Bila ya ukombozi wa kifikra na mtazamo watanzania hatuwezi kutoka hapa tulipo

JERRY

JF-Expert Member
Feb 18, 2009
630
502
Juzi juzi nilikuwa nchi za wenzetu walioendelea jambo moja nililolifurahia ni hulka ya wenzetu huko katika kujali mambo yao,Kama ni wakati wa kazi huwezi kuta watu wanachati sijui na wassaup au wako facebook au wanachezea simu,yani ni kazi tu.

Wanajali miundombinu yao YAANI BARABARA zao nzuri ajabu njia 12 na kuna guard rails kwa pembeni kila mahali kama ingekuwa kwetu watu wangeshatoa hizo guard rails kwenda kuuza skrepa, SI TUMEONA PALE MANZESE DARAJANI JINSI WATU WALIVOIBA VYUMA VYA PEMBENI MWA BARABARA( GUARD RAILS) ILI KUUZA SKREPA.Huezi kuta uchafu hata kidogo mabarabarani, lakini hapa kwetu mtu akinunua maji kamaliza anatupa chupa ovyo, kanunua muhindi kala kamaliza anajitupia barabarani ovyo, yaani kila kitu ni kujifanyia bila kujali.

wakati fulani wakati wa uzinduzi wa uwanja wa Taifa ule mpya nilikuwepo pale uwanjani wakati wa half time nikaamua kupitapita hapa na pale ili niweze kuuagalia vizuri uwanja huo mpya katika pitapita yangu nikaamua kuingia toilet nilichokiona moyo wangu ulisononeka sana yaani watu baada ya kukojoa kwenye sehemu zilizojengwa maalum kwa huduma hiyo(urinals) wao wamekojolea kwenye masinki ya kunawia(wash basins) mpaka kumejaa juu na fun enough sio sinki moja ni yote nikawa najiuliza hivi watz. tukoje nikakosa majibu.HEBU fikiria mtu anaiba mafuta ya Transforma?au nyaya za umeme? ua utakuta mtu amepakia nondo kwenye pickup halafu anaburuza kwenye lami?

TUNAHITAJI UKOMBOZI WA KIFIKRA ILI MAENDELEO YAJE, VINGINEVYO HATA HAYO MAENDELEO TUNAYOAHIDIWA SASA YAKIPATIKANA WATU WATAYAHUJUMU
 
Je uliona kamera ngapi ? Ulikopita na unafkri hizo kamera zinafanyakazi gani ? .bila kuondoa ccm hayo unayosema ni ndoto
 
Je uliona kamera ngapi Ulikopita na unafkri hizo kamera zinafanyakazi gani ? .bila kuondoa ccm hayo unayosema ni ndoto
 
Back
Top Bottom