Byendangwero
JF-Expert Member
- Oct 24, 2010
- 871
- 56
Tangu kuanza kwa bunge linaloendelea makinda amejitokeza wazi kwamba amepania kweli kweli kukwamisha wabunge wa CDM katika kutekeleza wajibu wao wa kuisimamia na kuikosoa serikali inapobidi. Katika njama zake hizo, Makinda anaonekana kusaidiwa na wabunge wa CCM na hata baadhi ya wabunge wa vyama vya upinzani ambao spika huyo huwapa upendeleo maalum wa kuzungumza na kutenda jinsi wapendavyo bila ya kuzingatia kanuni na maadili ya bunge. Kitu kinacho sababisha spika huyo kuonyesha jeuri hiyo, ni imani kwamba CDM haiwezi kumfanya chochote bungeni kwakuwa wabunge wa CCM kutokana na wingi wao watamrinda. Katika hali hiyo napendekeza spika huyo ashughulikiwe kwa nguvu ya umma; katika maandamano yanayotarajiwa kuendeshwa na CDM nchi nzima, njama hizo za Makinda ziwekwe wazi kwa umma, ili kote nchini walaani hizo hujuma zake.