Bila shaka ajenda ya kuomba ongezeko la posho ilikuwa ni ya madiwani wa CHADEMA, je watasusia vikao?

jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
32,631
2,000
Bila shaka yoyote na kwa kujikumbusha matukio kadhaa ni wazi kuwa ajenda ya madiwani kutaka kuongezewa posho ilikuwa ni ajenda iliyopenyezwa na madiwani wa Chadema.
Ajenda hii ilikuwa ni ajenda mbaya ya kuwaabisha madiwani ambao wanatakiwa kuwa karibu na wananchi na kuibua shida za wananchi au kutoa mapendekezo kwa serikali kuu jinsi ya kuboresha maisha ya wananchi wa hali ya chini na sio kutaka kunenepesha matumbo yao.

Tunakumbuka mkuu wa mkoa wa Arusha na mkurugenzi wa jiji la Arusha alivyotukanwa na madiwani wa chadema wakiongozwa na Lema kisa kukata kiwango cha posho cha madiwani.
Tunakumbuka pia madiwani wa Meru walivyosusia vikao katika halmashauri hiyo kisa kupunguzwa kwa posho.

Pia wapo madiwani wa manispaa ya Moshi ambao waligomea mafunzo ya uwezeshaji yaliyoandaliwa na Tamisemi kisa posho.

Mifano hii inaashiria kuumizwa sana kwa madiwani wa chadema kutokana na punguzo la posho.Imagine diwani wa Arusha alikuwa analiliia kulipwa posho ya nauli sh 100000 ilihali nauli ya tax haizidi elfu tatu.

Hakuna shaka ushawishi wa madiwani hawa katika mkutano wa ALAT ukipelekea kumtega Magufuli awaingezee posho.

Kwa kuwa Magufuli ni mzalendo na amedhamiria kutuokoa kutoka makucha ya wanasiasa waroho alikataa wazi wazi na bila kumung'unya neno,hasira ya kukataliwa kwa ajenda ilipelekea upotoshaji wa kauli ya Rais na mjadala ukahamishiwa kwenye nyongeza ya mishahara.

Ni vyema tujadili na kujua nini kitafuata baada ya Magufuli kukataa ombi hili la madiwani wa chadema lililowasilishwa kwa mdomo wa AlAT.

JE WATASUSIA VIKAO?
 
ikyenja

Senior Member
Mar 18, 2017
103
225
mnataka kutuambia kwamba mh mkuu hajui tofauti kati ya posho na mshahara?

Acheni udhalilishaji
 
Babati

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
38,329
2,000
Mwenyekiti wa ALAT ni CCM mwenzako na ndiyo aliyependekeza kuwepo kwa hiyo posho
 
Tairi bovu

JF-Expert Member
Sep 28, 2017
3,067
2,000
Maisha ya wananchi yanaathirika na kupandishwa posho za madiwani.Ni kwa nini unasema ninatania?wabaotania ni hao madiwani wanaotaka kuongezewa posho ilihali wananchi wanaowaongoza hawana fedha.
Maisha ya wananchi yanaathirika na kupandishwa posho za madiwani.Ni kwa nini unasema ninatania?wabaotania ni hao madiwani wanaotaka kuongezewa posho ilihali wananchi wanaowaongoza hawana fedha.
We jinga tu tangu uhuru hayo.maendleo ya wananchi hamjayaleta kwa sababu ya posho za madiwani? Jinga kweli wewe? Mmeuza nyumba za umma kwa vimada wenu na kujenga nyingine huko si nikufisidi mali za hao wananchi?rada, ndege, escrow, epa, meremeta haya yote yasingefanyika hao wananchi si wangekuwa na pesa yameletwa na hao madiwani wa chadema! Pesa kununua kivuko kibovu ni shilingi ngapi? Si zingeenda kwa hao wananchi? Lugumi je si pesa zingeenda kwa wananchi? Wananchi mnawajua leo wakati.mmeshauza nchi na watu wake? Pesa zilizotumika kuwahonga TUCTA ili waufyate si zingeenda kwa wananchi .
Wewe Jinga lao nitakuona wa maana kama UTAMSHAURI RAISI ATANGAZE MALI ZAKE ZOTE KAMA SHERIA INAVYOTAKA (SHERIA YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA) ILI TUJUE YEYE NI MSAFI HIVYO?
 
Shakidinkili

JF-Expert Member
Sep 28, 2013
459
225
Jadili kwanza uzalendo wa wabunge wetu ambao wanalamba posho kubwa za vikao mjengoni wakati ndio kazi walioiomba na wanalipwa mshahara mkubwa kwa kufanya kazi hiyo ya kutuwakilisha.
 
jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
32,631
2,000
Mwenyekiti wa ALAT ni CCM mwenzako na ndiyo aliyependekeza kuwepo kwa hiyo posho
Ukweli ni kuwa nyuma ya hilo ombi kuna ushahidi kama nilivyosema hapo juu wa shinikizo la madiwani wa Chadema.Upuuzi ni kujidai huoni ushahidi huo.
 
mjingamimi

JF-Expert Member
Aug 3, 2015
25,778
2,000
Kuumbe ni ajenda ya madiwani wa chadema ndo maana magufuli aliwakatalia. Ila ingekuwa agenda ya madiwani wa CCM angewakubalia.
Vipi Kama magufuli angekubali kuwaongezea posho. Madiwani wa CCM wangekubali au wangekataa.?
 
kamwe madiwani wa ccm wa sasa hawana uchu huo wa posho ndio maana hukusikia wakisusia vikao.
 
sandu77

Member
Oct 3, 2017
57
125
kama chadema wamewashinikiza hao ccm kumbe madiwani wa chadema wananguvu kushinda wa ccm kwa ninavyojua mm madiwani wa ccm ni wengi kuliko wa chadema iweje ajendayao ipite mpaka ikamufikie mkulu tena ikawa agenda ya madiwani wote nchi zima sjui hata na ww mleta maada kama umeleta kwaajili ya kulijadili tupate ufumbuzi kama hujalileta kwa mlengo kujipendekeza upate uteuzi mwenzio kakosa kaamua kuitoa hoja binafsi ya kuongezwa muda wa utawala wa raisi kisa kakosa uwaziri.
 
HELA

Senior Member
May 10, 2015
188
250
Bila shaka yoyote na kwa kujikumbusha matukio kadhaa ni wazi kuwa ajenda ya madiwani kutaka kuongezewa posho ilikuwa ni ajenda iliyopenyezwa na madiwani wa Chadema.
Ajenda hii ilikuwa ni ajenda mbaya ya kuwaabisha madiwani ambao wanatakiwa kuwa karibu na wananchi na kuibua shida za wananchi au kutoa mapendekezo kwa serikali kuu jinsi ya kuboresha maisha ya wananchi wa hali ya chini na sio kutaka kunenepesha matumbo yao.

Tunakumbuka mkuu wa mkoa wa Arusha na mkurugenzi wa jiji la Arusha alivyotukanwa na madiwani wa chadema wakiongozwa na Lema kisa kukata kiwango cha posho cha madiwani.
Tunakumbuka pia madiwani wa Meru walivyosusia vikao katika halmashauri hiyo kisa kupunguzwa kwa posho.

Pia wapo madiwani wa manispaa ya Moshi ambao waligomea mafunzo ya uwezeshaji yaliyoandaliwa na Tamisemi kisa posho.

Mifano hii inaashiria kuumizwa sana kwa madiwani wa chadema kutokana na punguzo la posho.Imagine diwani wa Arusha alikuwa analiliia kulipwa posho ya nauli sh 100000 ilihali nauli ya tax haizidi elfu tatu.

Hakuna shaka ushawishi wa madiwani hawa katika mkutano wa ALAT ukipelekea kumtega Magufuli awaingezee posho.

Kwa kuwa Magufuli ni mzalendo na amedhamiria kutuokoa kutoka makucha ya wanasiasa waroho alikataa wazi wazi na bila kumung'unya neno,hasira ya kukataliwa kwa ajenda ilipelekea upotoshaji wa kauli ya Rais na mjadala ukahamishiwa kwenye nyongeza ya mishahara.

Ni vyema tujadili na kujua nini kitafuata baada ya Magufuli kukataa ombi hili la madiwani wa chadema lililowasilishwa kwa mdomo wa AlAT.

JE WATASUSIA VIKAO?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom