Bila mshikamano wa kweli tanzania tuitakayo itakuwa ndoto kuiona | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bila mshikamano wa kweli tanzania tuitakayo itakuwa ndoto kuiona

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by sammosses, Aug 25, 2012.

 1. sammosses

  sammosses JF-Expert Member

  #1
  Aug 25, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,205
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Bila mshikamano wa kweli Tanzania tuitakayo itakuwa ni sawa na ndoto za Alinacha.Tutaimba sana amani na umoja lakini haki bila wajibu au wajibu bila haki ndiyo silaha pekee ya kuvunja umoja wetu wa kitaifa ulioasisiwa na Mwalimu J K nyerere.

  Watawala wamepata mashaka juu ya kuvunjika kwa umoja wetu wa kitaifa,lakini wakashindwa kutambua kila mbegu bora uipandayo na kuimwagilia vizuri lazima itamea juu ya ardhi.Mbegu iliyopandwa na kumwagia vizuri ya ukabila,udini na ukanda ilikuwa kama wimbo wa taifa katika kipindi cha uchaguzi kwa kuwagawa na kusahau misingi bora ya utaifa iliyosimikwa na viongozi wetu wa awali.

  Mshikamano huu leo hii unazidi kushika kasi ya kuvunjika kutokana na kudharauliana na kupuuzana katika ya mtu mmoja hadi mtu mwingine.Kupuuzana huko ndiko kulikopelekea watawala wetu kutunyang'anya ardhi na kuwapa wageni kwa bei sawa na bure. Mshikamano huu uliovunjika ndiyo uliopelekea watawala kutothamini umoja wetu wa kitaifa na kuamau kufisidi mali za umma kwa maslahi ya wachache na familia zao.

  Serikali moja inatoa kauli pingamizi mbili kama vile hawakai pamoja na kuamua mambo yao pamoja.Leo utasikia rais ana sema hivi baadae kidogo kauli ile ile itapingwa na waziri mkuu ambao wote ni wa serikali ya chama kimoja. Serikali hiyo hiyo ndiyo yenye kuruhusu ndege za kijeshi za taifa jingine kupitia ikulu kutua ndani ya anga la Tanzania na kuchukua wanyama wetu bila kufuata taratibu na serikali hiyo hiyo kujifanya kipofu juu ya sinto fahamu ya sakata hilo.

  Wananchi wamepoteza mshikamano kiasi cha kuamua kurubuniwa na kuuza haki yao ya kuchagua viongozi wawatakao kwa kuuza vipande vyao vya kupigia kura na kukosa ile haki ya kikatiba ya kumchagua wamtakaye.

  Umoja wetu ambao tuliishi kijamaa bila kujali itikadi zetu leo umebadilika na udini kuchukua nafasi yake. Mapigano ya kikabila nayo yameshika kasi,wafugaji na wakulima wana nyukana,Watanzania wanaitwa wavamizi katika ardhi yao ilihali wageni wakipewa hifadhi na kulindwa kama miungu watu ndani ya taifa linalo amini kuwa ni nchi ya amani.

  Wageni toka China wakiendelea kuwashambulia raia wetu na kupewa kinga na vyombo vyetu vya dola kwa kuwa tu wamepewa mlungula ama kishika tumbo. Kuvunjika kwa mshikamano na umoja wa kitaifa umesababisha maadili ya jamii kupotea na taifa kuingia katika mfumo wa kimagharibi na kuwakumbatia wa magharibi na kusahau mila na desturi za kitanzania.

  Tusipokuwa kuwa wakweli kwa kufumbiana macho na kuendekeza tabia ya kulindana itasababisha hali ya amani ndani ya nchi yetu kupotea kabisa kwa kujenga chuki miongoni mwetu.

  Ni bora tutafute njia muafaka wa kutatua matatizo yetu yanayo sababisha mshikamano huu na umoja wa kitaifa kupotea,tafakari!!!!
   
Loading...