wa London
5 kumiliki usafiri wa majini mambo kadhaa wa kadhaa

Wakati wa utawala wa kishenzi wa kireno, wazee wetu waliambulia ibada ya kulazimishwa kwa nguvu ya kikafiri tu!

Lakini kubwa wazanzibari wanajiuliza kama angebaki chini ya mreno leo tungekuwa wapi? koloni la Tanganyika hadi kufikia kuchaguliwa watawala? au Zanzibar leo ingelikuwa kama Cape Verde?

Ami Sheikh Thabit Kombo tutaendea kukukumbuka daima na Allah azidi kukurehemu, lakini hatukusamehe kamwe kuiuza Shirazi Party yetu kwa wakatamaji.
 
Karume. -Malawi
Mwinyi -Mkuranga
Shein Pangani
Jecha -Tabora
Vuai -Mombasa
Seif Idd. -Ushirombo
Wacha uwongo huo.. Sheni ni Pemba fyoko kabisa hana hata asili ya tanga.. kwa sababu ni CCM na amekuwa raisi na huko nyuma mlikuwa mnasema watu wa unguja(CCM) wanakubagueni na ndiyo maana hampewi raisi kutoka Pemba baada ya shein kuchaguliwa bila ya aibu mkaanzisha propaganda ya kuwa si mpemba... Vuai kwao si Mombasa bali ni mtu wa Urowa(wilaya ya kati unguja)..Jecha si kwao tabora bali yeye ni mtumbatu kutoka KIBENI wilaya ya ya kaskazini A unguja na Seif Ali iddi ni mtu wa Donge wilaya ya Kaskazini B Unguja. Cha kushangaza mtu anatoka Pemba leo anakuja Unguja anamkaribisha na mkizozana kidogo kwenye siasa anakumbia wewe Zanzibar siyo kwenu.. Na hicho ndiyo kinachowaponza ndugu zangu wa kipemba wanahisi wao wana haki Zaidi unguja kuliko yuko Muunguja ambao wazazi wake wapo for generation.
Tuje kuhusu waomani watu wanasema wameenda kuitwa kuja kuiokoa Zanzibar kutoka kwa wareno lakini historia haionyrshi kitu hicho kama kimetokea. Mimi sifikirii kama walikuja kuwaokoa watu wa Zanzibar kwani walipofika tu baada ya miaka michache wameshapora Zaidi ya 80 ya ardhi yote imekuwa yao na wakawaacha wale wenyeji walio wakuta kuwa watumwa katika nchi yao wenyewe.na sifikii kama leo kuna mzanzibar amabae ana miss utawala wa mu oman Zanzibar pengine utakuwa wewe na wenzako wachache.kwani bora tufe njaa lakini tuko huru kutiko biryani(leftover) lakini watumwa.
 
msumbiji na Angola zote zimetawaliwa na ureno na makoloni mengi yaliyotawaliwa na ureno yaliendelea kwani Mreno aliamini atatawala milelendio maana akawekeza sana hao waoman wasingekuja zanzibar ingekuwa nchi nzuri zaidi kwani tusingeshuhudia ubaguzi unaotokea sasa hivi
 
Nijuavyo mm mkoloni aliebaki zanzibar mpaka sasa ni mkoloni mweusi,nae akipenda asipende ataondoka kama walivyoondoka wakoloni wenzake ni swala la muda tu,kwetu sisi wazanzibar ukoloni hauna rangi.
 
Tunasikia lugha za kifidhuli na za kukebehi mwaliko wa Oman ndugu zetu wa kiroho kutusaidia kuwaondoa na kuuzika utawala wa kibeberu wa Kireno Zanzibar uliodumu karne kwa karne.

Tuliiushuhudia utawala wa kisultani ulivyoinyanyua Zanzibar na watu wake.

1. wakati wa vita vya dunia wazanzibari waliojiunga na jeshi laUingereza walikuwa wanapata " special treatment" na hata a chakula walikuwa wanapewa tofauti na watu wa makoloni yake.
2. Uchumi wa Zanzibar ulipanda na ulikuwa nchi ya pili barani Afrika baada ya Ghana
3. Nchi ya kwanza Afrika ya mashariki kuwana nuumba ya ghorofa na "lift".
4.Zanzibar imekuwa na taa za mitaaani kabla hata ya mji wa London
5 kumiliki usafiri wa majini mambo kadhaa wa kadhaa

Wakati wa utawala wa kishenzi wa kireno, wazee wetu waliambulia ibada ya kulazimishwa kwa nguvu ya kikafiri tu!

Lakini kubwa wazanzibari wanajiuliza kama angebaki chini ya mreno leo tungekuwa wapi? koloni la Tanganyika hadi kufikia kuchaguliwa watawala? au Zanzibar leo ingelikuwa kama Cape Verde?

Ami Sheikh Thabit Kombo tutaendea kukukumbuka daima na Allah azidi kukurehemu, lakini hatukusamehe kamwe kuiuza Shirazi Party yetu kwa wakatamaji.
Akili fupi ni chanzo cha maafa!! Msaada kwa kupewa samaki si msaada bali wa kufundishwa namna ya kupata samaki hao ndo msaada. Afurahiaye kupewa gari hali hajui namna ya kulitumia na kulifanyia huduma kiasi cha kumwezesha kupata jingine ni mgonjwa. Pole sana ndugu yangu kwa fikra yako. Nakualika kufanya tafakari na tafakuri yakinifu .....!!
 
Mm wote nakubali ila seif iddi kuniambia mzanzibar ckubali kasaa na kuhusu kutawaliwa bora kutawaliwa na mreno au mwarabu kuliko kutawaliwa na mkoloni mweusi (ccm) kutawaliwa na ccm ni sawa na kula kinyesi cha nguruwe
 
Hizbu wameiharibu zenji tunataka Machotara warudi, Na Tanganyika ipatikane
Uchotara una tuhusu nini sisi!! Cha msingi ni binadamu basi. Rangi, kabila, dini, itikadi, ukwasi, umaskini, ujinga n.k ni manjonjo tu. Ni ukweli usiopingika kuwa, mtoto akizaliwa mahali Fulani kwa mfano akazaliwa Moshi nchini Tanzania na akahamishiwa maeneo ya Uheheni huko Iringa Tanzanania angali na umri wa mwezi mmoja, akakulia huko na kuzeekea Iringa bila shaka kama hataambiwa hatajijua kama alizaliwa Moshi. Kwa mantiki hiyo atakua katika mazingira ya kihehe akifuata mila na desturi za kihehe. Ni mtu mzima anayeweza kumwingizia mambo ya ukabila kwa kumsimulia kuwa yeye siye Mhehe. Ubaguzi wa kikabila, rangi, itikadi, dini n.k ni matokeo ya fikra mbovu na potofu ya mwanadamu. Historia ni mwalimu mwema. Ni historia inayotuonesha tumetoka wapi, tuko wapi na tunaelekea wapi. Ni historia pia inayotuambia kwamba binadamu chanzo chetu ni kimoja tu. Yule aliyemwumba mwanadamu ni Mmoja tu wala hakuna mwingine. Hili linasindikizwa pia na Imani ya dini mbalimbali. Kila dini hukiri kuwa Mwumbaji ni mmoja tu. Kumbe ni kama familiya mmoja ya baba mmoja na mama mmoja akiwa na watoto wengi wengine wembamba, wengine wanene, wanjano, wekundu, weusi, weupe, wafupi, warefu, n.k lakini wote hawa ni zao la familiya moja. Ikitokea mmoja wapo anawona wengine kama wageni hivi ama hawafai kuwapo hapo basi ujue huyo namna yake ya kufikiri si sawa. Kumwambia mtoto ama ndugu yake hafai kuwepo hapa ndio huitwa UBAGUZI. Kwa hiyo ndugu yangu, angalia sana. Ni muhimu kuepuka makosa waliyoyatenda ndugu zetu siku zilizopita kutokana ama na ujinga, ama ugonjwa hadi kufikia hali ya kunyonya, kuiba, kuua, n.k wakijisahu kuwa wanaowafanyia ni ndugu zao. LENGA MBALI. KISASI SI TIJA
 
Mi.i namsubiri donald trump achagiwe .washirazi asilili yao sio afrika ni iran .someni historia na mji mkuu wa kwanza wa washirazi ulikua ni tumbatu .na baadae mji mkuuvukawa unguja ukuu kabla wareno haqajauvamia na kuuharibu .waomani waliombwa na washirazi waje wasaidie kuwaondoa wareno na kweli walikuja na kuwaondoa .ni fitna zililetwa kutoka bara za kuwagawa washirazi na waarabu .lakini wote walikua wanatawaliwa na sultani .na muengereza wote walikua maskini
 
Kasome vizuri historia.. hivyo ndiyo ulivyomezeshwa?.....Ujinga mbaya sana[/QUOTnibauhakika wewe ni BiG G au samaki .kwenye post yangu sijatukana wala kumuita yeyote mjinga .wewe umedandia humu jf .unatafunwa nn wewe?
 
"Naanza kueelewa kwa nini vijana wa CCM walibeba mabango dhidi ya ........ ", Nimeani ni kweli Waoman walipanga Mapinduzi Zanzibar, Zanzibar si sehemu ya Oman, Tatizo nini Oman?, Zanzibar imekuwa nchi ya Amani miaka yote, Tanzania imekuwa nchi ya mbali zote kwa miaka yote hiyo kwa nini leo tufitinishe?, Tanzania hawezi kuchezewa kama Yemen, ONYO KWA WATU WENYE MLENGO WAKO, ONYO NA OLE WAKO.
 
Back
Top Bottom