Bila ya kuwa na roho ngumu kwa wanawake utakufa siku si zako

Darubini1

JF-Expert Member
Jul 27, 2017
393
429
Nirudi katika mada, in short nilijaliwa mtoto na huyu mke, na niliishi nae kwa raha na shida,
Ilifika wakati nikaona mambo japo yapo sawa lakini kwa jicho la pili mbeleni si kuzuri.
Nikatafuta plan B kama suluhisho la kudumu.

Bila kutarajia nilifanikisha mipango ya kupambana nje ya nchi. Nikiwa nje kwa muda mrefu
nilijitahidi kumweka karibu huyu kiumbe wangu na mtoto. na ilikuwa hivyo hadi pale nilipo sema natarajia kurudi mda mfupi kwa mapumziko. Kweli alifurahi (SANA).

Sasa siku ya safari ikawadia, akanijulisha tu kwamba yupo nyumbani kwa wazazi wake, ila nikifika atanipokea kwani ni jirani na airport then tutaelekea sote nyumbani. Cha kushangaza nilifika sikumkuta zaidi ya mdogo wangu, ambaye nilimkabithi mizigo atangulie nayo ili kumsubiri huyu kiumbe.

Alipofika tu nilimwona kabadilika kila idara ya mwili, kwa utani nikamuuliza kwani una mimba. alistuka
akacheka na kujibu ni mwili tu. katika maongezi wakati tupo maeneo ya kujidai niliyoya miss, alikuwa ni mtu wa wasiwasi kila muda. Nikaona si mahala rafiki inabidi kuondoka, moja kwa moja nyumbani.

Hapo ndo nilistaajaabu niliyoyasikia kutoka kwake, kwamba anaogopa anataka arudi kwao. why kimya..
Nilijiongeza na kumwambia wewe una mtoto mchanga si bure, kweli akanijibu ndio yupo nyumbani kwao. Daaah, kwanza nilimtazamaaa kama sekunde 20, kisha malaika wa huruma akanijia gafla kunizuia nisifanye jambo ovu.

Nilijikuta namjibu tu, kwamba si kosa lake ni kosa langu kukaa mbali ili kutengeneza maisha ya mtoto, chukua nauli ya taxt rudi nyumbani kwenu kaendelee na maisha uliyoyachagua.
Sababu ya ukaribu na mwanangu ktk mawasiliano sikutaka kujiwekea record mbovu. Nilimwacha ktk mazingira ya nafsi na kumfuta moyoni, ktk mazingira ya nje nilionekana kawaida nikiendelea na maisha tena bila mashaka ya roho nikiwa mwenyewe na ratiba zangu.

Nipo na amani kwa kuwa mpaka naondoka tena mwanangu hajaua kuwa nime muacha mama yake kwa nia njema kabisa, baadae labda atajua hilo. Inahitaji ujasiri wa kujitambua ni kitu gani uko nacho mkononi katika maisha yako, kisha jiulize maswali nini kitatokea endapo uta panic na kufanya balaa, na kipi kitaharibika nikimwacha aende zake kwa amani na mimi niendelee na lengo langu la awali.

Kwa uhalisia wazazi wake walikuwa hawanisomi vizuri, ama nitaongeleaje hilo jambo, pale nilipo kwenda kuwatembelea. Tuliongea ya hapa na pale mpaka naondoka sikugusia jambo lolote zaidi. Pia wanajua binti yao nime mwacha aendelee na maisha yake. Hapo kumbuka kale kachanga kapo na bibi yake kamepakatwa nakaona. Moyoni nasema tu kuwa hajaja duniani apate tabu Mungu amkuze aje aione dunia ilivyo.
Mwisho niliaga nikaondoka kwa amani.

MAISHA MENGINE YANAENDELEA KAMA KAWAIDA.
 
Last edited:
Mwanamke ni mzuri na mtamu kabla ya ndoa, baada ya ndoa na kuzaa, hapo ndipo makeke, na tabia nzuri au mbaya ya mwanamke zinapojitokeza, ukiwa na bahati, umepata ila kama ndio kama wengine wengi, lazima ile kwako tu, tujihadhari wanaume...:(:mad:
 
Pole sana mkuu, na hongera kwa ujasiri huo,
Rafiki angu ashawahi nifata niomba ushauri kama huu kaacha mke kijiji wana watoto wa3 watu wakatia mimba nkamwambia amwache tuu aoe mwingine akabisha kaondoka kwa lengo la kwenda kumdhuru jiran mtia mimba na mke wake,
Kafika anataka kuliazisha mama yake akamweka kikao na kumwambia "kama umetoka ndani ya tumbo langu usijaribu kumfanya chochote mke wako wala aliempa mimba ulitegemea ataishije miaka 2 yote kwani ni roboti? Na hakuna kumfukuza kama humtaki ondoka wewe hapa nyumbani"
Ikabidi awe mpole tuu, sasa hivi mke wake ana mimba ya huyo rafiki yangu maisha yanayoendelea.
 
Back
Top Bottom