Bila upinzani nchi hii ingekuwaje leo?

BEHOLD

JF-Expert Member
Nov 17, 2013
5,047
2,000
Huwa inashangaza na kusikitisha kuona jinsi utawala huu wa awamu ya tano unavyojitahidi kuhujumu na kuwachukia wapinzani na vyama vya upinzani. Serikali imekuwa inatumia nguvu nyingi za ki-dola na rasilimali fedha kwa mabilioni ya shilingi na wakati mwingine mateso na mauaji vimetumika ili tu kuua wapinzani na upinzani nchi hii.

Tumemsikia Raisi Magufuli alilalama hadharani jinsi nchi ilivyofikishwa pabaya na waliomtangulia.
Cha ajabu hajui kuwa hao anaowalalamikia na kuwalaumu kwa kuifikisha nchi hii pabaya wametoka ndani ya chama chake na amekua nao na anaishi nao.

Raisi amesahau jinsi upinzani ulivyosaidia kuibua maovu na hata kuyakemea maovu yaliyokuwa yakifanyika ndani ya serikali iliyoongozwa na chama chake. Pengine hajui kuwa hata yeye ni zao la mawimbi ya siasa za upinzani wa nchi hii.

Ni upinzani huu huu ulioibua kashfa mbalimbali ndani serikali na kuzuia madhara zaidi, ni upinzani huu huu umeleta changamoto zilizopelekea serikali zetu kujiboresha kiutendaji n.k

Ni vema Raisi akafahamu kufa kwa upinzani hakutaleta amani na usalama kwake au kwa chama chake.
Mwaka 1992 CCM ilikuwa na uwezo wa kuzuia uanzishwaji wa Mfumo wa vyama vingi. Lakini busara na hekima za baadhi viongozi ndani ya chama wakati huo, wakaona ipo haja kubwa ya kuwa na siasa za ushindani na kukosoana.

Ukiona uongozi usiopenda kupewa changamoto na kukosolewa ni sawa na kusafiria mashua iliyotobolewa chini huku maji yakiingia kidogo kidogo.
Unajua mwisho wake itakuwaje?......
 
Richard irakunda

JF-Expert Member
Oct 23, 2018
3,512
2,000
Bila upinzani nadhani awamu ya sita ingekuwa na raisi kilaza zaidi ulimwenguni genius BASHITE

Sent using my iPhone using jamiiforum app
 
ForeverMore

JF-Expert Member
Nov 12, 2014
540
1,000
Ungeweza kuta wakina Lissu, Mbowe, Kabwe wote ni CCM.
Na labda awamu ya tano raisi angekuwa Lowassa.
Kikubwa ni kwamba upinzani ungekuwa ndani kwa ndani yaani makundi ndani ya chama kimoja.

Mambo yangeweza kuwa ovyo au mazuri. Hatuwezi jua. Na kujifanya kuwa unajua mambo yange kuwaje ni ukosefu wa imagination.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
TIBIM

JF-Expert Member
Dec 1, 2017
8,026
2,000
Ingekuwa kama unaovoona sasa,upigaji ufisadi rushwa maradufu,mauaji ya raia sababu ya ukosefu wa utawala wa Sheria, viongozi wa dini lzm upigwe chapa ili wale yaani wanamuogopa mwanadamu kuliko Mungu.
 
TIBIM

JF-Expert Member
Dec 1, 2017
8,026
2,000
Ingekuwa jela ndogo inayosimamiwa na manyapara na kupe wa Lumumba
Ushauri wa chid wameambiwa jela haina mwenyewe hivo waboreshe magereza kuwe kuzuri,hakuna kiitwacho kinga kinga ni busara za ajae maana katiba sio msahafu makaburi yatafukuliwa mbeleni juu ya matumizi mabaya ya Madaraka, matumizi mabaya ya fedha za umma Bila idhini ya bunge, upotevu wa watu pasipo hatua,nk.Hivo wahusika chain nzima wajiandae tu halitosalia jiwe lisiloguswa ili taifa lipone.Wamepanda chuki watavuna chuki Leo punda ni wa thamani kuliko MTU.
 
GEBA2013

JF-Expert Member
Feb 22, 2014
3,758
2,000
UPINZANI IMARA ni afya ya nchi
Upinzani ni dira ya nchi
Upinzani ni kioo ya nchi

Sisi tuliopita nyakati za chama kimoja tunajua athari yakutokuwa na vyama vya upinzani.
 
Kikarara78

JF-Expert Member
Nov 18, 2010
1,496
2,000
Boss BEHOLD Mada nzuri sana, nilishawahi kuliongelea hili.
Hakuna Maendeleo bila UPINZANI wa kweli na madhubuti. Watu wengi wamekuwa wanabeza sana Upinzani,
Ila ukweli Upinzani wamefanya kazi kubwa sana, iwapo wanakabiliwa na changamoto nyingi sana za kazi zao.

Kwa ujumla Upinzani upo kila mahali, Kwenye Familia zetu, Mashuleni, Makazini, yaani popote pale lazima utakuta Upinzani.

Huwa inashangaza na kusikitisha kuona jinsi utawala huu wa awamu ya tano unavyojitahidi kuhujumu na kuwachukia wapinzani na vyama vya upinzani. Serikali imekuwa inatumia nguvu nyingi za ki-dola na rasilimali fedha kwa mabilioni ya shilingi na wakati mwingine mateso na mauaji vimetumika ili tu kuua wapinzani na upinzani nchi hii.

Tumemsikia Raisi Magufuli alilalama hadharani jinsi nchi ilivyofikishwa pabaya na waliomtangulia.
Cha ajabu hajui kuwa hao anaowalalamikia na kuwalaumu kwa kuifikisha nchi hii pabaya wametoka ndani ya chama chake na amekua nao na anaishi nao.

Raisi amesahau jinsi upinzani ulivyosaidia kuibua maovu na hata kuyakemea maovu yaliyokuwa yakifanyika ndani ya serikali iliyoongozwa na chama chake. Pengine hajui kuwa hata yeye ni zao la mawimbi ya siasa za upinzani wa nchi hii.

Ni upinzani huu huu ulioibua kashfa mbalimbali ndani serikali na kuzuia madhara zaidi, ni upinzani huu huu umeleta changamoto zilizopelekea serikali zetu kujiboresha kiutendaji n.k

Ni vema Raisi akafahamu kufa kwa upinzani hakutaleta amani na usalama kwake au kwa chama chake.
Mwaka 1992 CCM ilikuwa na uwezo wa kuzuia uanzishwaji wa Mfumo wa vyama vingi. Lakini busara na hekima za baadhi viongozi ndani ya chama wakati huo, wakaona ipo haja kubwa ya kuwa na siasa za ushindani na kukosoana.

Ukiona uongozi usiopenda kupewa changamoto na kukosolewa ni sawa na kusafiria mashua iliyotobolewa chini huku maji yakiingia kidogo kidogo.
Unajua mwisho wake itakuwaje?......
 
MPIGA ZEZE

JF-Expert Member
May 16, 2011
2,454

Hii ni hoja isiyohitaji mjadala (kwa waTz wanaoangalia mambo objectively). Kama Mtukufu Rais angekuwa na washauri wazuri au angekuwa anashaurika (pia ni jambo lisilohitaji ushauri, alipaswa kuliona na kulitambua kama Mtz ye yote yule) angewachukulia wapinzani (wanasiasa walio katika vyama vya upinzani) na upinzani kwa jumla (wananchi wenye mitazamo tofauti na ya kwake na hawajinasibishi na chama cho chote - hawa ni wengi sana) kama wadau wa maendeleo (kwa maana pana ya dhana ya maendeleo. Dhana aliyo nayo kuhusu maendeleo ni dhana finyu sana na ninafikiri inachangia sana kumpotosha na kuelekeza taifa kusikostahili).
 
Emisesayo

Senior Member
Feb 16, 2019
129
250
najaribu kuwaza kwasauti.Bashite angelikua naibu rais alafu makao makuu ya nchi yangekuwa mwanza
 
uporo wa wali ndondo

JF-Expert Member
Dec 3, 2013
3,204
2,000
Tungekuwa mbali mno..wapizani wametucheleweshea maendeleo sababu ya kuwasubiria waseme wanataka nini wakati wao wenyewe hawajui wanataka nini.
 
semikchz

Member
Feb 13, 2019
5
45
Boss BEHOLD Mada nzuri sana, nilishawahi kuliongelea hili.
Hakuna Maendeleo bila UPINZANI wa kweli na madhubuti. Watu wengi wamekuwa wanabeza sana Upinzani,
Ila ukweli Upinzani wamefanya kazi kubwa sana, iwapo wanakabiliwa na changamoto nyingi sana za kazi zao.

Kwa ujumla Upinzani upo kila mahali, Kwenye Familia zetu, Mashuleni, Makazini, yaani popote pale lazima utakuta Upinzani.
Sio kila nchi ili iendelee lazima kuwe na upinzani.kwanz upinzan ndo chanzo cha nchi za third world countries kufilisika kutokan na muda na pesa nyingi hutumika kwa ajil ya vitu vya kipumbavu.kuliko kuendeleza nchi husika.pia janga la umasikini ndio tatizo, kiongozi anapoingia madarakani lazima ajibenefishe yeye kwanz kisha hapo ndo nchi inafata.just remind u mfumo wa vyama vingi uliletwa kama condition kwa nchi za kimaskini ili ziweze kupata misaada mbali mbali.kwa upande mwingine ni sawa tu upinzani ukiondolewa na nchi itadevelop

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kikarara78

JF-Expert Member
Nov 18, 2010
1,496
2,000
Sio kila nchi ili iendelee lazima kuwe na upinzani.kwanz upinzan ndo chanzo cha nchi za third world countries kufilisika kutokan na muda na pesa nyingi hutumika kwa ajil ya vitu vya kipumbavu.kuliko kuendeleza nchi husika.pia janga la umasikini ndio tatizo, kiongozi anapoingia madarakani lazima ajibenefishe yeye kwanz kisha hapo ndo nchi inafata.just remind u mfumo wa vyama vingi uliletwa kama condition kwa nchi za kimaskini ili ziweze kupata misaada mbali mbali.kwa upande mwingine ni sawa tu upinzani ukiondolewa na nchi itadevelop

Sent using Jamii Forums mobile app

Boss semikchz Unajua Mh. Rais alipita kutokana na Upinzani ndani wa Chama chao??? Labda utueleze wewe kwa uelewa wako, Upinzani ni nini??? !!!
Pili, hizo Nchi zilizoendelea unataka kutuambia hawana Upinzani???
Tofauti Nchi zilizoendelea Upinzani wao ni wa Maendeleo, Chaguzi zikiisha wanakuwa kitu kimoja, lakini kwetu ni tofauti. Mifano ni mingi.
 
Nanye Go

JF-Expert Member
Oct 29, 2018
6,820
2,000
Bila upinzani nchi ingekuwa Mufilisi, wangeibaaa na labda nasisi tungeisha ibiwa.
 
Said Stuard Shily

JF-Expert Member
Jul 18, 2017
1,304
2,000
Tungekuwa mbali mno kwani chini ya chama kimoja tunge-apply Intraspecific critism politics other than rubbish critism from CHADEMA .
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom