Huwa inashangaza na kusikitisha kuona jinsi utawala huu wa awamu ya tano unavyojitahidi kuhujumu na kuwachukia wapinzani na vyama vya upinzani. Serikali imekuwa inatumia nguvu nyingi za ki-dola na rasilimali fedha kwa mabilioni ya shilingi na wakati mwingine mateso na mauaji vimetumika ili tu kuua wapinzani na upinzani nchi hii.
Tumemsikia Raisi Magufuli alilalama hadharani jinsi nchi ilivyofikishwa pabaya na waliomtangulia.
Cha ajabu hajui kuwa hao anaowalalamikia na kuwalaumu kwa kuifikisha nchi hii pabaya wametoka ndani ya chama chake na amekua nao na anaishi nao.
Raisi amesahau jinsi upinzani ulivyosaidia kuibua maovu na hata kuyakemea maovu yaliyokuwa yakifanyika ndani ya serikali iliyoongozwa na chama chake. Pengine hajui kuwa hata yeye ni zao la mawimbi ya siasa za upinzani wa nchi hii.
Ni upinzani huu huu ulioibua kashfa mbalimbali ndani serikali na kuzuia madhara zaidi, ni upinzani huu huu umeleta changamoto zilizopelekea serikali zetu kujiboresha kiutendaji n.k
Ni vema Raisi akafahamu kufa kwa upinzani hakutaleta amani na usalama kwake au kwa chama chake.
Mwaka 1992 CCM ilikuwa na uwezo wa kuzuia uanzishwaji wa Mfumo wa vyama vingi. Lakini busara na hekima za baadhi viongozi ndani ya chama wakati huo, wakaona ipo haja kubwa ya kuwa na siasa za ushindani na kukosoana.
Ukiona uongozi usiopenda kupewa changamoto na kukosolewa ni sawa na kusafiria mashua iliyotobolewa chini huku maji yakiingia kidogo kidogo.
Unajua mwisho wake itakuwaje?......