Bila ya Muungano leo hii Zanzibar wangekuwa wanachapana!

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,782
Hili halina ubishi kinachofanya mpaka leo hii kuwe na amani visiwani Unguja na Pemba hata kuweza kuishi pamoja ni uwepo wa Serikali ya Muungano, laiti kama Muungano usingekuwepo Unguja na Pemba wangeshafarakana zamani sana na wangefanyiana umafia wa kufukuzana, Waunguja wangefukuzwa Pemba na vivyo hivyo Wapemba wangefukuzwa Unguja na hii isingeishia hapo ingekuja kugeuka uhasama na vita kubwa kati ya watu wanaojiita Waarabu/Machotara na Waafrika weusi, na maafa ya kama Rwanda na Burundi yangetokea yaani ethnic Cleansing na Waarabu ndiyo wangemalizwa hapa kwa maana wako wachache!

Hivyo semeni yoote na kejelini mnavyotaka lkn uwepo wa Serikali ya Muungano ndiyo sababu ya Unguja na Pemba kuwa intact, na siku mikithubutu kujimegua huwo ndiyo mwisho wenu kwani sioni ni jinsi gani Unguja na Pemba chini ya Maalim Seif wanaweza kuishi pamoja na kuunda Serikali ya pamoja, silioni hilo!

Ikumbukwe Historia ya hivi visiwa viwili siku zote kulikuwa na chombo cha kati kati kilichowaweka pmja kulikuwa na Sultani, akaja Mzungu (Mjerumani na Mwingereza kwa nyakati mbalimbali) na mwishowe tukaja sisi Waafrika wenyewe hivyo leo hii ukiondoa Serikali ya Muungano ombwe kubwa litabakia na kutakuwa hakuna tena Zanzibar bali kuna Unguja na Pemba na hilo halitatokea kwa Amani na utulivu bila ya kuacha makovu ya kudumu!

Kuna sababu kwa nini Raisi Magufuli alisema kwamba yeye kazi yake ni kuhakikisha Usalama Visiwani humo, na kwamba yuko tayari kama Amiri Jeshi Mkuu kuhahakisha Usalama unaishi huko!
 
Kwa mantiki yako tuungane na Burundi wasiuuwane?
Vipi Rwanda mbona Kuna amani,Zanzibar wanaweza kukaa kwa amani demokrasia ikiachiwa huru
 
Umeongea ukweli mtupu na siku zote msema ukweli anao maadui wengi kuliko mwongo. Kinachowaweka pamoja na ile hali ya wao kuwa chini ya Tanzania. Wao kwa wao wana vinyongo vingi, wana makovu mengi sana. Mfano ni kile kilichojionyesha wakati wa bunge maalum la katiba, jinsi walivyokuwa wanatukanana na kugeuka vioja kwa wajumbe kutoka Tanzania Bara.
Binadamu anapoishi na mwenzake kitu muhimu ni ule uwezo wa kuvumilia udhaifu wa mwenzake. Sisi tunawavumilia wazanzibari na wao wanatuvumilia sisi. Ni sawa sawa na uhusiano wa mme na mke nyumbani, kila mmoja ni lazima ajishushe kwa faida ya ustawi wa maisha marefu ya ndoa.
 
Kwa mantiki yako tuungane na Burundi wasiuuwane?
Vipi Rwanda mbona Kuna amani,Zanzibar wanaweza kukaa kwa amani demokrasia ikiachiwa huru

Rwanda kuna amani amekwambia nani? Rwanda kuna utulivu tu kwa sasa, lkn uwezekano wa kulipuka muda wowote ule upo, lkn Rwanda na Burundi hazituhusu ila Unguja na Pemba zinatuhusu ni ndugu zetu wa Damu wakazi wengi wa Unguja na Pemba ni Wahamiaji ktk Tabora, Kigoma, Kilwa, Lindi, Tanga, Bagamoyo n.k hivyo usalama wao unatuhusu moja kwa moja!

Acheni kulishwa maneno Wazungu tangu wamewafundisha neno demokrasia basi mnafikiri ni suluhisho la kila kitu wkt Wazungu wenyewe hao hao wanaweka limit ya hiyo hiyo demokrasia kwa mfano Mohamed Morsi ambaye Chama chake cha Muslim Brotherhood kilishinda Uchaguzi wa Kidemokrasia huko Misri na kuondoa utawala ya Kijeshi lkn Wazungu hawakumpenda Mohamedi Mursi na Chama chake ingawaje alichaguliwa kidemokrasia na kilichotokea Jeshi la Misri chini uangalizi wa Marekani, NATO na Israel wakampindua na leo hii yuko jela anasubiri go ahead ya Obama ili anyongwe, sasa kosa lake ni lipi Mohamed Mursi mpaka ahukumiwe kunyongwa wakati alishinda kwenye uchaguzi?

Mbona Umoja wa Mataifa uko kimya? mbona ICC haiendi kukamata Wanajeshi waliompindua? Mbona Wazungu wenu hawajawawekea vikwazo vya Kiuchumi Jeshi lililopindua nchi kwanza ndiyo wanawaongezea misaada?

Hivyo acheni kukaririshwa na Wazungu sijui upuuzi wa demokrasia, hakuna kitu kama hicho Dunia hii, mwenye nguvu ndiyo anaamua na swala la Zanzibar Serikali ya Muungano ndiyo ina nguvu na ndiyo inapaswa ihakikis
he Unguja na Pemba inabakia intact!
 
Barbarosa said:
...Hivyo acheni kukaririshwa na Wazungu sijui upuuzi wa demokrasia, hakuna kitu kama hicho Dunia hii, mwenye nguvu ndiyo anaamua na swala la Zanzibar Serikali ya Muungano ndiyo ina nguvu na ndiyo inapaswa ihakikishe Unguja na Pemba inabakia intact!
Huo ni UKABURU na mara zote huwa una MWISHO. Makaburu wa SA walikuwa na nguvu sana ukilinganisha na Serikali ya Muungano wa Tanzania, lakini ilifika mahali nguvu ya wenye haki ikatawala. Kinachosumbua Zanzibar ni UBAGUZI unaofanywa na kundi dogo lenye kudhani wataongoza milele!
 
Hawa ikibidi ni kutengana nao
Kwamimi sioni nacho kipata kutoka Zanzibar
Wala sioni tatizo waki jibagua
Itafikia mahali uwe hivyo
 
Barbarosa unachekesha kweli. Mvutano wote huu unaotokea ni kwasababu ya Muungano. Kama usingelikuwepo Muungano basi Zanzibar ingelikuwa salama na ingelikuwa mbali leo. Mbona huko nyuma tukiishi salama? Kutofahamiana kumeanza ulivyokuja huu Muungano tu!
Hujaona wewe ulivyokuwa ukisoma shuleni (primary school) mtoto mwenye kaka anavyomchokoza kila mtu? Yote ni kwasababu anamtegemea kaka na kama kaka hayupo anakuwa na adabu zake.
Hata kama hivyo unavyoeleza wewe ni sawa, sasa tutakutegemeeni nyinyi kwa usalama wetu mpaka lini? Huoni hio ni hali ambayo ni temporary tu?
Wachina wanakuja na 60b Dollars, AfDB na 1.1b! Sisi tubakie kungojea crumbs kutoka kwenu? Yanamwisho haya!
 
!

Nisome vizuri nimelielezea hilo kwamba siku zote Zanzibar kumekuwa na mtu wa kati kati aliyewafanya waishi pamoja mwanzoni alikuwa Sultani, akaja Mzungu na sasa Muungano yaani kuna outside force ndiyo inayounganisha Unguja na Pemba leo hii Serikali ya Muungano ikitoka hilo ombwe litazibwa na nani?
Kwa kifupi kinachounganisha Unguja na Pemba kihistoria ni chombo kilicho kati kati yao (Neutral) yaani alikuwa Sultani, akaja Mzungu na sasa Serikali ya Muungano wao kama wao hawajahi kuishi pmj na wakiachwa wenyewe wtachapana na kuanza kufukuzana tu na hatimaye ethnic cleansing kama Rwanda kutokea!
Waingereza waliwaacha kidogo tu baada ya Uhuru kilichotokea unakijua Muungano ukaingia kuziba pengo la Waingereza hivyo Muungano ukivunjika na Serikali ya Muungano kukoma kuwepo hakutakalika yaliyotokea baada ya Muingereza kuondoka yatarudia tena na mwishowe kuanza kuchapana na kumalizana kabisa!!

Usisahau kwamba mabaki ya Sultani mpaka elo hii yanaishi uhamishoni Uingereza wakitegemea siku moja kurudi kutawala Zanzibar sasa unafikri Waunguja watakubali?
 
Rwanda kuna amani amekwambia nani? Rwanda kuna utulivu tu kwa sasa, lkn uwezekano wa kulipuka muda wowote ule upo, lkn Rwanda na Burundi hazituhusu ila Unguja na Pemba zinatuhusu ni ndugu zetu wa Damu wakazi wengi wa Unguja na Pemba ni Wahamiaji ktk Tabora, Kigoma, Kilwa, Lindi, Tanga, Bagamoyo n.k hivyo usalama wao unatuhusu moja kwa moja!

Acheni kulishwa maneno Wazungu tangu wamewafundisha neno demokrasia basi mnafikiri ni suluhisho la kila kitu wkt Wazungu wenyewe hao hao wanaweka limit ya hiyo hiyo demokrasia kwa mfano Mohamed Morsi ambaye Chama chake cha Muslim Brotherhood kilishinda Uchaguzi wa Kidemokrasia huko Misri na kuondoa utawala ya Kijeshi lkn Wazungu hawakumpenda Mohamedi Mursi na Chama chake ingawaje alichaguliwa kidemokrasia na kilichotokea Jeshi la Misri chini uangalizi wa Marekani, NATO na Israel wakampindua na leo hii yuko jela anasubiri go ahead ya Obama ili anyongwe, sasa kosa lake ni lipi Mohamed Mursi mpaka ahukumiwe kunyongwa wakati alishinda kwenye uchaguzi?

Mbona Umoja wa Matifa uko kimya? mbona ICC haiendi kukamata Wanajeshi waliompindua? Mbona Wazungu wenu hawajawawekea vikwazo vya Kiuchumi Jeshi lililopindua nchi kwanza ndiyo wanawaongezea misaada?

Hivyo acheni kukaririshwa na Wazungu sijui upuuzi wa demokrasia, hakuna kitu kama hicho Dunia hii, mwenye nguvu ndiyo anaamua na swala la Zanzibar Serikali ya Muungano ndiyo ina nguvu na ndiyo inapaswa ihakikis
he Unguja na Pemba inabakia intact!
....lkn pia, dunia, afrika na tanzania haiwezi fanya kosa kumwachia fidhuli wa haki uhuru na hadhi ya mtu mweusi atawale sbb ya demokrasia...Adolf Hitler na NAZI yake waliingia madarakani kidemokrasi pia...
 
mkuu nadhani ungefanya utafiti zaidi.
ungetambua migogoro ya zanzibar inaletwa na nani ?
waliojenga chuki Zanzibar kwamba machotara wa Kipemba ni vibaraka wa Oman ni nani ? hadi kufikia hatua ya kuwapindua..
Ninachoelewa maendeleo ya Zanzibar yamezidi kuporomoka kadiri mambo ya Muungano yalivyoongezwa..
zamani Bara walikua wanaenda Zanzibar kufunga mizigo.
sasahivi hela za utalii zaishia bara,foreign exchange bara,makusanyo ya bandari bara,mabilioni ya Zanzibar yaliyokuwepo EAC bank yamefia bara..
kamgao zanzibar wanakokapata kutoka bara hakilingani na mpunga wanaoupeleka huko.
kweli Tanganyika ndio wanaoshikilia amani ya visiwani..
hata mauwaji ya january 27 2001 kisiwani Pemba,amri ilitoka bara !
asante mkoloni mweusi.
 
Barbarosa unachekesha kweli. Mvutano wote huu unaotokea ni kwasababu ya Muungano. Kama usingelikuwepo Muungano basi Zanzibar ingelikuwa salama na ingelikuwa mbali leo. Mbona huko nyuma tukiishi salama? Kutofahamiana kumeanza ulivyokuja huu Muungano tu!
Hujaona wewe ulivyokuwa ukisoma shuleni (primary school) mtoto mwenye kaka anavyomchokoza kila mtu? Yote ni kwasababu anamtegemea kaka na kama kaka hayupo anakuwa na adabu zake.
Hata kama hivyo unavyoeleza wewe ni sawa, sasa tutakutegemeeni nyinyi kwa usalama wetu mpaka lini? Huoni hio ni hali ambayo ni temporary tu?
Wachina wanakuja na 60b Dollars, AfDB na 1.1b! Sisi tubakie kungojea crumbs kutoka kwenu? Yanamwisho haya!
...lkn kama muungano ni jambo baya na umewakwamisha, mbona bado nyie(Zanzibar), mko vizuri zaidi kwa hali zote kuwazidi Comoro ambao wako jirani na ufaransa(mayotte). ...comoro, wamepungukiwa nini kinachowafanya wazidiwe na Tanzania visiwani ?wamepungukiwa amani na utulivu? Mapungufu kiimani? Wamezidiwa (wacomoro)Unafiki na uzandiki wa viongozi wa kisiasa, na baadhi ya wanazuoni wao wanaoutumia uislam kwa maslahi ya kisiasa, au wamezidiwa na upuuzi wa harkati za kinasaba dhidi ya "uafrika wa kibara"....mbona wako nyuma sana na wakiwa hawajaungana na yeyote?
 
mkuu nadhani ungefanya utafiti zaidi.
ungetambua migogoro ya zanzibar inaletwa na nani ?
waliojenga chuki Zanzibar kwamba machotara wa Kipemba ni vibaraka wa Oman ni nani ? hadi kufikia hatua ya kuwapindua..
Ninachoelewa maendeleo ya Zanzibar yamezidi kuporomoka kadiri mambo ya Muungano yalivyoongezwa..
zamani Bara walikua wanaenda Zanzibar kufunga mizigo.
sasahivi hela za utalii zaishia bara,foreign exchange bara,makusanyo ya bandari bara,mabilioni ya Zanzibar yaliyokuwepo EAC bank yamefia bara..
kamgao zanzibar wanakokapata kutoka bara hakilingani na mpunga wanaoupeleka huko.
kweli Tanganyika ndio wanaoshikilia amani ya visiwani..hata
mauwaji ya january 27 2001 kisiwani Pemba,amri ilitoka bara !
asante mkoloni mweusi.
...lkn na fursa za biashara na kimaisha ambazo zimepatikana bara kwa wazanzibar..?..unafahamu kuwa wakenya wengi wenye uwezo wa kufanya biashara, kilimo, na hata kuajiriwa, wanakosa hizo fursa kwa sababu tu, siwatanzania....lkn jamaa wa asili ya zanzibar wanazipata sababu ni watanzania...mbona mna fikra muflis za kudharau kuti kavu mlilokalia ? , , ,
 
Rwanda kuna amani amekwambia nani? Rwanda kuna utulivu tu kwa sasa, lkn uwezekano wa kulipuka muda wowote ule upo, lkn Rwanda na Burundi hazituhusu ila Unguja na Pemba zinatuhusu ni ndugu zetu wa Damu wakazi wengi wa Unguja na Pemba ni Wahamiaji ktk Tabora, Kigoma, Kilwa, Lindi, Tanga, Bagamoyo n.k hivyo usalama wao unatuhusu moja kwa moja!

Acheni kulishwa maneno Wazungu tangu wamewafundisha neno demokrasia basi mnafikiri ni suluhisho la kila kitu wkt Wazungu wenyewe hao hao wanaweka limit ya hiyo hiyo demokrasia kwa mfano Mohamed Morsi ambaye Chama chake cha Muslim Brotherhood kilishinda Uchaguzi wa Kidemokrasia huko Misri na kuondoa utawala ya Kijeshi lkn Wazungu hawakumpenda Mohamedi Mursi na Chama chake ingawaje alichaguliwa kidemokrasia na kilichotokea Jeshi la Misri chini uangalizi wa Marekani, NATO na Israel wakampindua na leo hii yuko jela anasubiri go ahead ya Obama ili anyongwe, sasa kosa lake ni lipi Mohamed Mursi mpaka ahukumiwe kunyongwa wakati alishinda kwenye uchaguzi?

Mbona Umoja wa Mataifa uko kimya? mbona ICC haiendi kukamata Wanajeshi waliompindua? Mbona Wazungu wenu hawajawawekea vikwazo vya Kiuchumi Jeshi lililopindua nchi kwanza ndiyo wanawaongezea misaada?

Hivyo acheni kukaririshwa na Wazungu sijui upuuzi wa demokrasia, hakuna kitu kama hicho Dunia hii, mwenye nguvu ndiyo anaamua na swala la Zanzibar Serikali ya Muungano ndiyo ina nguvu na ndiyo inapaswa ihakikis
he Unguja na Pemba inabakia intact!
Hayo yote ni mapovu tuu
Ukweli ni kwamba Zanzibar ni nchi nyingine tofauti na Tanganyika na tunaikalia kwa mabavu
Kuwepo watu wenye asili ya Tanganyika ni hoja. ya hovyo kwani watu kama hao wapo Rwanda Uganda Congo na Malawi na hatuwaingilii mambo yao
Ama kwa hoja ya mwenye nguvu ndiye hutawala na hakuna unachokiita ujinga wa demokrasia KWA NINI MNAITISHA UCHAGUZI?
 
...lkn na fursa za biashara na kimaisha ambazo zimepatikana bara kwa wazanzibar..?..unafahamu kuwa wakenya wengi wenye uwezo wa kufanya biashara, kilimo, na hata kuajiriwa, wanakosa hizo fursa kwa sababu tu, siwatanzania....lkn jamaa wa asili ya zanzibar wanazipata sababu ni watanzania...mbona mna fikra muflis za kudharau kuti kavu mlilokalia ? , , ,
ni kweli mkuu..
fikiria pia Watanganyika waliopo Zanzibar wanaofaidika na fursa za kibiashara, ajira na uwekezaji..
hizi kasumba kwamba bara wanaisaidia zanzibar hazina nafasi..
waweke uhuru wa maoni, Watanganyika waamue wapendayo na wazanzibari waamue wapendayo..
cha kushangaza eti kwenye kura ya maoni ya katiba CCM walisema SUALA LA MUUNGANO LISIJADILIWE
 
..Muungano unatakiwa uwatendee haki wa-Znz wote.

..Maalim Seif ameshinda uchaguzi, hivyo serikali ya muungano inapaswa kuulinda ushindi huo.

..nguvu na mbinu zilizotumika kuhakikisha Shein anaongoza kwa amani zitumike kuhakikisha Maalim Seif naye anaongoza kwa amani huku visiwa vya Unguja na Pemba vikiwa pamoja.

..Tanganyika tunafanya makosa kuegemea upande wa ccm kuwakandamiza ndugu zao wa cuf. Matokeo yake tunakuwa sehemu ya tatizo, na siyo sehemu ya suluhisho.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom