Bila shaka tumepata picha kamili, uvunjifu wa haki huzalisha chuki ya kudumu

Nyankurungu2020

JF-Expert Member
Oct 2, 2020
4,087
6,568
Ukienda South Africa hii leo ukakutana na ndugu wa Steven Biko na ukafanya nao mazungumzo lazima watakuambia kweli kuwa kuna kovu kubwa ndani ya mioyo yao.

Maana ndugu yao aliuawa bila hatia na utawala dhalimu wa makaburu. Tena aliuawa kifo kibaya. Huu ni mfano tu ambao unaonesha namna gani ukiukwaji wa haki za binadamu unaweza kuzalisha chuki ya kudumu.

Kwa hapa Tanzania kuna chuki kubwa sana ndani ya mioyo ya watanzania hasa baada ya Tundu Lissu kumiminiwa risasi zaidi ya 33 kama vile yeye sio binadamu.

Maana ni tukio ambalo kila mtu haamini kuwa anaweza kufanyiwa binadamu aliyekuwa anahoji masuala ya msingi juu ya taifa lake.

My take: Taifa linalotenda haki humuinua Mungu.
 
Kuna mijitu inajidanganya eti taarifa za kifo cha mtu katili zikitolewa italeta taharuki. Watu wanasubiria kwa haaamu sana kusikia hivyo tunywe bia mpka asubuhi. Baada ya dhiki sasa faraja.
Asubuhi hii kuna mtu nimemsikia akisema hajawahi kunywa pombe ila ikitangazwa jamaa ka RIP atakunywa pombe hadi alale bar. Hapa ndipo awamu ya tano ilipowafikisha Watanzania.
 
Umetoa mfano wa Lissu ambaye alikuwa hapa nchi kwa zaidi ya miezi 3 akasepa kwa njia ya kihuni. Kwa nini unamsemea wakati muda aliokuwepo hapa angefuatilia upelelezi wa shambulio dhidi yake?

Rejea kauli zake kwenye majukwaa ya kampeni, je, ziligusa kushambuliwa kwake zaidi ya kufitinisha Rais aliyeko madarakani na jamii. Huoni yeye Lissu ndiye mwenye silika ya visasi?
 
Sidhani kama aliondoka kihuni. Pia sidhani kama anatakiwa afuatilie suala lake. Ila nimezungumzia juu ya shambulio lake limejenga chuki kubwa ndani ya mioyo ya watanzania.
 
Nikiwa job jana, njemba zingine hazinywi pombe lakin wamekiri watapiga K Vant za kutosha na nyama choma.
Kama hivi
JamiiForums1336214174.jpg
 
Umetoa mfano wa Lissu ambaye alikuwa hapa nchi kwa zaidi ya miezi 3 akasepa kwa njia ya kihuni. Kwa nini unamsemea wakati muda aliokuwepo hapa angefuatilia upelelezi wa shambulio dhidi yake?

Rejea kauli zake kwenye majukwaa ya kampeni, je, ziligusa kushambuliwa kwake zaidi ya kufitinisha Rais aliyeko madarakani na jamii. Huoni yeye Lissu ndiye mwenye silika ya visasi?
Ficha ujinga wako wew kibwetele.
Subiria mama yko apigwe risasi ndio uharishe hyo maneno mdomoni mwako. Taifa bado lina watu wajinga sana wa aina yako
 
Chuki imo humu mitandaoni mitaani kuko safi mno hakuna chuki
Chuki kama itakuwa mtandaoni, mtaani au mahali popote, ukweli utabakia pale pale kuwa kuna chuki.

Chuki ya mtandaoni unaifahamu kwa sababu watu wamejificha kwa ID fake, huko mtaani hakuna wa kuonesha wazi kwa sababu akiionesha, atajutia au kupotezwa kabisa.

Chuki ipo, hilo halibishaniwi. Chuki dhidi ya utawala huu ipo wazi toka makundi mbalimbali, hasa kwa sababu ya utawala kutotenda wala kusimamia haki.
 
Back
Top Bottom