Bila upinzani imara, Magufuli asingekuwa Rais

DR. MWAKABANJE

JF-Expert Member
Nov 7, 2012
1,976
3,124
Habari kila mwanachama hapa.

Ukweli ni kwamba tangu awamu ya tano ishike hatamu ya uongozi kuna mambo mengi yamebadilika sana, yaweza kuwa chanya au hasi...tunashukuru kwa yaliyomema lakini lazima tuyasemee zaidi yaliyohasi ili tujenge Tanzania iliyo salama na bora kwa kuishi kwa kila mmoja wetu....isiwe Tanzania ya wachache wenye kulindwa na kila aina ya silaha..

Tanzania ina makundi mbali mbali ya watu lakini kisiasa wapo wapinzani, chama tawala na walio na makengeza ya kisiasa yaani hawa sio CCM wala upinzani wao wanaangalia kote kote na kuleta mzania wa hoja kwa kuzingatia maslahi ya Taifa ya leo na kesho, wale wenye makengeza nawaalika tujadili hoja zifuatazo;

1. Awamu hii chuki baina ya makundi mawali hasimu tajwa imekuwa kubwa sana, swali je CCM chini ya mwenyekiti wake wanajua kuwa bila upinzani Magufuli asingekuwa rais? Yaani kiufupi kusingekuwa na serikali inayoitwa ya Magufuli inayojiita inatetea wanyonge. Sasa lengo la kukandamiza upinzani kwa kiwango tunachoshuhudia lengo ni nini kuna fichwa nini? Bila upinzani CCM hawakuwaza kumsimamishi JPM awe mgombea wa urais ni hadi pale walipoona hakuna mtu atakayesimama na akaeleweka kwa wananchi wakaona bora JPM, hivyo awe waziri, RC DC na wengine has wa kuteuliwa awamu hii wajue ni kwa sababu ya wapinzani wamepata nafasi hizo, yaani kwa mfano inawezekana kabisa rais hata angetoka CCM lakini si JPM Makonda au Gambo wasingekuwa maRC.

2. Maoni mbadala yanachukuliwa kama upinzani na upinzani unachukuliwa kama uasi na usaliti, hii dhana inatubomoa sana na mbaya zaidi viongozi wetu awamu hii wanatuaminisha hivyo, hawajengi hata hoja inabaki tu kuporomosha matusi au vijembe...nina mashaka hata ndani ya chama tawala dalili zipo kuwa hakuna kuhoji, kupinga wala kudadisi, ni mbaya sana tukiacha viongozi wetu wafikiri na kuamua kila kitu kwa niaba yetu....anaye sikika ndani ya CCM ni mwenyekiti na katibu mwenezi tu ukiuliza jibu ni chama kina taratibu zake. Ukweli ni kuwa tumekuwa taifa la kuto kuhoji awamu hii.

3. Je CCM wana uhakika kuwa mfumo wa sasa wa ukandamizaji demokrasia unawajenga zaidi?? Kuna viongozi ukiwasikiliza wanahisi wao walikuwa wasafi sana ndo maana wakapewa dhamana ya kutuongoza na wanafikiri serikali ya Kikwete ilichukiwa kwa ufisadi tu...hakuna hata upambane na ufisadi huku ukinyima haki ni sawa na bure, be just, be fair kuanzia matendo hadi maneno utapendwa tu wala hutatumia nguvu....kama ilivyo kifo ni kwa kila binadamu hata madaraka yatapita. Kwa ujumla wake hata ukataze mikutano huku wewe ukifanya kwa mgongo mwingine siku ya mwisho wewe uliyepo madarakani utakuwa na wakati mgumu kuliko mpinzani wako.

Sisi sote ni ndugu tupendane hata kwa tofauti tulizonazo...ubaguzi na chuki ni tabia tena ipandayo chuki na mauti. Anayemchukia CCM au upinzani ujue anaroho ya chuki moyoni mwake hata kwa watu/ makundi mengine yasiyo sawa naye kama waliotofauti na dini yake, rangi yake, kabila lake, waliomzidi kipato, fikra nk.

Asubuhi njema.
 
Kisha leo anawaona kama mbwa wakati lowassa ndie aliye msaidia kupata kura. Pia inasemekana kwa upande wa ccm aliyeshinda alikua Amina kwa kura za kambi ya lowassa.
 
Baada ya Lowasa ku- cross the floor, ikaonekana hapa timbwili haliwezekani. Wakakorofishana kwenye vikao. Membe, Lowasa wakaonekana wameonewa. Basi kama mbaya mbaya, kila kundi likose. Basi ndio wakateuliwa ambao hawakuwa na mashiko ,ambao hawakuwa na upande. Ndio akapita "Mungu"!
 
Alikuwepo mfalme na falme zilipita. Huu nao utapita. Hakuna kitakachoishi milele.

Nimkumbushe Rais wangu magufuli na Serikali yake ya CCM mafanikio makubwa hupimwa pale utakapokuwa haupo tena.
 
Habari kila mwanachama hapa.

Ukweli ni kwamba tangu awamu ya tano ishike hatamu ya uongozi kuna mambo mengi yamebadilika sana, yaweza kuwa chanya au hasi...tunashukuru kwa yaliyomema lakini lazima tuyasemee zaidi yaliyohasi ili tujenge Tanzania iliyo salama na bora kwa kuishi kwa kila mmoja wetu....isiwe Tanzania ya wachache wenye kulindwa na kila aina ya silaha..

Tanzania ina makundi mbali mbali ya watu lakini kisiasa wapo wapinzani, chama tawala na walio na makengeza ya kisiasa yaani hawa sio CCM wala upinzani wao wanaangalia kote kote na kuleta mzania wa hoja kwa kuzingatia maslahi ya Taifa ya leo na kesho, wale wenye makengeza nawaalika tujadili hoja zifuatazo;

1. Awamu hii chuki baina ya makundi mawali hasimu tajwa imekuwa kubwa sana, swali je CCM chini ya mwenyekiti wake wanajua kuwa bila upinzani Magufuli asingekuwa rais? Yaani kiufupi kusingekuwa na serikali inayoitwa ya Magufuli inayojiita inatetea wanyonge. Sasa lengo la kukandamiza upinzani kwa kiwango tunachoshuhudia lengo ni nini kuna fichwa nini? Bila upinzani CCM hawakuwaza kumsimamishi JPM awe mgombea wa urais ni hadi pale walipoona hakuna mtu atakayesimama na akaeleweka kwa wananchi wakaona bora JPM, hivyo awe waziri, RC DC na wengine has wa kuteuliwa awamu hii wajue ni kwa sababu ya wapinzani wamepata nafasi hizo, yaani kwa mfano inawezekana kabisa rais hata angetoka CCM lakini si JPM Makonda au Gambo wasingekuwa maRC.

2. Maoni mbadala yanachukuliwa kama upinzani na upinzani unachukuliwa kama uasi na usaliti, hii dhana inatubomoa sana na mbaya zaidi viongozi wetu awamu hii wanatuaminisha hivyo, hawajengi hata hoja inabaki tu kuporomosha matusi au vijembe...nina mashaka hata ndani ya chama tawala dalili zipo kuwa hakuna kuhoji, kupinga wala kudadisi, ni mbaya sana tukiacha viongozi wetu wafikiri na kuamua kila kitu kwa niaba yetu....anaye sikika ndani ya CCM ni mwenyekiti na katibu mwenezi tu ukiuliza jibu ni chama kina taratibu zake. Ukweli ni kuwa tumekuwa taifa la kuto kuhoji awamu hii.

3. Je CCM wana uhakika kuwa mfumo wa sasa wa ukandamizaji demokrasia unawajenga zaidi?? Kuna viongozi ukiwasikiliza wanahisi wao walikuwa wasafi sana ndo maana wakapewa dhamana ya kutuongoza na wanafikiri serikali ya Kikwete ilichukiwa kwa ufisadi tu...hakuna hata upambane na ufisadi huku ukinyima haki ni sawa na bure, be just, be fair kuanzia matendo hadi maneno utapendwa tu wala hutatumia nguvu....kama ilivyo kifo ni kwa kila binadamu hata madaraka yatapita. Kwa ujumla wake hata ukataze mikutano huku wewe ukifanya kwa mgongo mwingine siku ya mwisho wewe uliyepo madarakani utakuwa na wakati mgumu kuliko mpinzani wako.

Sisi sote ni ndugu tupendane hata kwa tofauti tulizonazo...ubaguzi na chuki ni tabia tena ipandayo chuki na mauti. Anayemchukia CCM au upinzani ujue anaroho ya chuki moyoni mwake hata kwa watu/ makundi mengine yasiyo sawa naye kama waliotofauti na dini yake, rangi yake, kabila lake, waliomzidi kipato, fikra nk.

Asubuhi njema.
kaka kwa kweli umenena, wenye akili tumekuelewa sana,
 
Tanzania tuna upinzani dhaifu na usio na dira wala malengo
 
Upinzani imara upo ccm. Magufuli kainuliwa na makundi pinzani ndani ya ccm.

Nje ya ccm hakuna upinzani imara maana wao wanategemea kupata wagombea wa nafasi kubwa kutokea ccm
 
Back
Top Bottom