Bila utayari wa CCM kwenye katiba mpya sio rahisi CHADEMA kufanikiwa harakati zao

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Mar 29, 2012
10,174
22,189
Bila utayari wa CCM kwenye katiba mpya sio rahisi CHADEMA kufanikiwa harakati zao.

Leo nimeona nifafanue hili suala la katiba mpya ili angalau wafuasi wa CHADEMA waelewe kwamba wanachofanya kwa sasa ni ndoto za mchana. Ni sawa na kupiga ngumi ukuta. Ni kweli kunahitajika marekebisho kwenye katiba iliyopo lakini mchakato wake utakuwa mrahisi endapo CCM watakuwa tayari kwa hilo.. twende nami hatua kwa hatua uone ugumu ulipo kwenye kufanikiwa hizi harakati za chama cha Mbowe.

Wanachofanya CHADEMA kwa sasa ni kumshinikiza Rais wa Tanzania, Mama Samia kuruhusu mchakato wa katiba mpya uanze. Huenda wakafanikiwa kumshawishi Rais kuruhusu utungaji wa katiba mpya. Ila kuna mambo CHADEMA ni kama wanasahau ambayo mimi leo nimeamua kuwakumbusha bila malipo yoyote.

Kwanza wakumbuke Rais wa JMT ni mwanachama na mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi. Serikali inayoongozwa na Rais wa JMT inatekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM. Kwahiyo rais ametokana na CCM na bila kuwa mwanachama wa CCM sio rais. Kwahiyo Rais wa Tanzania wa sasa ni ngumu kwenda kinyume na chama kilichomweka madarakani. Tukumbuke ibara hii;
39.-(1) Mtu hatastahili kuchaguliwa kushika kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano isipokuwa tu kama-
(c) ni mwanachama, na mgombea aliyependekezwa na chama cha siasa;

Inawezekana Rais akaona madai ya CHADEMA yana tija lakini chama chake, CCM, kikawa hakitaki hilo suala basi anaweza tumia ibara ya 37(1) ya katiba kuruhusu mchakato uanze.
Ibara ya 37(1) ya katiba ya JMT
37.-(1) Mbali na kuzingatia masharti yaliyomo katika Katiba hii, na sheria za Jamhuri ya Muungano katika utendaji wa kazi na
shughuli zake, Rais atakuwa huru na hatalazimika kufuata ushauri atakaopewa na mtu yeyote, isipokuwa tu pale anapotakiwa na Katiba hii au na sheria nyingine yoyote kufanya jambo lolote kulingana na ushauri anaopewa na mtu au mamlaka yoyote.

Baada ya uamuzi wa Rais, serikali itaandaa muswada na kuuchapisha katika Gazeti la Serikali na kuwasilishwa Bungeni ambapo baadaye utapitishwa kuwa sheria ya Mabadiliko ya Katiba. Sheria hii itakayotungwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itaridhiwa na Baraza la Wawakilishi Zanzibar kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar ya Mwaka 1984. Je, kwa bunge lenye zaidi ya 90% watakuwa tayari kupitisha huu muswada uliotokana na madai ya wapinzani? Huenda labda wabunge wa CCM wakaona kuna vitu vya kubadili kwenye katiba kwa manufaa ya chama chao wakaamua kupitisha muswada.

Baada ya sheria kusainiwa na rais basi kinachofuata ni uundaji wa tume ya mabadiliko ya katiba. Sheria ya Mabadiliko ya Katiba inampa Rais ambaye ni mwenyekiti wa CCM mamlaka ya kuteua Tume ya Mabadiliko ya Katiba. Hii tume inaweza isiende sawa na matakwa ya mwenyekiti wa CCM na chama chake kama ilivyokuwa kwa jaji Warioba lakini bado CCM itakuwa na nafasi ya kuamua katiba iweje katika hatua ya bunge la katiba ambayo ni hatua ya kujadili rasimu ya katiba iliyopendekezwa na tume.

Kwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Bunge Maalum la Katiba (BMK) linakuwa na wajumbe kutoka makundi matatu. Kundi la kwanza linakuwa ni wabunge wote wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kundi la pili linakuwa ni wajumbe wote wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar. Kundi la tatu linahusisha uteuzi wa wajumbe 201 wanaoteuliwa na Mhe. Rais wa Muungano kutoka makundi mbalimbali ya kijamii hapa Tanzania. Makundi hayo ya kijamii yanakuwa ni AZAKI, taasisi za kidini, vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu, taasisi za elimu, makundi ya watu wenye ulemavu, vyama vya wafanyakazi, vyama vya wafugaji, vyama vya wavuvi, vyama vya wakulima na makundi mengine yenye malengo yanayofanana. Makundi haya yote yanapewa idadi ya wajumbe kama sheria ilivyoelekeza. Hapa kwenye bunge la katiba ndo wapinzani hukwama na kuamua kususa.

Mheshimiwa Rais kwenye uteuzi wa wajumbe 201 hawezi fanya kosa la kuteua watu wenye itikadi tofauti na CCM. Ikumbukwe wabunge wa bunge la JMT ambao karibu wote ni wanaCCM pia ni wabunge wa bunge la mabadiliko ya katiba. Hivyo itoshe kusema zaidi ya nusu ya wabunge wa bunge la katiba wanakuwa ni wanaCCM. Hapa wapinzani lazima wakwame na kutoka nje ya ukumbi wa bunge.

Lakini kabla ya kufika kote huko ni kwamba tayari Mama Samia kashasema kipaumbele chake ni kujenga uchumi na sio kutunga katiba mpya kwa muda huu. Na pia kwa maneno ya ovyo yanayotamkwa na makada wa CHADEMA ni dhahiri kwamba rais na wazalendo wengi wameshawapuuza CHADEMA. Imagine mtu kama Mdude anatamka hadharani atamnyoa Rais wa JMT kwa wembe aliomnyolea mtangulizi wake, au Heche anayesema tusimwite Rais mama, je wataweza kumshawishi rais aamue kuanzishwa mchakato wanaoutaka? Nawashauri wafuasi wa CHADEMA wapuuze harakati za viongozi wao kwasababu ni ndoto za mchana. Nashauri CHADEMA wakae na CCM na kuwaelewesha kwanini CCM isiendelee kuwaona CHADEMA kama wendawazimu.
 
Inawezekana Rais akaona madai ya CHADEMA yana tija lakini chama chake, CCM, kikawa hakitaki hilo suala.
Suala la katiba halipaswi kuwa hisani ama hiari ya ccm. Kwahiyo kama ccm wakikaza shingo wajue kabisa ule mtanange wa "tukose wote" unakuja. Patachimbika, hapatakalika, tutagawana mbao.

Kumbuka: Vijana tunaamini hatupewi ajira kwasabb ya katiba mbovu.
 
Suala la katiba halipaswi kuwa hisani ama hiari ya ccm. Kwahiyo kama ccm wakikaza shingo wajue kabisa ule mtanange wa "tukose wote" unakuja. Patachimbika, hapatakalika, tutagawana mbao.

Kumbuka: Vijana tunaamini hatupewi ajira kwasabb ya katiba mbovu.
Huu ujinga mnaujaribu kwa mama yenu tu, kwa JPM mliweka mikia wote ndani, hata Mange alikuwa jasiri zaidi ya Mbowe, ngoja mlete ujinga tena mpigwe pigwe virungu bahati mbaya hamtakuwa na sehemu za kutuma picha tena kwa kuwa Mama ameshawapa mabeberu maliasili hawatakuwa na muda tena na nyie.
 
Suala la katiba halipaswi kuwa hisani ama hiari ya ccm. Kwahiyo kama ccm wakikaza shingo wajue kabisa ule mtanange wa "tukose wote" unakuja. Patachimbika, hapatakalika, tutagawana mbao.

Kumbuka: Vijana tunaamini hatupewi ajira kwasabb ya katiba mbovu.
Hakuna kitu mtafanya.
 
Suala la katiba halipaswi kuwa hisani ama hiari ya ccm. Kwahiyo kama ccm wakikaza shingo wajue kabisa ule mtanange wa "tukose wote" unakuja. Patachimbika, hapatakalika, tutagawana mbao.

Kumbuka: Vijana tunaamini hatupewi ajira kwasabb ya katiba mbovu.
Wewe hujitambui kabisa Kama wenzio tu. Suala la KATIBA ni la kisiasa, linahitaji majority na Kuna kupiga KURA kwa kila kipengele. Kifupi mtaachwa mseme weeeeee ikifika wakati wa Maamuzi unaambiwa tupige kura. Mchezo kwisha mnasusa Kama mwaka uleeeeee.
Labda nikukumbushe Kama kina Mdee covid-19 hamuwatambui kweli basi huku Bara mna WABUNGE 8 tu wakati CCM wako 382 yaani sawa na asiliamia 2% kwa ukawa na 98% kwa ccm, kule Zanzibar mna WABUNGE 8 kati ya 77 sawa na asiliamia 9+.. na CCM watabaki na WABUNGE 69 sawa na 90%+
Sasa hapo kura zikipigwa mnapita wapi.. Lazima mkimbie na kususa tu.
Hata mkisema itungwe sheria MPYA ya Katiba... JIULIZE mswada unaandaliwa na Nani!??
Bungeni utajadiliwa na Nani..!!??
Bungeni mswaada utapitishwa na Nani!?? Hao Wabunge 8!??
Yaani nyinyi mtapigwa kidemokrasia kabisaaa asubuhi kweupeeee
Huo mkwara mnaopiga Ni sawa na Fisi kumpiga mkwara Tembo..

Wenzenu walitunga Katiba Bora kule Kenya, Zanzibar, S Afrika walianza kutengeneza majority kwanza ndio wakasumbuka na Katiba na baadhi yao waliingia madarakani kabisa ndio wakabadili Katiba. Sasa wewe unataka agenda yako itekelezwe na Serikali ya mwenzio!?
 
Sasa wewe unataka agenda yako itekelezwe na Serikali ya mwenzio!?
Hapo kwenye maandishi meusi. Katiba siyo ajenda ya mtu fulani ama kundi fulani tu. Hii ni ajenda ya watanzania.

Na umeandika kwamba unaweza kutumika mfumo ulioueleza hapo juu kupitisha ujinga wa chama tawala kuwa ndiyo katiba.

Ndugu acha nikuambie wanaodai katiba ni watu smart kuliko hata hao watawala. Acha kukariri.
 
Hapo kwenye maandishi meusi. Katiba siyo ajenda ya mtu fulani ama kundi fulani tu. Hii ni ajenda ya watanzania.

Na umeandika kwamba unaweza kutumika mfumo ulioueleza hapo juu kupitisha ujinga wa chama tawala kuwa ndiyo katiba.

Ndugu acha nikuambie wanaodai katiba ni watu smart kuliko hata hao watawala. Acha kukariri.
Sexless huna hoja unajiropokea tu kama Mdude. CCM haiwezi kutekeleza ajenda ya CHADEMA. Na katika hao watanzania kuna wanaCCM wengi mno. Anyway, pigeni makelele muwezavyo lakini uamuzi uko CCM.
 
Back
Top Bottom