Bila ya kurahisisha taratibu zetu za uhamiaji, ziara za Rais Samia nchi jirani zitakuwa ni kazi bure

Red Giant

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
15,658
20,885
Ni wazi kuwa ziara za Rais kwenye nchi jirani au kokote kule ni kuboresha mahusiano kati ya nchi hizo na Tanzania ili watanzania tufaidike. Sasa ili wananchi wafaidike wanatakiwa kwenda huko kiurahisi, lakini ajabu Tanzania taratibu za mtu kutoka nje ni ngumu sana. Kuna masuala mengi uhamiaji wanayo katika kutoa passport ambayo ni urasimu usio na ulazima. Urasimu uliowekwa na elites ili wao tu ndiyo waendelee kufaidika na fursa zilizopo huko nje.

Utaratibu wetu uliopo ni wa kizamani sana, na wakicommunist. Kwenye nchi za ukomunist ni elites tu ndiyo walikuwa na pendeleo la kutoka nje ya nchi. Ndiyo kisa cha kujenga ukuta wa Berlin, ndiyo sababu North Korea huwezi kutoka kirahisi. Hata hapa kwetu ipo hivyo, si rahisi kutoka nchi hii, hilo ni pendeleo la elites tu. Lakini kiukweli hadi muuza vitumbua ana haki ya kutoka bila vipingamizi.

Watu kutoka nje ya nchi kuna faida nyingi sana. Zinaleta pesa za kigeni, Remittances, kupata maarifa mapya, zinapunguza mzigo wa ukosefu wa ajira na mengine mengi. Katika nchi ya Nigeria, pesa zinazotumwa na raia waliopo nje ni za pili baada ya mafuta katika kuchangia GDP ya nchi hiyo.

Unafikiri kwanini serikali ya Mexico haiwazuii wahamiaji haramu kwenda Marekani, na tena inaencourage watu wahamie Marekani? Kuna faida kubwa sana kwa uchumi wa nchi.

Turahisishe utaratibu wa kuondoka nchini, Iwe rahisi kwa daktari, mwalimu, nesi, fundi gereji au mchoma mishikaki kuhamia DRC, Zambia, Kenya, South Africa, Angola nk. Ni si tu kuwarahisishia, bali pia washawishiwe na kusaidiwa kuhamia huko.

Kitu kingine, mipaka ya dunia inabadilika. Miongo kadhaa ijayo kunaweza kuwa na shirikisho la EA. Sasa siku linafika tutashangaa wakenya, wanyarwanda, na waganda wamejaa EA yote wakichukua fursa na sisi tukiwa tupotupo tu. Wenzetu wanachukua fursa huko Sauth Sudan wakati sisi tunaulizana barua za mualiko. Kuna juzi kati walikuja na utaratibu eti mtu aliye nje ya nchi apate barua ya muajiri huko anapoenda kurenew passport! Urasimu wa kizembe kabisa.

Maoni yangu, utaratibu wa kupata passport urahisishwe. Napendekeza.

1. Kigezo cha kupata passport kiwe ni mtu kuwa na number ya NIDA tu. Taarifa za NIDA zilichukuliwa kwa undani sana. Hata hao uhamiaji walihusika na wakatia sahihi zao kuwa mtu huyu ni mtanzania. Kigezo cha mtu kupata passport kiwe hicho tu.

2. Bei ya passport ipungue, napendekeza iwe 50,000. Au hata chini ikiwezekana.

Kwahiyo basi, mtu akiwa na kitambulisho /number ya NIDA na Tsh 50,000 upewe passport yake, ikiwezekana siku hiyohiyo.

Petro alimwambia Yesu.

"Bwana, waruhusu watu waende kwenye vijiji na mashamba ya karibu wakajitafutie chakula. Hapa tulipo ni nyika tupu."
 
Nasubiri ziara za ng'ambo. Anatakiwa kwenda Australia, Argentina, Sri Lanka, Newsland, New Papua Guine. Mtembea Bure si Mkaa bure. Unalionaje hili mleta mada?
 

Similar Discussions

34 Reactions
Reply
Back
Top Bottom