karv
JF-Expert Member
- Dec 26, 2019
- 1,799
- 3,221
Habari zenu wapendwa
Nidhamu ya mwanafunzi imeshuka kutokana na kufutwa kwa adhabu ya viboko shuleni.
Miaka ya nyuma mwanafunzi alikuwa na nidhamu ya hali ya juu. Mwanafunzi alikuwa anaheshimu mwalimu kama alivyo heshimu wazee wake. Alipokemewa na mwalimu akisikiliza kwa sauti.
Mwalimu alipomuhukumu mwanafunzi shuleni, mwanafunzi huyo alikiri na kukubali kosa lakini kwa sasa hali haipo ivyo.
Kwa sasa mwanafunzi alihukumiwa na mwalimu ataondoka kwa kilio hadi nyumbani na kutoa malalamiko kuwa amepigwa. Na mzazi au mlezi bila ya kuuliza ataenda mbio hadi kwa mwalimu na kuanza kubwata na kutoa lugha chafu na kutaka kupigana na mwalimu na wengine huenda mbali hadi kuwafanyia mambo ya kishirikina.
Uchache wa walimu shuleni na watoto kuzurura hovyo mtaani pia huchangia kupungua kwa nidhamu. Vile vile walimu kufanya biashara shuleni kuliko kufundisha darasani pia huchangia nidhamu kushuka.
Tunaomba serikali kupitia wizara husika itazame suala la utoro kwa wanafunzi na walimu kwa ujumla.
Ukiangalia kwa undani utaona wanafunzi wengi hasa wa sekondari hizi za kata huzurula sana mitaani ukiuliza watakujibu shuleni hakuna walimu.
Vile vile kuna suala la wanafunzi wa kike wa sekondari wanapanga uraiani. Hawa ni wepesi sana kupata mimba ukizingatia wengi hujihusisha na mapenzi na watu wanaoishi nao karibu pindi tu hali zao za kifedha zinapokuwa chini.
Na kwa kumalizia napongeza uwepo wa shule za sekondari za kata lakini shule hizo bila walimu ni kama nyumba bila mlango wala madirisha
Ahsante naomba kuwasilisha