Bila rushwa hupati cheti cha Kifo au Kuzaliwa RITA mkoani Arusha

Bukene

Member
May 27, 2016
59
125
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza ni kwamba kupata cheti cha kuzaliwa au kifo kutoka ofisi ya kutoa vyeti hivyo (RITA) Mkoani Arusha ni shughuli kubwa sana.

Ukifika mara ya kwanza unakuta foleni ndefu ya ajabu. Ukifanikiwa kuwakuta watendaji unapewa namba ya kulipia (Kontro namba)
ukisha lipia ndio utaambiwa njoo baada ya wiki tatu. Ukirudi baada ya wiki tatu unakuta mazingira ya mlundikano wa watu ni vilevile,
inakuchukua siku nzma nyingine kufanikiwa kuwakuta wahusika.

Ukiwakuta wahusika wanakuambia cheti husika hakionekani ndio imetoka hivyo, hapo ni wewe ujiongeze kama unaharaka uwaone kwa njia inayoitwa kujiongeza.

Imekuwa ni jambo la kawaida kabisa pale ofisi za RITA Arusha kuambiwa njoo baada ya wiki moja, nk kumbe kinachotakiwa ni RUSHWA

Cha ajabu ofisi hizi za RITA zipo jengo moja na ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Arusha lakini mambo ya ajabu na kutesa wananchi yanafanyika

Ni lini wananchi watapata huduma ya bila kutakiwa kutoa RUSHWA kwa watu walioajiriwa na kulipwa kwa KODI zetu?
 

black sniper

JF-Expert Member
Dec 10, 2013
17,047
2,000
Hapo dawa ni mabango tu akija Rais ili watimuliwe hao wanaojiita wakuu
Rushwa kuondoka ni ngumu ila kama watakaza itapungua
 

Vicky-Abelly

Member
May 27, 2016
72
125
Pale ofisi za RITA Arusha kuna sijui ni wasichana au wamama kazi yao kubwa ni kula rushwa na kujibu wateja wasioweza kujiongeza mbovu tu

Kama Kamanda wa TAKUKURU atapata ujumbe huu anaombwa kutupia jicho pale. Pameharibika sana kwa rushwa na kusumbua raia kwa kuambiwa njoo wiki ijayo bila kupata vyeti vyao.
 

Ikombabhuki

Member
Jan 17, 2021
79
150
Yaani Arusha Rita ni uozo mtupu, wale wabibi wanajion bado wasichana wamejaa dharau na kiburi! Njoo baada ya wiki tatu! Wananikeraaaaa! Rushwa tu zimewajaa vichwani. Nimetelekeza cheti cha mtoto pale kwa ujinga wao huu! Nitakiendea wakistaafu wabibi wale
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom