Bila upinzani kutegemea nguvu kutoka nje ya siasa hawatashinda. Case Study: DRC.

ungejua kuitofautisha CCM na vyama vingine vinavyoweka wafalme madarakani , usingesema haya. kwa yaliyotokea Kongo .
Mkuu, kama CCM hakuna ufalme, ilikuwaje Benard Membe akatolewa povu kubwa wiki mbili tatu tu zilizopita?
 
ungejua kuitofautisha CCM na vyama vingine vinavyoweka wafalme madarakani , usingesema haya. kwa yaliyotokea Kongo , huwezi kufananisha na Tanzania na kwa Tanzania CCM tutaongoza sana mpaka tuseme basi kwa sababu :nia, uwezo na sababu tunazo.

Tofauti ya CCM na hivyo vyama vingine ni kwamba CCM inabadalisha kiongozi , hivyo ni vigumu kwa kiongozi kuchokwa na tunachagua viongozi waliobeba matarajio ya wananchi (mfano ni Rais Magufuli).

wananchi hawabadilishi chama kwa sababu wana mapenzi nacho, wananchi wanachagua chama kilichobeba matarajio yao kiuchumi, kidiplomasia, kimaendeleo na kijamii na kwa CCM ina hazina ya viongozi wenye mtazamo wa kubadilisha nchi na wananchi wake hivyo si rahisi CCM kuchokwa na kupelekea kuchagua upinzani wq matukio
Ccm huwa haichaguliwi,inajichagua yenyewe kwa kutumia tume yao,na polisi,acha kabisa kuwasema wananchi kuwa wanaichagua,wananchi walishaichoka na wewe unajua hilo,hutaki kusema kwakuwa ukiwa ccm na akili zonaenda likizo.
Sijaona matarajio aliyobeba mkuu wa kaya kwa wananchi zaidi ya shida tu anayotupa. Hana hata utu kabisa. Mifano ipo mingi tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vyama vya upinzani Tanzania hasa Zanzibar vimekuwa vikishinda chaguzi mbalimbali lkn vimekuwa vikiporwa ushindi kwa sababu havina nguvu yeyote zaidi ya kutegemea sanduku la kura. Sanduku la kura peke yake haliwezi kuwapeleka ikulu.

Ushindi wa uchaguzi hasa kiti cha urais ni zaidi ya siasa, chama cha Mapinduzi hakitegemei siasa kushinda uchaguzi, kina tegemea nguvu ya ziada nje ya siasa, siasa inatumika kama ngazi tu ya kuhalalisha ushindi.

Leo Kongo upinzani umetangazwa washindi sio kwa nguvu zao, Tume ya uchaguzi CENI ilikuwa na uwezo kabisa wa kugeuza matokeo lkn haikuthubutu kutokana na nguvu ya nje hasa Kanisa Katoliki na shinikizo la nchi za Ulaya na Marekani ambayo tayari ilianza kusogeza manowari zake kwenye pwani ya Congo.Trump sent 80 US troops to Gabon over possible violence in DR Congo

Ushindi wa uchaguzi unategemea nguvu ya uchumi, unategemea jumuiya za kijamii, unategemea nchi marafiki, unategemea ushawishi kwenye jumuiya za kimataifa, bila kuwa supported na makundi haya huwezi kuingia ikulu hata kama utashinda kwa 100%.

CCM ina rafiki zake China, FRELIMO, ANC, Swapo, MPLA haiogopi hata kuwakaribisha kwenye kampeni zake, na ndio wanaosaidiana hata mbinu za kuiba matokeo, upinzani unaogopa kuwatambua marafiki zake eti wataambiwa wanashirikiana na mabeberu. Acheni uoga.

Shirikianeni na viongozi wa dini, Makanisa na Misikiti waziwazi msiogope kuambiwa mnaingiza dini kwenye siasa, mbona wao kila sehemu wanaongozana nao. Shirikianeni na vyama vya kijamii kama LHRC, TUKTA, CWT, TLC, NGOs, hamna sababu ya kujifichaficha.

Tafuteni mashirika ya ndani na nje yenye influence na politics za maziwa makuu, tell them what you think Tanzania is ought to be, hakuna sababu ya kujifungia Ufipa na Mtendeni kama watoto yatima, tell the world know what is happening in Tanzania.

Tafuteni mapema misaada kwa vyama na nchi marafiki ili kujiandaa na uchaguzi wa 2020 acheni kutegemea ruzuku, nani akupe ruzuku ili umshinde, mlishaambiwa mapema kuwa serikali haiwezi kuondoka kwa kipande cha karatasi ya kura.

Uoga wenu ndio kushindwa kwenu.

Politics is beyond ballot box.

By, Mwana JF mzoefu Quinine.
Hongera mkuu umeongea pointi sana. Lakini nitoe comment kuhusu ulichosema kuhusu viongozi wa Dini wa hapa Tanzania. Hao ni tatizo kubwa sana. wanatumiwa na serikali tena kwa peremende tu. Congo kanisa liko imara sana.Mfano tu mwaka jana Kanisa lilishiriki maandamano na mapadre wakiwa katika mavazi yao ya ibada waliandamana na kuhimili mabomu ya machozi. hii ilikuwa ishara yenye nguvu sana kwamba kanisa liko imara.
catholicCongo-3j.jpg

Katika maandamano hayo, watu 6 waliuwawa, zaidi 50 walijeruhiwa na wengi walikamatwa na Polisi. Kama unavyoona katika picha, mapadre walishiriki kikamilifu.

catholicCongo-4.png

Hii ilikuwa ni sadaka ya damu iliyomwagika. na cha kushangaza, hata madhehebu mengine ya kikristu PAMOJA NA WAISLAMU, wote waliunga mkono maandamano hayo. Kwa hiyo hicho kilichotokea kwenye uchaguzi, ni matokeo ya sadaka iliyotolewa na damu ya wapambanaji iliyomwagika, imegharimia ushindi huu wa upinzani.

Sasa njoo hapa kwetu uone kichekesho. Kanisa Katoliki sasa hivi limefyata mkia kabisa. utashangaa Askofu tena "Senior" kwa maana ya umri wake na kwamba amewahi kuwa Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, namuongelea Askofu Severin NiweMugizi, mpaka hivi sasa passport yake inashikiliwa na Serikali, ikiwa ni namna ya kumtisha na ku-discourage maaskofu wengine wasijaribu kutikisa kiberiti. lakini Maaskofu wenzie wameuchuna, wamemwacha kwenye mataa apambane na hali yake. Na kama haitoshi, wakati wa sherehe za kuadhimisha miaka 150 ya uinjilishajim, Maaskofu Katoliki walidiriki kumwalika Rais Magufuli na kumpa nafasi ya kuongea. walitumia pia nafasi hiyo KUOMBA MISAADA MBALIMBALI!!!! UDHAIFU GANI HUU?

YOHANE MBATIZAJI alithubutu kumkoromea HERODE, mfalme MWENYE NGUVU enzi hizo. na hatimaye aliuwawa lakini mpaka leo anakumbukwa.

Kwa hiyo ndugu usijaribu kutulinganisha na Congo kwa upande wa viongozi wa dini.
 
Vyama vya upinzani Tanzania hasa Zanzibar vimekuwa vikishinda chaguzi mbalimbali lkn vimekuwa vikiporwa ushindi kwa sababu havina nguvu yeyote zaidi ya kutegemea sanduku la kura. Sanduku la kura peke yake haliwezi kuwapeleka ikulu.

Ushindi wa uchaguzi hasa kiti cha urais ni zaidi ya siasa, chama cha Mapinduzi hakitegemei siasa kushinda uchaguzi, kina tegemea nguvu ya ziada nje ya siasa, siasa inatumika kama ngazi tu ya kuhalalisha ushindi.

Leo Kongo upinzani umetangazwa washindi sio kwa nguvu zao, Tume ya uchaguzi CENI ilikuwa na uwezo kabisa wa kugeuza matokeo lkn haikuthubutu kutokana na nguvu ya nje hasa Kanisa Katoliki na shinikizo la nchi za Ulaya na Marekani ambayo tayari ilianza kusogeza manowari zake kwenye pwani ya Congo.Trump sent 80 US troops to Gabon over possible violence in DR Congo

Ushindi wa uchaguzi unategemea nguvu ya uchumi, unategemea jumuiya za kijamii, unategemea nchi marafiki, unategemea ushawishi kwenye jumuiya za kimataifa, bila kuwa supported na makundi haya huwezi kuingia ikulu hata kama utashinda kwa 100%.

CCM ina rafiki zake China, FRELIMO, ANC, Swapo, MPLA haiogopi hata kuwakaribisha kwenye kampeni zake, na ndio wanaosaidiana hata mbinu za kuiba matokeo, upinzani unaogopa kuwatambua marafiki zake eti wataambiwa wanashirikiana na mabeberu. Acheni uoga.

Shirikianeni na viongozi wa dini, Makanisa na Misikiti waziwazi msiogope kuambiwa mnaingiza dini kwenye siasa, mbona wao kila sehemu wanaongozana nao. Shirikianeni na vyama vya kijamii kama LHRC, TUKTA, CWT, TLC, NGOs, hamna sababu ya kujifichaficha.

Tafuteni mashirika ya ndani na nje yenye influence na politics za maziwa makuu, tell them what you think Tanzania is ought to be, hakuna sababu ya kujifungia Ufipa na Mtendeni kama watoto yatima, tell the world know what is happening in Tanzania.

Tafuteni mapema misaada kwa vyama na nchi marafiki ili kujiandaa na uchaguzi wa 2020 acheni kutegemea ruzuku, nani akupe ruzuku ili umshinde, mlishaambiwa mapema kuwa serikali haiwezi kuondoka kwa kipande cha karatasi ya kura.

Uoga wenu ndio kushindwa kwenu.

Politics is beyond ballot box.

By, Mwana JF mzoefu Quinine.
Nguvu gani ya nje itabadili matokeo ya ndani bila kufanya uvamizi kama Ivory Coast?
Wananchi Wakiwaamini watawapigia kura ba watasimama kidete wapinzani Wapate madaraka.
Haya mambo ya kutegemea nguvu za nje yatawatokea watu puani. There is no free lunch in this world. Nguvu kubwa ni nguvu ya ndani mangii
 
Kwa upande wa diplomatic DRC na Tz ni tofauti sana ndomana si rahisi kwa Tanzania upinzani waingie Ikulu.

Sent from my SM-J530F using Tapatalk
 
Hii ni wazi kabisa. Bila external forces, wasahau suala la kushinda nafasi hasa ya URAISI.
 
Katika mbinu ambayo CCM imeitumia kuendelea kuwa madarakani ni kubadili wagombea na mwenyekiti. Hii inasababisha hichi chama kiwe kama ni muunganiko wa vyama vingi ndani ya chama kimoja. Siasa zao zinabadilika badilika sana. Embu angalia CCM ya magufuli Ilivyo tofauti na CCM ya kikwete. Utasema ni vyama tofauti kabisa. Jaribu kuvuta picha CCM ya mtu mwingine wakati utakapofika labda ccm ya Membe au ccm ya makamba nayo itakuwa tofauti kabisa na ya Magufuli. Sasa ukichukua hili + sapoti ya Jeshi + usalama wa Taifa hivi upinzani unachomoaje?
Hizo + + ongeza na Tume ya uchaguzi. In fact Vyama pinzani vinakabiliana na CCM, Jeshi, Usalama, Tume n.k. Yaani timu ya watu wawili inashindana na timu ya watu 22. Ni ngumu kushinda.
 
Back
Top Bottom