Bila maamuzi magumu tusitegemee maendeleo Tanzania

Joblube

JF-Expert Member
Mar 4, 2011
369
151
Moja ya nchi zilizo barikiwa kuwa na rasilimali nyingi zinazoweza kutuleta maendeleo ni Tanzania, tunazo mbuga za wanyama, tunayo maziwa, tunayo madini (Dhahabu, Almasi, chumvu, makaa ya mawe,ulanga, chuma, industrial minerals zote na mengine mengi), tunayo bahari ambao kijografia tulipo tulipaswa sisi ndio tunufaike na biashara na nchi zisizo na bahari lakini wapi Kenya ndio wananufaika zaidi.

Mashirika yale yalioanzishwa na Baba wa Taifa hili la Tanzania kama (Ndege, Reli, Bandari, viwanda vya urafiki, sungura tex yapo hoi na mengine yamekufa hapa kuna tatizo. Watanzania kwa uhalisia wao ni watu tumebarikiwa kiakili kwa hili hakuna ubishi nenda kwa nchi za wenzetu ambapo watanzania wanafanya kazi ni watu wanaoaminiwa sana karibu katika nyanja zote. Sasa jiulize kwanini tunarasilimali nyingi, tunawataalamu wazuri tuu lakini tupo hapa tulipo (lipo tatizo nitaeleza).

Nchi ya Korea ya Kusini haina rasilimali nyingi kama tulizonazo sisi ,wao wanaagiza karibu kila kitu kutoka nje lakini ni miongoni mwa nchi zenye kuzalisha magari na meli duniani pamoja na kiagiza chuma kutoka nje. Ndugu zanga watanzania historia inatuonyesha wenzetu wa Korea ya Kusini walifanya maamuzi magumu. Rais wa nchi hiyo Park alipoingia madarakani mwaka 1962 alikuwa na vision na vipaumbele vitano tuu Elimu, ICT,Nishati,Viwanda na kingine nimekisahau. Wakati huo uchumi wa Korea ya kusini ulikwa sawa na Watanzania lakini leo hii Korea ya Kusini ni moja ya nchi zenye uchumi imara dunia kwa nini commitment and vision.

Nimeeleza hayo yote kuonyesha kuwa bila kuwa na uongozi wenye maono usiotafuta faida yake wenyewe na kwa wanaomzunguka hatuwezi kutoka hapa tulipo, tutaendelea kufurahia vimafanikio visivyo na maana pana. Historia inaonyesha Rais Park aliingia madarakani kwa kupindua uongozi (Mungu pishilia mbali isiwe hivyo kwa Tanzania) kwa msingi huo alikuwa free kutekeleza yale aliyoyamini hakukuwa msukumo kutoka kwa wa poembeni.

Ndugu zangu tatizo letu sisi ni mfumo tulionao ndani ya CCM, mfumo huu hauwezi kutupatia Rais aliyehuru, na hata akipatikana mtu msafi atachanganyika na zaidi ya aslimia 50% ya viongozi maslai, atafurukuta kwa muda mwisho atakuwa poluted mfano mzuri na Mh Benyamini Mkapa ambaye kwa kweli yeye alikuwa na nafasi nzuri kwa kuwa hakuingizwa na kikundi cha watu bali nguvu ya Baba wa Taifa lakini ameishia wapi aliingia kwa mbwembe na kutangaza mali zake na kweli kwa wakati huo alikuwa na dhamira ya kweli wala isiyo ya kinafiki lakini muda si muda akamezwa na mfumo sidhani kama alivyotoka madarakani alituambia ana mali kiasi gani(athari za mfumo CCM). Tunamlaumu Mh Rais Kikwete bure tazama ameingiaje madarakani kamwe hawezi kuwa huru tutaendelea kutwanga maji kwenye kini.

Nini kifanyike kwa maoni yangu maamuzi magumu yafanywe na Watanzania lije jua ije mvua CCM ipumzike kwanza kwa amani. Halafu tumtafute mtu nje ya CCM na hasa CHADEMA ambao wamejipambanua kuwa wanaweza kwa sasa hata kwa kuwatizama vinginevyo tutaendelea kulia mwaka hata mwaka.

Mungu Ibariki Tanzania
 
No, ulitakiwa kuwa na kichwa cha habari kinachosomeka"Bila kuwasambaratisha Freemasons hatuwezi kupata maendeleo Tanzania."

Back
Top Bottom