Bila mashtaka ya ununuzi wa Airbus 320 mnatuzuga! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bila mashtaka ya ununuzi wa Airbus 320 mnatuzuga!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Nov 23, 2011.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Nov 23, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,376
  Trophy Points: 280
  Suala la ununuzi wa magari ya ATCL tumeliandika sana hapa tangu mwanzo na kuweka ushahidi wote wa nani alikuwa na gari gani na alilipata vipi na tuliweka mikataba ya ununuzi wa magari yale. Angalau sasa kidogo wamefuatilia jambo hili. Hata hivyo kashfa kubwa zaidi ATCL ilikuwa ni ya ununuzi wa Airbus 320 ununuzi ambao umeliletea taifa hasara kubwa zaidi kuliko huo wa magari. Sasa kama TAKUKURU na vyombo vingine havitaleta mashtaka kwenye hili tutaona ni geresha tu.

  Ununuzi wa Airbus ndio uliogubikwa na ukiukwaji mkubwa sana wa kanuni zote za manunuzi ya umma, na kama tulivyoonesha umelisababishia taifa gharama kubwa na ulisaidia sana kulizamisha shirika hilo hata kuondoa uwezekano wote wa kuweza kufufuka na kuwa shirika la kisasa.

  Kwa hiyo, bila kuleta mashtaka dhidi ya wahusika wote - wakitaka vielelezo vyote vipo humu humu - itakuwa ni kuwadanganya watu. NI kuchezea hisia za Watanzania kwani makosa waliyoshtakiwa nayo hayalingani kabisa na mambo ambayo waliyasababisha ATCL.

  Thats all..
   
 2. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #2
  Nov 23, 2011
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,066
  Trophy Points: 280
  Kwenye nchi yetu hii 'mazingaombwe' mengi mno! Hiyo kesi unaweza kuta ni 'ulaji mwingine' kwa 'watu wengine' na haitafika popote pa maana.
   
 3. SHERRIF ARPAIO

  SHERRIF ARPAIO JF-Expert Member

  #3
  Nov 23, 2011
  Joined: Aug 25, 2010
  Messages: 7,081
  Likes Received: 1,814
  Trophy Points: 280
  Mzee Mwanakijiji umenena!
  Inawezekana keshamhonga tailor-made suits raisi wa nchi
   
 4. l

  limited JF-Expert Member

  #4
  Nov 23, 2011
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 300
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  ii nchi bwana kila kukicha wizi wa mali ya umma unakuwa bold kiasi cha kutisha sasa hawana hata haya
   
 5. SOBY

  SOBY JF-Expert Member

  #5
  Nov 23, 2011
  Joined: Sep 19, 2011
  Messages: 1,265
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  When it comes to investigative reporting, I always compare you to Matt Taibbi of The mighty"Rolling Stone Magazine".
  So why don't you break it down for us in Kijarida?
   
 6. Keynes

  Keynes JF-Expert Member

  #6
  Nov 23, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 498
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Serikali na taasisi zake ifike mahala wawe wanachukua hatua za mapema pale tatizo linapotokea ....ilikua haina sababu ya kusubiri shirika life kabisa ndo wakamshtaki kiongozi.
  NOW KESI ITACHUKUA MUDA NA GHARAMA NYINGI TU za kuhuni huni.
   
 7. m

  muchetz JF-Expert Member

  #7
  Nov 23, 2011
  Joined: Aug 16, 2010
  Messages: 496
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 45
  MM
  Mwendesha mashtaka ni presidential appointee
  Mwanasheria ni presidential appointee
  Jaji mkuu ni presidential appointee

  Hela aloiba imeliwa pia na watu walioko kwenye ring hiyo hiyo? What do u expect?
  Mi navyojua watakutana ili kuweka mambo sawa, Mshitakiwa ataambia akubali kiasi kidogo cha udhalilishaji(a bit of degradation), Mwendesha mashtaka tunga mashtaka yanayokaribiana na ukweli kwa karibu lakini kisheria yawe mbali na ukweli, Mwanasheria achaguliwe yule wa shule ya kata and finally Jaji awe mkali sana na ubabaishaji wa mwendesha mashtaka na mwanasheria.

  In all that confusion mtaona kama vile wanapigana, changanyana, hawaelewani e.t.c halafu jama anaachiwa huru kwa ushahidi dhaifu. Kuna baki na wapiga makofi, walo nuna, kasirika e.t.c all of it confusion. In meantime wao wako kwenye deal ingine.

  That is Tanzania (today), that is the Government and that is CCM. Just create confusion

  PERIOD.
   
 8. SHERRIF ARPAIO

  SHERRIF ARPAIO JF-Expert Member

  #8
  Nov 23, 2011
  Joined: Aug 25, 2010
  Messages: 7,081
  Likes Received: 1,814
  Trophy Points: 280
  Hata mtuhumiwa ni presidential appointee!!
  Hii kesi ni kiini macho tu bora wangei-dismiss
   
 9. only83

  only83 JF-Expert Member

  #9
  Nov 23, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  Serikali ya CCM inafanya kitu kimoja kwa watanzania...inatuvuruga na kutupoteza kwenye malengo ya msingi...haiwezekani wanafahamu sababu ya kufa kwa hili shirika muda mrefu sana lakini hawana dhamira ya dhati kuwaadibisha wanaofanya ujinga huu...wanasubiria kuwaadibisha dagaa halafu mapapa bado wanakula raha mtaani....kwa vyovyote vile tutegemee mengi sana kwenye hizi mahakama zetu,lakini yasiyo na tija kwa taifa..mtasikia mkurugenzi wa shirika ***** mara ***** halafu watu kama Ngeleja na Malima na wengine walioitia Taifa hasara wanapeta...mfano mawaziri waliokuwa madarakani wakati ATCL inakufa wako wapi? wanafanya nini? Je wameojiwa? Haya ndio maswali ya kujiuliza..vinginevyo mimi nasema CCM ni chama kinachopaswa kutoaminika kwasasa....
   
 10. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #10
  Nov 23, 2011
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,312
  Likes Received: 1,783
  Trophy Points: 280
  This problem was seen even before it happened.As usual kulindana na kuleta masarau ndio kunatupelekea kupata hizi hasara kubwa zisizoweza elezeka. Lini tutakua na kuanza kufanya mambo kama watu wazima tunaojua tunafanya nini? Nani kasema ukifanya kazi za umma ndio una immune ya kufanya lolote unalotaka bila kuwajibishwa? Hivi kweli kama Taifa tunapenda kuona viongozi wetu wakubwa wakidhalilishwa baada ya kumaliza muda wa madaraka yao?
  Aibu kweli!!
   
 11. Mlangaja

  Mlangaja JF-Expert Member

  #11
  Nov 23, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 541
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Sina matumaini na chochote kinachofanywa na magamba. Naona ni heri tukaiharibu kabisa nchi na kuanza upya. Hakuna tunachofanya. Upuuzi umezagaa kila mahali. Haiwezekani hata siku moja nchi kupiga hatua kwa ujinga huu unaoendelea. Hivi nani kawaloga hawa viongozi wetu. Katiba ambayo ingeziba mianya ya matitizo haya imechakachuliwa sasa tufanye nini? Kwangu naona tuibomoe kabisa nchi hii na baada ya hapo tuanze upya.
   
 12. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #12
  Nov 23, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Ati analia.....

  [​IMG]
   
 13. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #13
  Nov 23, 2011
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,625
  Likes Received: 1,381
  Trophy Points: 280
  only in tanzania is this possible!
   
 14. S

  Sheba JF-Expert Member

  #14
  Nov 23, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 210
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mwanakijiji,

  Yuko Mwanafalsafa mmoja aliyewahi kusema kuwa, "Ujinga wetu si mkubwa kuliko kushindwa kwetu kutumia kila tunachokijua". Kwa maana nyepesi, tunakuwa wajinga zaidi si kwa kuwa hatujui mambo mengi, ila kwa kuwa hatuwezi kutumia hata ujuzi wa machache tuliyonayo kujiendeleza.

  Falsafa hii nimeikumbuka wakati nikisoma thread yako. Naungana na wewe juu ya uchungu tulio nao kwa kusikia tunaibiwa kila siku na viongozi, hali na sisi wananchi tukiiba kidogokidogo kutokana na uwezo wetu mdogo wa kufikia rasilimali kubwa. Tunaagiza magari kisha tuna-undervalue bei ili kukwepa kodi, tunanunua bidhaa bila kudai risiti etc.


  Sasa tumetumbukia kwenye mtego wa kulala na kuamka tukitafuta ufisadi mpya ili tuliwaze nyoyo zetu kwa kulaani wengine. Naamini hili halitufikishi mbali. Na mbaya zaidi, tunapoteza nguvu nyingi kwenye kupambana na wezi ambao wametuibia sehemu ndogo sana ya utajiri wetu kwa gharama ya kuacha kutumia nguvu zetu kubuni mbinu za kutumia rasilmali nyingi zaidi tulizobaki nazo, na hivyo tunatoa mwanya kwa mafisadi kuendelea kutuibia.

  Mimi naamini, kwa dhati kabisa, tunahitaji mwafaka wa kitaifa. Laiti tungechora mstari na kuanza kusimamia rasilimali zilizopo tunaweza kusonga mbele zaidi. Kiasi tulichoibiwa ni kidogo sana ikilinganishwa na utajiri wa nchi hii. Lakini kadiri tunapopoteza muda kuhangaika na kiduchu tulichoibiwa, tunajisahau na kuacha rasilimali nyingi zilizopo nazo kuliwa na mafisadi. Wanantutengenezea richmond, badala ya kumalizana nalo mara moja tunahangaika nalo weeeeeeee tukija kukurupuka tunakuta kumbe mule walishahama wameshatula kwenye mradi wa bomba la gesi.

  Nchi hii imeibiwa rasilimali zake toka enzi za ukoloni na bado haijaishiwa. Sisi ni matajiri sana. Hatuna budi kuelekeza nguvu zetu kudhibiti na kutumia hichi tulichonacho badala ya kukimbizana na kiduchu kilichopopolewa na wachache. Ufisadi uko Asia na ulaya tena mkubwa zaidi kuliko uliopo sasa hapa nchini. Nchi inajengwa na fedha haijalishi ni safi au chafu. Marekani, ulaya na Asia zimejengwa kwa fedha safi na chafu. Tatizo hapa kwetu, wanaotuibia hawawekezi katika uchumi wetu, pia hawawekezi katika mambo ambayo yanafaida kwa wananchi walio wengi. Hapa tunao bakhresa, naamini anatuibia au alituibia lakini amewekeza kwenye sekta ambayo manufaa yake yanafikia wengi. Ufisadi unaweza kutafsiriwa kama " stage of primitive accumulation of capital", kinachofanywa baada ya hapo na hiyo capital ndio tatizo. Pale ambapo wanawekeza katika umma si jambo baya, pale ambapo wanawekeza kwenye kupata mamlaka zaidi ya kushika dola na kuendeleza ukwapuaji mdio inakuwa tatizo na hatari.

  Makala hizi za mayowe zinatupumbaza tu, hazitusaidiiii.
   
 15. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #15
  Nov 23, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  Smile and wave ....................boyz! , just smile and wave acting cute and cuddly ! ni maneno ya Skipper kwenye cartoon ya "The penguins of Madagascar"
   
 16. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #16
  Nov 23, 2011
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Analia?
  Alipostaafu aliitisha press conference na kujitapa sana na hata kulaumu uongozi wa awamu ya tatu kuwa ulimchafulia jina kwa kumuondoa madarakani kule PPF!
  Atakoma kuringa!
   
 17. Zed

  Zed JF-Expert Member

  #17
  Nov 23, 2011
  Joined: Mar 28, 2009
  Messages: 359
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Mwanakijiji anakumbukumbu nzuri kuliko wengi wetu tunaosahau baada ya wiki mmoja tu! Sioni kwanini Mattaka ashtakiwe kwa ufisadi mdogo wakati ufisadi mkubwa kiasi hiki unafumbiwa macho. Ama huu ulikuwa na maslahi ya wakubwa? Tujikumbushe kidogo hapa:

  Tanzanian taxpayers are set to pay a Lebanese aviation company a total of Sh22.64billion ($12.58 million) for service that wasn't delivered, The Guardian on Sunday can reveal today.
  The amount, which is more than what the government gave Air Tanzania two months ago, is another instance of poor contracting signed by the national airline when former Chief Executive Officer David Mattaka was at the helm, and a Lebanese aviation firm, Wallis Trading Company Inc.
  While Mattaka was the CEO of ATCL, Andrew Chenge, a former Attorney General and now Bariadi East MP was the Minister for Infrastructure, during 2007 when the bogus contract was signed.

  Ironically, those responsible for the costly and dubious contracts walk freely as taxpayers feel the pinch, amid skyrocketing prices of basic commodities. In September this year, the government gave Sh16 billion as a bailout package for the troubled national airline, ATCL. The allocated money however, is yet to be released by the Treasury.
  The $12.5 million which is due to be paid is the leasing cost for Airbus 320 -214 for the past 34 months where the plane was grounded, The Guardian on Sunday has established.
  Reliable sources from ATCL and within the Treasury confirmed to The Guardian on Sunday about the hefty payments to be paid to a Lebanese company anytime soon.
  They told The Guardian on Sunday at different moments this week that there was a push to have the payments made soon, though there was opposition on the legitimacy of the massive payments.
  The said aircraft, A320-214 was leased from Wallis Trading in October 2007 but in a questionable set of circumstances it was immediately grounded for major technical maintenance in France, where it remained there for seven months until May 2008, when it was deployed to fly the Dar- Johannesburg route.
  Officials of the Ministry of Communications and Transport as well as the Treasury disclosed to this paper: "This aircraft operated for seven months from May to December 2008 but as per agreement the lease bill of $370,000 a month begun to accumulate right away from the date of signing that agreement and no difference on that bill regarding the period the aircraft was operational or grounded for maintenance."
  Thus the government is compelled to cater for $15.17 million for lease fee of non-operational aircraft, used for seven months out of 48 months of the lease period from 9th October 2007 to 27th October 2011, when the aircraft was officially released by ATCL to the leaser - Wallis Trading.
  "The contract lease agreement was for a duration of six years and since the aircraft has been released before completion of the agreed period, the government is also responsible for paying compensation in view of that early termination of the agreement, bringing the total amount of money to be paid to Wallis to more than $32million (Sh57 billion)".
  The Gurdian on Sunday has established that the exact amount due to be paid is $32,659,316.12.
  It has also been established that although there are some government officials posing serious questions on the authenticity of the accumulated debt, several senior officials at the Ministry of Transport and Finance were ready to see the payment effected soon.
  An independent expert in the airline business told this paper that the market value of leasing aircraft like the one leased by ATCL could not go higher than $250,000 a month and wondered as to why the operational and non-operation leasing bill remained the same.
  "During maintenance period the aircraft is entirely rested therefore there is no operational cost, how comes then the charges remain the same. This is a straight forward point; what I know is that the cost could have been renegotiated and brought down to about $30,000 a month when the plane was on the ground. A contract like this is a poor one," the expert intoned.
  Due to the fact that ATCL was once partly privatised to South African Airways which had bought 49 percent of ATCL shares back in 2002, negotiations for the debt payment also included the Consolidated Holding Corporation (CHC), which oversees all state owned firms earmarked for divestiture. As it stands it is a matter of time before the staggering amount of money could be fully paid to the leaser-Lebanese Company as it only awaits the signature of the Permanent Secretary at the Ministry of Finance.
  One the key paragraphs in aircraft (Airbus 320-214) release agreement reads: "……Additionally a lump-sum of compensation is payable to the leasing firm for early termination and for failure by the lessee to deliver the aircraft in the condition required under schedule 3 paragraph 6 and (10-13) of the lease agreement.
  The Other Cost remain outstanding (OA) and TA amount and the period of other terms for payment have been agreed today between us, you, the Ministry of finance and Technical Committee, appointed by the government-CHC subject to the letter signed by the Permanent Secretary of Finance as per the discussion between him and Wallis at the ministry on October 27th 2011 at 9.30."
  And as the government prepares to pay $32.6 million accrued from leasing the aircraft, The Guardian on Sunday has been reliably informed that the same plane was sold by Wallis Trading to Zimbabwe at $16 million, less than 50 percent of lease bill payable by Tanzania.
  Also according to an official document at the Ministry of Transport and CHC the airbus debt forms more than half of the total ATCL debt which by end of October 2011 stood at Sh90 billion. Total Airbus 320 – 214 lease debt is Sh57 billion.
  The said aircraft was leased in 2007 in the preparation for a second divestiture of ATCL, to be partly sold to the Chinese company Sonangol, which never signed a formal contractual agreement with the Government but had pledged to buy ATCL not less than five Airbus aircraft by 2012.
  In line with the then eagerly awaited ATCL take-over by Sonangol, the ATCL management rushed to obtain lease of the A320-214 from Wallis Trading, a company said to have a close working relationship with Sonangol.
  The plane operated in Liberia on a lease basis and then leased to South American state of El Salvador, the sources indicated.
  By the time Tanzania entered into lease agreement in October 2007 the aircraft was due to go for a major technical maintenance, known as ‘Check C' plus 12 years but that fact was only established after the agreement was penned leading to the aircraft be grounded in France for seven months.
  Experts inside the troubled airline had earlier advised ATCL management to instead acquire a Boeing 737-300, which consumes 15 percent less fuel than an A320 but it carries 128 passengers unlike A320 which has a 150 seat capacity.
  To start with, the 737-300 would have been suitable to operate regional and domestic routes, considering the current business outlook for ATCL, in the view of an ATCL official.
  The two aircraft have similar types of engines but the 737-300 has less power than the A320.
  Since ATCL has already been operating the Boeing 737-200, it would have been cheaper and easy for the latter to adjust to the 737-300 in terms of training and developing the same calibre of pilots and engineers familiar with Boeing technology.
  Air Tanzania Company Limited (ATCL), a limited liability company, was established under the Companies Act to take over the operating assets, and specified rights and liabilities of ATC, as well as the creation of a new company, Air Tanzania Holding Company (ATHCO), to take over the non-operating assets and all other liabilities of ATC.
  South African Airways was the winning bidder and in December 2002, after signing an agreement with the government, it bought a 49 per cent stake in ATC for $20m, of which $10m was the value of the shares and the remaining $10m for the capital and training account for financing its proposed business plan.  SOURCE: GUARDIAN ON SUNDAY

   
 18. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #18
  Nov 23, 2011
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,066
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo mkuu, kama nimekuelewa vema, unataka tuendelee kuwekeza kwenye ATCL na tusihangaike na wanaokwapua? Hii si inaweza kuwa sawasawa na kujaribu kujaza maji kwenye pipa lililotoboka na huku wengine wakiendelea kuongeza matundu? Tutafanikiwa kulijaza hilo pipa?
   
 19. Ngisibara

  Ngisibara JF-Expert Member

  #19
  Nov 23, 2011
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 2,083
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 180
  Nyie mwataka haki huku Mwenzenu afurahia kuwa na kesi iliyopangwa ikapangika kama ilivyotakiwa

  [​IMG]
   
 20. PatPending

  PatPending JF-Expert Member

  #20
  Nov 23, 2011
  Joined: Aug 17, 2007
  Messages: 490
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Ni ununuzi au ukodishaji wa Airbus 320?
   
Loading...